< 2 Samweli 20 >
1 Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mfanya fujo jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, “Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende nyumbani kwake, Israeli.”
Il se trouvait là un méchant homme, nommé Schéba, fils de Bichri, Benjamite. Il sonna de la trompette, et dit: « Nous n'avons pas de part en David, et nous n'avons pas d'héritage dans le fils de Jessé. Chacun dans sa tente, Israël! »
2 Hivyo watu wote wa Israeli wakamwacha Daudi na kumfuata Sheba mwana wa Bikri. Lakini watu wa Yuda wakamfuata mfalme wao kwa karibu sana, kutoka Yordani njia yote hadi Yerusalemu.
Et tous les hommes d'Israël cessèrent de suivre David et suivirent Saba, fils de Bichri; mais les hommes de Juda se rallièrent à leur roi, depuis le Jourdain jusqu'à Jérusalem.
3 Daudi alipofika katika kasri lake huko Yerusalemu, akawachukua masuria aliokuwa amewaacha kulitunza kasri, na akawaweka katika nyumba chini ya uangalizi. Aliwaandalia mahitaji yao lakini hakulala nao tena. Hivyo walikuwa wametengwa hadi siku ya kufa kwao, waliishi kama wajane.
David arriva dans sa maison à Jérusalem; et le roi prit les dix femmes de ses concubines, qu'il avait laissées pour garder la maison, et les mit sous tutelle; il leur donna de la nourriture, mais il n'entra pas chez elles. Elles restèrent ainsi enfermées jusqu'au jour de leur mort, vivant dans le veuvage.
4 Kisha mfalme akamwambia Amasa, “Uwaite watu wa Yuda ndani ya siku hizi tatu; wewe pia uwepo hapa.”
Et le roi dit à Amasa: « Convoque-moi les hommes de Juda d'ici trois jours, et sois ici présent. »
5 Hivyo Amasa akaenda kuwaalika watu wote wa Yuda kwa pamoja, lakini akatumia muda mrefu kulika mfalme alivyokuwa amemwamuru.
Amasa alla donc convoquer les hommes de Juda, mais il resta plus longtemps que le temps qui lui avait été fixé.
6 Hivyo Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatufanyia madhara zaidi ya Absalomu. Chukua watumishi wa bwana wako, askari wangu, na umfuatie asije akaingia katika mji wenye ngome na kututoroka.”
David dit à Abishai: « Maintenant, Saba, fils de Bichri, nous fera plus de mal qu'Absalom. Prends les serviteurs de ton seigneur et poursuis-le, de peur qu'il ne se procure des villes fortifiées et ne se dérobe à nos yeux. »
7 Ndipo watu wa Yoabu wakamfuatia, pamoja na Wakerethi na Wapelethi na mashujaa wote. Wakatoka Yerusalemu ili kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Les hommes de Joab partirent à sa suite, avec les Kéréthiens, les Péléthiens et tous les hommes forts, et ils sortirent de Jérusalem pour poursuivre Saba, fils de Bichri.
8 Walipokuwa katika jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa silaha ya vita aliyokuwa ameivaa, alikuwa pia na upanga uliokuwa umefungwa na mkanda katika kiuno chake. Kadili alivyoendelea mbele upanga ukadondoka.
Lorsqu'ils arrivèrent à la grande pierre qui est à Gabaon, Amasa vint à leur rencontre. Joab était vêtu de l'habit de guerre qu'il avait revêtu, et il portait une ceinture avec une épée attachée à sa taille dans son fourreau; et comme il avançait, elle tomba.
9 Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.
Joab dit à Amasa: « Est-ce que tu te portes bien, mon frère? » Joab prit Amasa par la barbe avec sa main droite pour l'embrasser.
10 Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakadondoka chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Mais Amasa ne prit pas garde à l'épée qui était dans la main de Joab. Celui-ci le frappa au corps, et répandit ses entrailles à terre; il ne le frappa plus, et il mourut. Joab et son frère Abischaï poursuivirent Saba, fils de Bichri.
11 Kisha mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa naye akasema, “Aliye upande wa Yoabu na aliyeupande wa Daudi na amfuate Yoabu.”
Un des jeunes gens de Joab se tenait près de lui et disait: « Que celui qui est favorable à Joab, et qui est pour David, suive Joab! »
12 Amasa akawa anagalagala katika damu yake katikati ya njia. Mtu yule alipoona kwamba watu wote wamesimama, akambeba Amasa na kumweka shambani kando ya njia. Akatupa vazi juu yake kwa maana aliona kila mmoja aliyekuja alisimamaa pale.
Amasa gisait, baignant dans son sang, au milieu de la route. Quand l'homme vit que tout le peuple s'arrêtait, il emporta Amasa hors du chemin dans les champs et jeta sur lui un vêtement, quand il vit que tous ceux qui passaient près de lui s'arrêtaient.
13 Baada ya Amasa kuondolewa njiani watu wote wakamfuata Yoabu katika kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Lorsqu'il fut retiré de la route, tout le peuple se mit à la suite de Joab pour poursuivre Saba, fils de Bichri.
14 Sheba akazipita kabila zote za Israeli mpaka Abeli wa Beth Maaka, na katika nchi yote ya Berite ambao pia walijikusanya pamoja pia na kumfuatia Sheba.
Il traversa toutes les tribus d'Israël, jusqu'à Abel, jusqu'à Beth Maaca, et tous les Berites. Ils se rassemblèrent, et marchèrent aussi après lui.
15 Walimpata na kumzingira huko Abeli wa Bethi Maaka. Wakajenga buruji ya kuhusuru mji nyuma ya ukuta. Jeshi lote lilokuwa pamoja na Yoabu likaugongagonga ukuta ili uanguke.
Ils vinrent l'assiéger à Abel, à Beth Maaca, et ils élevèrent contre la ville un monticule qui se dressait contre le rempart; tout le peuple qui était avec Joab frappait la muraille pour la renverser.
16 Ndipo mwanamke mwerevu akapiga kelele kutoka ndani ya mji, “Sikiliza, Yoabu, tafadhari sikiliza! Sogea karibu nami ili niongee nawe.”
Alors une femme sage cria de la ville: « Écoute, écoute! Dis à Joab: Approche-toi d'ici, que je te parle. »
17 Hivyo Yoabu akakaribia, mwanamke akamwambia, “Je wewe ni Yoabu? Akajibu, “ni mimi.” mwanamke akamwambia, “Sikiliza maneno ya mtumishi wako.” Akajibu, “Nasikiliza.”
Il s'approcha d'elle; et la femme dit: « Es-tu Joab? » Il a répondu: « Je le suis. » Puis elle lui dit: « Écoute les paroles de ton serviteur. » Il a répondu: « J'écoute. »
18 Ndipo aliposema,”Hapo zamani ilisemwa, 'Bila shaka tafuteni ushauri huko Abeli,' na kwamba ushauri huo utakata maneno.
Elle prit alors la parole et dit: « Autrefois, on disait: « On demandera conseil à Abel », et c'est ainsi qu'on a réglé une affaire.
19 Sisi ni mji ulio miongoni mwa miji yenye nguvu na aminifu sana katika Israeli. Mnataka kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kuumeza urithi wa Yahwe?”
Je suis de ceux qui sont pacifiques et fidèles en Israël. Vous cherchez à détruire une ville et une mère en Israël. Pourquoi voulez-vous engloutir l'héritage de Yahvé? »
20 Ndipo Yoabu alipojibu na kusema, “Iwe mbali, iwe mbali nami, hata nikameze au kuharibu.
Joab répondit: Loin de moi, loin de moi l'idée d'engloutir ou de détruire.
21 Hiyo si kweli. Lakini mtu kutoka katika nchi ya milima ya Efraimu, aitwaye Sheba mwana wa Bikri, ameinua mkono wake kinyume cha mfalme, kinyume cha Daudi. Mtoeni yeye nami nitauacha mji.” Mwanamke akamwambia Yoabu, “Utarushiwa kichwa chake kutoka juu ya ukuta.”
Il n'en est pas ainsi. Mais un homme de la montagne d'Ephraïm, nommé Schéba, fils de Bichri, a levé la main contre le roi, contre David. Délivre-le, et je quitterai la ville. » La femme dit à Joab: « Voici, on te jettera sa tête par-dessus la muraille. »
22 Kisha mwanamke akawaendea watu wote wa mji kwa hekima yake. Wakakiondoa kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumrushia Yoabu. Ndipo alipopiga tarumbeta na watu wa Yoabu wakauacha mji kila mtu nyumbani kwake. Na Yoabu akarejea Yerusalemu kwa mfalme.
Alors la femme alla vers tout le peuple dans sa sagesse. Ils coupèrent la tête de Saba, fils de Bichri, et la jetèrent à Joab. Celui-ci sonna de la trompette, et ils se dispersèrent hors de la ville, chacun dans sa tente. Puis Joab retourna à Jérusalem auprès du roi.
23 Yoabu alikuwa juu ya jeshi lote la Israeli na Benaya mwana wa Yehoiada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi.
Joab était à la tête de toute l'armée d'Israël; Benaja, fils de Jehojada, était à la tête des Kéréthiens et des Péléthiens;
24 Adoramu alikuwa juu ya watu waliofanya kazi ya shokoa na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mkumbushaji.
Adoram était à la tête des hommes soumis au travail forcé; Josaphat, fils d'Ahilud, était archiviste;
25 Sheva alikuwa mwandishi, na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.
Sheva était scribe; Tsadok et Abiathar étaient sacrificateurs;
26 Ira wa Yairi alikuwa mhudumu mkuu wa Daudi.
Ira, le Jaïrite, était chef des services de David.