< 2 Samweli 1 >

1 Baada ya kifo cha Sauli, Daud alirudi kutoka kuwashambulia Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.
サウルが死んだ後、ダビデはアマレクびとを撃って帰り、ふつかの間チクラグにとどまっていたが、
2 Siku ya tatu, mtu mmoja alikuja kutoka kambi ya Sauli nguo zake zikiwa zimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake. Alipofika kwa Daudi alinamisha uso wake chini akajifanya yeye mwenyewe kuwa si kitu.
三日目となって、ひとりの人が、その着物を裂き、頭に土をかぶって、サウルの陣営からきた。そしてダビデのもとにきて、地に伏して拝した。
3 Daudi akamuliza, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Nimeponyoka kutoka kambi ya Israeli.”
ダビデは彼に言った、「あなたはどこからきたのか」。彼はダビデに言った、「わたしはイスラエルの陣営から、のがれてきたのです」。
4 Daudi akamwambia, “Tafadhari nieleze jinsi mambo yalivyokuwa.” Akajibu, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wameanguka, na wengi wao wameuawa. Sauli na Yonathani mwanawe pia wameuawa.”
ダビデは彼に言った、「様子はどうであったか話しなさい」。彼は答えた、「民は戦いから逃げ、民の多くは倒れて死に、サウルとその子ヨナタンもまた死にました」。
5 Daudi akamwuliza kijana, “unajuaje kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wameuawa?”
ダビデは自分と話している若者に言った、「あなたはサウルとその子ヨナタンが死んだのを、どうして知ったのか」。
6 Yule kijana akajibu, “Kwa bahati nilikuwa juu ya Mlima Gilboa, na pale alikuwepo Sauli ameegemea mkuki wake, na magari ya farasi na waongozaji walikuwa karibu kumkamata.
彼に話している若者は言った、「わたしは、はからずも、ギルボア山にいましたが、サウルはそのやりによりかかっており、戦車と騎兵とが彼に攻め寄ろうとしていました。
7 Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, 'Mimi hapa.'
その時、彼はうしろを振り向いてわたしを見、わたしを呼びましたので、『ここにいます』とわたしは答えました。
8 Akaniuliza, 'Wewe ni nani?' Nikamjibu, 'Mimi ni Mwamaleki,'
彼は『おまえはだれか』と言いましたので、『アマレクびとです』と答えました。
9 Akaniambia, Tafadhari simama juu yangu uniuwe, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.'
彼はまたわたしに言いました、『そばにきて殺してください。わたしは苦しみに耐えない。まだ命があるからです』。
10 Hivyo nilisimama juu yake nikamuuwa, kwa maana nilijua kwamba asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka. Ndipo nikachukuwa taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, na nimevileta hapa kwako, bwana wangu.”
そこで、わたしはそのそばにいって彼を殺しました。彼がすでに倒れて、生きることのできないのを知ったからです。そしてわたしは彼の頭にあった冠と、腕につけていた腕輪とを取って、それをわが主のもとに携えてきたのです」。
11 Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.
そのときダビデは自分の着物をつかんでそれを裂き、彼と共にいた人々も皆同じようにした。
12 Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.
彼らはサウルのため、またその子ヨナタンのため、また主の民のため、またイスラエルの家のために悲しみ泣いて、夕暮まで食を断った。それは彼らがつるぎに倒れたからである。
13 Daudi akamwambia yule kijana, “Unatokea wapi?” Akajibu, mimi ni kijana wa mgeni Mwamaleki.”
ダビデは自分と話していた若者に言った、「あなたはどこの人ですか」。彼は言った、「アマレクびとで、寄留の他国人の子です」。
14 Daudi akamwambia, “Kwa nini haukuogopa kumwua mfalme, mtiwa mafuta wa Yahwe kwa mkono wako?”
ダビデはまた彼に言った、「どうしてあなたは手を伸べて主の油を注がれた者を殺すことを恐れなかったのですか」。
15 Daudi akamwita mmojawapo wa vijana na akamwambia, “Nenda ukamuue.” Hivyo kijana huyo akaenda na kumpiga hata ata chini, Mwamaleki akafa.
ダビデはひとりの若者を呼び、「近寄って彼を撃て」と言った。そこで彼を撃ったので死んだ。
16 Ndipo Daudi akamwambia Mwamaleke aliyekufa, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako kwa kuwa kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako kusema, Nimemuua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe.
ダビデは彼に言った、「あなたの流した血の責めはあなたに帰する。あなたが自分の口から、『わたしは主の油を注がれた者を殺した』と言って、自身にむかって証拠を立てたからである」。
17 Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe.
ダビデはこの悲しみの歌をもって、サウルとその子ヨナタンのために哀悼した。
18 Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Bow kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari.
これは、ユダの人々に教えるための弓の歌で、ヤシャルの書にしるされている。彼は言った、
19 “Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
「イスラエルよ、あなたの栄光は、あなたの高き所で殺された。ああ、勇士たちは、ついに倒れた。
20 Msiiseme katika Gathi, msiitangaze katika mitaa ya Ashikeloni, ili binti za wafilisti wasifurahi, ili binti za wasiotailiwa wasisherehekee.
ガテにこの事を告げてはいけない。アシケロンのちまたに伝えてはならない。おそらくはペリシテびとの娘たちが喜び、割礼なき者の娘たちが勝ちほこるであろう。
21 Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu. wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haiwezi tena kutiwa mafuta.
ギルボアの山よ、露はおまえの上におりるな。死の野よ、雨もおまえの上に降るな。その所に勇士たちの盾は捨てられ、サウルの盾は油を塗らずに捨てられた。
22 Kutoka katika damu ya waliouawa, kutoka katika miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu.
殺した者の血を飲まずには、ヨナタンの弓は退かず、勇士の脂肪を食べないでは、サウルのつるぎは、むなしくは帰らなかった。
23 Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
サウルとヨナタンとは、愛され、かつ喜ばれた。彼らは生きるにも、死ぬにも離れず、わしよりも早く、ししよりも強かった。
24 Enyi binti wa Israeli lieni juu ya Sauli, aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
イスラエルの娘たちよ、サウルのために泣け。彼は緋色の着物をもって、はなやかにあなたがたを装い、あなたがたの着物に金の飾りをつけた。
25 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka vitani! Yonathani ameuawa juu ya mahali pako pa juu.
ああ、勇士たちは戦いのさなかに倒れた。ヨナタンは、あなたの高き所で殺された。
26 Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
わが兄弟ヨナタンよ、あなたのためわたしは悲しむ。あなたはわたしにとって、いとも楽しい者であった。あなたがわたしを愛するのは世の常のようでなく、女の愛にもまさっていた。
27 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka na silaha za vita zimeteketea!”
ああ、勇士たちは倒れた。戦いの器はうせた」。

< 2 Samweli 1 >