< 2 Samweli 14 >
1 Yoabu mwana wa Seruya akatambua kwamba moyo wa mfalme ulitamani kumwona Absalomu.
洗鲁雅的儿子约押,知道王心里想念押沙龙,
2 Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwelevu. Akamwambia, “Tafadhari, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa.
就打发人往提哥亚去,从那里叫了一个聪明的妇人来,对她说:“请你假装居丧的,穿上孝衣,不要用膏抹身,要装作为死者许久悲哀的妇人;
3 Kisha ingia kwa mfalme na umwambiye maneno nitakayokueleza.” Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme.
进去见王,对王如此如此说。”于是约押将当说的话教导了妇人。
4 Wakati mwanamke kutoka Tekoa alipoongea na mfalme, aliinamisha uso wake chini na kusema,
提哥亚妇人到王面前,伏地叩拜,说:“王啊,求你拯救!”
5 “Mfalme, anisaidie.” Mfalme akamwambia, “Shida yako ni nini?” Akajibu, Ukweli ni kwamba mimi ni mjane, mme wangu alikufa.
王问她说:“你有什么事呢?”回答说:“婢女实在是寡妇,我丈夫死了。
6 Mimi, mtumishi wako, nilikuwa na wana wawili, wakagombana shambani, na hakukuwa na wa kuwaachanisha. Mmoja wao akampiga mwenziwe na kumwua.
我有两个儿子,一日在田间争斗,没有人解劝,这个就打死那个。
7 Na sasa ukoo wote umeinuka juu ya mtumishi wako, wanasema, 'Mtoe aliyempiga nduguye, ili tumwue kulipe uhai wa nduguye aliyeuawa.' Na hivyo watamwangamiza mrithi. Hivyo watalizima kaa liwakalo nililobakiwa, hata kumwondolea mme wangu jina na mzao juu ya uso wa nchi.”
现在全家的人都起来攻击婢女,说:‘你将那打死兄弟的交出来,我们好治死他,偿他打死兄弟的命,灭绝那承受家业的。’这样,他们要将我剩下的炭火灭尽,不与我丈夫留名留后在世上。”
8 Hivyo mfalme akamwambia mwanamke, “Nenda nyumbani kwako, nami nitaagiza jambo la kukufanyia.”
王对妇人说:“你回家去吧!我必为你下令。”
9 Mwanamke kutoka Tekoa akamjibu mfalme, “Bwana wangu mfalme, hatia na iwe juu yangu na juu ya familia ya baba yangu. Mfalme na kiti chake cha enzi hawana hatia.”
提哥亚妇人又对王说:“我主我王,愿这罪归我和我父家,与王和王的位无干。”
10 Mfalme akasema, “Yeyote atakayekwambia neno umlete kwangu, naye hatakugusa tena.”
王说:“凡难为你的,你就带他到我这里来,他必不再搅扰你。”
11 Kisha mwanamke akasema, “Tafadhari mfalme amkumbuke Yahwe Mungu wake, ili kwamba mlipa kisasi cha damu asiaribu zaidi, ili kwamba wasimwangamize mwanangu.” Mfalme akajibu, “Kama Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utaanguka chini.”
妇人说:“愿王记念耶和华—你的 神,不许报血仇的人施行灭绝,恐怕他们灭绝我的儿子。”王说:“我指着永生的耶和华起誓:你的儿子连一根头发也不致落在地上。”
12 Kisha mwanamke akasema, “Tafadhari acha mtumishi wako anene neno moja zaidi kwa bwana wangu mfalme.” Akasema, “Sema.”
妇人说:“求我主我王容婢女再说一句话。”王说:“你说吧!”
13 Hivyo mwanamke akasema, “Kwa nini basi umetenda kwa hila dhidi ya watu Mungu? Maana kwa kusema hivi, mfalme ni kama mtu mwenye hatia, kwa kuwa mfalme hamjamrudisha tena mwanaye aliyeondoka.
妇人说:“王为何也起意要害 神的民呢?王不使那逃亡的人回来,王的这话就是自证己错了!
14 Kwa maana sisi sote tutakufa, kwa kuwa tu kama maji yamwagwayo juu ya ardhi na kwamba hayawezi kukusanywa tena. Lakini Mungu hatachukua uhai; badala yake, utafuta njia kwa walio mbali kurejeshwa.
我们都是必死的,如同水泼在地上,不能收回。 神并不夺取人的性命,乃设法使逃亡的人不致成为赶出、回不来的。
15 Sasa basi, nimesema jambo hili kwa bwana wangu mfalme, kwa sababu watu wamenitisha. Hivyo mtumishi wako akajinenea nafsini mwake, 'Sasa nitaongea na mfalme. Huenda mfalme akampa mtumishi wake haja yake.
我来将这话告诉我主我王,是因百姓使我惧怕。婢女想,不如将这话告诉王,或者王成就婢女所求的。
16 Kwa maana mfalme atanisikiliza, ili kwamba kumtoa mtumishi wake katika mikono ya mtu ambaye angeniangamiza mimi na mwanangu pamoja, tutoke katika urithi wa Mungu.
人要将我和我儿子从 神的地业上一同除灭,王必应允救我脱离他的手。
17 Kisha mtumishi wako akaomba, 'Yahwe, tafadhari ruhusu neno la bwana wangu mfalme linipe msaada, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu kwa kutofautisha wema na ubaya.' Yahwe, Mungu na awe pamoja nawe.”
婢女又想,我主我王的话必安慰我;因为我主我王能辨别是非,如同 神的使者一样。惟愿耶和华—你的 神与你同在!”
18 Ndipo mfalme akajibu na kumwambia yule mwanamke, Tafadhari usinifiche neno lolote nikuulizalo.” Mwanamke akajibu, “Basi bwana wangu mfalme na aseme sasa.
王对妇人说:“我要问你一句话,你一点不要瞒我。”妇人说:“愿我主我王说。”
19 Mfalme akasema, Je siyo mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu na kusema, “Kama uishivyo bwana wangu mfalme, hakuna awezae kuelekea mkono wa kulia wala wa kushoto kwa yale bwana wangu mfalme aliyosema. Ni mtumishi wako Yoabu aliyeniambia na kuniagiza kusema kile mtumishi wako alichokisema.
王说:“你这些话莫非是约押的主意吗?”妇人说:“我敢在我主我王面前起誓:王的话正对,不偏左右,是王的仆人约押吩咐我的,这些话是他教导我的。
20 Mtumishi wako Yoabu amefanya hivi ili kubadilisha hali ya kile kinachotendeka. Bwana wangu ni mwenye akili kama hekima ya malaika wa Mungu, ajuaye yote yatendekayo ndani ya nchi.”
王的仆人约押如此行,为要挽回这事。我主的智慧却如 神使者的智慧,能知世上一切事。”
21 Hivyo mfalme akamwambia Yoabu, “Tazama, nitatenda jambo hili. Nenda na umrudishe huyo kijana Absalomu.”
王对约押说:“我应允你这事。你可以去,把那少年人押沙龙带回来。”
22 HivyoYoabu akainamisha uso wake chini juu ya ardhi katika heshima na shukurani kwa mfalme. Yoabu akasema, “Mtumishi wako amejua kwamba amepata neema mbele zako, bwana wangu, mfalme, kwa vile mfalme amempa mtumishi wake haja ya moyo wake.
约押就面伏于地叩拜,祝谢于王,又说:“王既应允仆人所求的,仆人今日知道在我主我王眼前蒙恩了。”
23 Hivyo Yoabu akainuka na kwenda Geshuri, akamrejesha Absalomu Yerusalemu tena.
于是约押起身往基述去,将押沙龙带回耶路撒冷。
24 Mfalme akasema, “Na arudi nyumbani kwake, lakini hasinione uso wangu.” Hivyo Absalomu akarudi katika nyumba yake mwenyewe, na hakuweza kuuona uso wa mfalme.
王说:“使他回自己家里去,不要见我的面。”押沙龙就回自己家里去,没有见王的面。
25 Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu. Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote.
以色列全地之中,无人像押沙龙那样俊美,得人的称赞,从脚底到头顶毫无瑕疵。
26 Alipokata nywele za kichwa chake mwishoni mwa kila mwaka, kwa sababu zilikuwa nzito juu yake, alipima nywele zake zaidi ya shekeli mia mbili, kwa kiwango cha kipimo cha mfalme.
他的头发甚重,每到年底剪发一次;所剪下来的,按王的平称一称,重二百舍客勒。
27 Kwake Absalomu walizaliwa wana watatu na binti mmoja, jina lake Tamari. Alikuwa mwanamke mzuri.
押沙龙生了三个儿子,一个女儿。女儿名叫她玛,是个容貌俊美的女子。
28 Absalomu akaishi Yerusalem miaka miwili pasipo kuona uso wa mfalme.
押沙龙住在耶路撒冷足有二年,没有见王的面。
29 Kisha Absalome akatuma neno kwa Yoabu ili ampeleke kwa mfalme, lakini Yoabu hakwenda kwake. Hivyo Absalomu akatuma neno mara ya pili, lakini Yoabu hakuja bado.
押沙龙打发人去叫约押来,要托他去见王,约押却不肯来。第二次打发人去叫他,他仍不肯来。
30 Hivyo Absalomu akawambia watumishi wake, “Tazameni, shamba la Yoabu lipo karibu na langu, naye ana shayiri kule. Nendeni mkalichome moto” Hivyo watumishi wa Absalome wakalichoma moto lile shamba.
所以押沙龙对仆人说:“你们看,约押有一块田,与我的田相近,其中有大麦,你们去放火烧了。”押沙龙的仆人就去放火烧了那田。
31 Kisha Yoabu akainuka na kwenda nyumbani kwa Absalomu akamwambia, “Kwa nini watumishi wako wamelichoma moto shamba langu?
于是约押起来,到了押沙龙家里,问他说:“你的仆人为何放火烧了我的田呢?”
32 Absalomu akamjibu Yoabu, “Tazama nilituma neno kwako kusema, 'Njoo ili nikutume kwa mfalme kusema, “Kwa nini nilikuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningesalia huko. Kwa hiyo sasa niache niuone uso wa mfalme na kama nina hatia basi na aniue.”
押沙龙回答约押说:“我打发人去请你来,好托你去见王,替我说:‘我为何从基述回来呢?不如仍在那里。’现在要许我见王的面;我若有罪,任凭王杀我就是了。”
33 Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi juu ya uso nchi mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.
于是约押去见王,将这话奏告王,王便叫押沙龙来。押沙龙来见王,在王面前俯伏于地,王就与押沙龙亲嘴。