< 2 Samweli 16 >
1 Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo.
大衛剛過山頂,見米非波設的僕人洗巴拉着備好了的兩匹驢,驢上馱着二百麵餅,一百葡萄餅,一百個夏天的果餅,一皮袋酒來迎接他。
2 Mfalme akamuliza Siba, “Kwa nini umeleta hivi vitu?” Siba akajibu, “punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili kunywa watakaozimia nyikani.”
王問洗巴說:「你帶這些來是甚麼意思呢?」洗巴說:「驢是給王的家眷騎的;麵餅和夏天的果餅是給少年人吃的;酒是給在曠野疲乏人喝的。」
3 Mfalme akauliza, “Na mjukuu wa bwana wako yuko wapi?” Siba akamjibu mfalme, “Tazama, yeye amesalia Yerusalemu kwa maana alisema, 'Leo nyumba ya Israeli itanirudishia ufalme wa baba yangu.”
王問說:「你主人的兒子在哪裏呢?」洗巴回答王說:「他仍在耶路撒冷,因他說:『以色列人今日必將我父的國歸還我。』」
4 Kisha mfalme akamwambia Siba, “Tazama, yote yaliyomilikiwa na Mefiboshethi sasa yatakuwa yako.” Siba akajibu, “Nainama kwa unyenyekevu kwako bwana wangu mfalme. Na nipate kibari mbele zako.”
王對洗巴說:「凡屬米非波設的都歸你了。」洗巴說:「我叩拜我主我王,願我在你眼前蒙恩。」
5 Mfalme Daudi alipokaribia Bahurimu, akaja mtu kutoka katika ukoo wa Sauli, jina lake Shimei mwana wa Gera. Kadiri alivyokuwa akitembea alikuwa akilaani.
大衛王到了巴戶琳,見有一個人出來,是掃羅族基拉的兒子,名叫示每。他一面走一面咒罵,
6 Akamrushia Daudi mawe na maofisa wa mfalme, bila kujali jeshi na walinzi wa mfalme waliokuwa kulia na kushoto mwa mfalme.
又拿石頭砍大衛王和王的臣僕;眾民和勇士都在王的左右。
7 Shimei akalaani, “Nenda zako, toka hapa, mwovu wewe, mtu wa damu!
示每咒罵說:「你這流人血的壞人哪,去吧去吧!
8 Yahwe amelipa yote kwa ajili ya damu ya familia ya Sauli, ambaye unatawala badala yake. Yahwe ameweka ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao. Na sasa umeangamia kwa kuwa ni mtu wa damu.”
你流掃羅全家的血,接續他作王;耶和華把這罪歸在你身上,將這國交給你兒子押沙龍。現在你自取其禍,因為你是流人血的人。」
9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, “Kwa nini mbwa mfu anamlaani bwana wangu mfalme? Tafadhari niache niende nikamwondolee kichwa chake.”
洗魯雅的兒子亞比篩對王說:「這死狗豈可咒罵我主我王呢?求你容我過去,割下他的頭來。」
10 Lakini mfalme akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya? Pengine ananilaani kwa kuwa Yahwe amemwambia, 'Mlaani Daudi.' Nani sasa awezaye kumwambia, 'Kwa nini unamlaani mfalme.”
王說:「洗魯雅的兒子,我與你們有何關涉呢?他咒罵是因耶和華吩咐他說:『你要咒罵大衛。』如此,誰敢說你為甚麼這樣行呢?」
11 Hivyo Daudi akamwambia Abishai na watumishi wake wote, “Tazameni, mwanangu aliyezaliwa kutoka katika mwili wangu anatafuta uhai wangu. “Si zaidi sana mbenjamini huyu akatamani anguko langu? Mwacheni alaani, kwa maana Yahwe amemwamru kufanya hivyo.
大衛又對亞比篩和眾臣僕說:「我親生的兒子尚且尋索我的性命,何況這便雅憫人呢?由他咒罵吧!因為這是耶和華吩咐他的。
12 Huenda Yahwe akaangalia maangaiko niliyofungiwa, na kunirudishia mema kwa jinsi nilivyolaaniwa leo.”
或者耶和華見我遭難,為我今日被這人咒罵,就施恩與我。」
13 Hivyo Daudi na watu wake wakaendelea njiani wakati Shimei kando yake ubavuni mwa mlima, aliendelea kulaani na kumrushia mavumbi na mawe huku akienda.
於是大衛和跟隨他的人往前行走。示每在大衛對面山坡,一面行走一面咒罵,又拿石頭砍他,拿土揚他。
14 Kisha mfalme na watu wake wote wakachoka, na akapumzika wakati wa usiku walipopumzika wote.
王和跟隨他的眾人疲疲乏乏地到了一個地方,就在那裏歇息歇息。
15 Absalomu na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye wakaja Yerusalemu na Ahithofeli alikuwa pamoja naye.
押沙龍和以色列眾人來到耶路撒冷;亞希多弗也與他同來。
16 Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, “Mfalme aishi daima! mfalme aishi daima.
大衛的朋友亞基人戶篩去見押沙龍,對他說:「願王萬歲!願王萬歲!」
17 Absalomu akamwambia Hushai, “Je huu ndiyo utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?”
押沙龍問戶篩說:「這是你恩待朋友嗎?為甚麼不與你的朋友同去呢?」
18 Hushai akamwambia Absalomu, “Hapana! badala yake, yule ambaye Yahwe, watu hawa na watu wote wa Israeli wamemchagua huyo ndiye nitakaye kuwa upande wake na ndiye nitakaye kaa naye.
戶篩對押沙龍說:「不然,耶和華和這民,並以色列眾人所揀選的,我必歸順他,與他同住。
19 Kwani ni nani ninayepaswa kumtumikia? Je sipaswi kutumika mbele za mwana? kama nilivyotumika mbele za baba yako ndivyo nitakavyofanya mbele zako”
再者,我當服事誰呢?豈不是前王的兒子嗎?我怎樣服事你父親,也必照樣服事你。」
20 Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako kuhusu tunachopaswa kufanya.”
押沙龍對亞希多弗說:「你們出個主意,我們怎樣行才好?」
21 Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Nenda ulale na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza kasri, na waisraeli wote watasikia kwamba umekuwa kitu kinachonuka kwa baba yako. Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu.”
亞希多弗對押沙龍說:「你父所留下看守宮殿的妃嬪,你可以與她們親近。以色列眾人聽見你父親憎惡你,凡歸順你人的手就更堅強。」
22 Hivyo wakatanda hema kwa ajili ya Absalomu juu ya kasri na Absalomu akalala na masuria wa baba yake mbele za Israeli wote.
於是人為押沙龍在宮殿的平頂上支搭帳棚;押沙龍在以色列眾人眼前,與他父的妃嬪親近。
23 Nyakati hizo ushauri aliokuwa akitoa Ahithofeli ulikuwa ni kama mtu anavyosikia kutoka katika kinywa cha Mungu mwenyewe. Hivyo ndivyo jinsi ushauri wa Ahithofeli ulivyoonekana kwa Daudi na Absalomu
那時亞希多弗所出的主意好像人問上帝的話一樣;他昔日給大衛,今日給押沙龍所出的主意,都是這樣。