< 2 Petro 3 >

1 Ssa, ninakuandikia wewe, mpendwa hii barua ya pili ili kukuamsha katika akili, 2 ili kwamba uweze kukumbuka maneno yaliyosemwa kabla na manabii watakatifu na kuhusu amri ya Bwana wetu na mwokozi kwa kutumia mitume. 3 Ujue ili kwanza, kwamba wasaliti watakuja katika siku za mwisho kuwasaliti ninyi, wakienenda sawasawa na matakwa yao. 4 Na wakisema “Iko wapi ahadi ya kurudi? Baba zetu walikufa, Lakini vitu vyote vilikuwa hivyo tangu mwanzo wa uumbaji. 5 Wakajifanya kusahau kwamba nchi na mbingu vilianza kutokana na maji na kupitia maji zamani za kale, kwa neno la Mungu, 6 na kwamba kupitia neno lake na maji yakawa ulimwengu kwa kipindi hicho, ikiwa imejaa maji, iliharibiwa. 7 Lakini sasa mbingu na dunia zimetunzwa kwa neno hilo hilo kwa ajili ya moto. Vimehifadhiwa kwa ajili ya siku ya hukumu na maangamizi ya watu wasio wa Mungu 8 Hii haiwezi kuchenga ujumbe wako, wapendwa, kwamba siku moja kwa bwana ni kama miaka elfu moja. Na miaka elfu moja ni kama siku moja. 9 Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi, kama inavyofikiriwa kuwa, Lakini yeye ni mvumilivu kwa ajili yenu, yeye hatamani hata mmoja aangamie, Lakini hutamani kutoa muda ili wote wapate kutubu. 10 Ingawa, siku ya Bwana itakuja kama mwizi, mbingu itapita kwa kupaza kelele. Vitu vitateketezwa kwa moto. Nchi na vitu vyote vilivyomo vitafunuliwa wazi. 11 Kwa kuwa vitu vyote vutateketezwa kwa njia hii. Je utakuwa mtu wa aina gani? Uishi kitakatifu na maisha ya kimungu. 12 Inakupasa kujua na kutambua haraka ujio wa siku ya Mungu. Siku hiyo mbingu itateketezwa kwa moto. Na vitu vitayeyushwa katika joto kali. 13 Lakini kutokana na ahadi yake, tunasubiri mbingu mpya na nchi mpya, ambapo wenye haki wataishi 14 Hivyo wapendwa kwa kuwa tunatarajia vitu hivi, jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye. 15 Na zingatia uvumilivu wa Bwana wetu katika wokovu, kama mpendwa kaka yetu Paulo, alivyowaandikia ninyi, kutokana na hekima ambayo alipewa. 16 Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake, kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa. Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo, Na kama wanavyofanya kwa maandiko. Kuelekea maangamizi yao. 17 Hivyo, wapendwa kwa kuwa mnayafahamu hayo. Jilindeni wenyewe ili kwamba msipotoshwe na udanganyifu wa walaghai na kupoteza uaminifu. 18 Lakini mkue katika neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo. Na sasa utukufu una yeye sasa na milele. Amina. (aiōn g165)

< 2 Petro 3 >

The World is Destroyed by Water
The World is Destroyed by Water