< 2 Wafalme 6 >

1 Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.
眾先知的弟子對厄里叟說:「看,我們同你住的地方太窄小了,
2 Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi.” Elisha akajibu, “unaweza kwenda mbele.”
請你讓我們到約旦河去,每人取一根樑木,在那裏建造我們的住所。」他答說:「你們去罷! 」
3 Mmoja wao akasema, “Nenda na watumishi wako tafadhali.” Elisha akajibu, “Nitaenda.”
其中一個人說:「請你也同你的僕人一起去! 」厄里叟答說:「我去。」
4 Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.
先知便同他們一起去了。他們到了約旦河,就砍伐樹木。
5 Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, “la hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!”
其中一個,砍木樑時,斧頭掉在水裏了,就大聲叫喊說:哎唷! 我主,這把斧子是借來的啊! 」
6 Basi mtu wa Mungu akasema, “kiliangukia wapi?” Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. akakata fimbo, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
天主的人問他說:「斧頭掉在那裏﹖」那人將那地方指給先知看。先知即砍下一塊木頭,丟在那裏,使斧頭浮了上來。
7 Elisha akasema, “Kichukue.” Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.
先知對他說:「你拿上來罷! 」他就伸手拿了上來。
8 Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, “kambi yangu itakuwa sehemu flani na flani.”
阿蘭王同以色列交戰時,與自己的臣商議說:要在某某地方埋伏。
9 Basi huyo mtu wa Mungu akamtuma kwa mfalme wa Israeli, akisema, “Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo.”
但天主的人打發人去見以色列王說:「你要小心提防,不要經過某某地方,因為阿蘭人已在那裏設下埋伏。」
10 Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.
以色列王就派人去偵察天主的人警告他的地方;他就小心防備,不只一兩次。
11 Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, “Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?”
阿蘭王為此事心中頗為煩惱,遂將臣僕召來,對他說:「難道你們不能告訴我:我們中誰支持以色列王嗎﹖」
12 Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, “Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala!”
一個臣僕答說:「我主,大王! 沒有誰支持,只有以色列的先知厄里叟,將君王在密室裏所談的事,都告訴了以色列王。」
13 Yule mfalme akajibu, “Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata.” Akaambiwa, “Tazama yuko Dothani.”
阿蘭王說:「你們去看看他在那裏,我好派人去捉拿。」有人告訴君王說:「他在多堂。」
14 Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.
阿蘭王就打發馬隊戰車和強大的部隊前去,夜間到了那裏,將城圍住。
15 Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, “Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?”
天主的人的僕人清早起來出門時,看見軍隊車馬將城包圍了,就對先知說:「哎! 我主,我們怎麼辦﹖」
16 Elisha akajibu, “usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao.”
先知答說:「不必害怕,因為偕同我們的,比他們的還多。」
17 Elisha akajibu na kusema, “Yahwe, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona.” Ndipo Yahwe alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto yamemzunguka Elisha!
厄里叟就祈禱說:「上主,求你開啟他的眼,叫他看見。」上主就開了僕人的眼,他看見遍山都是火馬車,圍繞著厄里叟。
18 Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa Yahwe na kusema, “Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba.” Hivyo Yahwe akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.
敵人下到先知那裏的時候,厄里叟懇求上主說:「求你打擊這個民族,使他們眼目失明。」上主果然照厄里叟的話打擊了他們,使他們眼目失明。
19 Kisha Elisha akawaambia Washami, “Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta.” Ndipo akawaongoza kweda Samaria.
厄里叟對他們說:「不是這條路,也不是這座城;你們跟我來,我要領你們到你們尋找的人那裏去。」於是先知領他們到了撒瑪黎雅。
20 Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, “Yahwe, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona.” Yahwe akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.
他們一進了撒瑪黎雅,厄里叟就祈禱說:「上主,開啟這些人的眼睛,叫他們看見。」上主果然開了他們的眼睛;他們一看,自己竟在撒瑪黎雅城內。
21 Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, “Baba yangu, niwaue? Niwaue?”
以色列王看見他們,就對厄里叟說:「我父,要殺死他們嗎﹖」
22 Elisha akajibu, “Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.”
厄里叟答說:「不要殺他們;你自己用弓劍擄來的人,你豈可殺死﹖你要為這些人預備飯和水,叫他們吃喝,然後讓他們回到自己的主上那裏去。」
23 Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Wasahami halikurudi kwa mda mrefu katika nchi ya Israeli.
君王就給他們預備了盛宴,叫他們吃了喝了,打發他們回到自己的主上那裏去。從此,阿蘭隊伍再沒有侵犯以色列地方。
24 Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.
這事以後,阿蘭王本哈達得集合了他所有的軍隊,上來圍困撒瑪黎雅。
25 Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
撒瑪黎雅被圍困後,陷於嚴重的飢荒,甚至一個驢頭,值八十「協刻耳」銀子,四分之一「卡步」豆莢,值五「協刻耳」銀子。
26 Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoka akamlilia akisema, “Nisaidie, bwana wangu, mfalme.”
當以色列王從城牆上經過時,有一個婦人呼求他說:「我主大王,救救我罷! 」
27 Akasema, “Kama Yahwe hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?”
君王答說:「如果上主不救你,我怎能救你﹖靠禾場﹖靠酒池﹖」
28 Mfalme akaendelea, “Nini kinakusumbua?” Akajibu, “Huyu mwanamke ameniambia, 'Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wakwangu kesho.”
君王問那婦人說:「你有什麼事﹖」婦人答說:「這個女人曾對我說:把你的兒子交出來,我們今天吃;留下我的兒子,我們明天吃。
29 Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, “Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake.”
於是我們就把我的兒子煮著吃了。第二天我對那女人說:把你的兒子交出來給我們吃,她卻把自己的兒子藏了起來。」
30 Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia chini, dhidi ya ngozi yake.
君王聽了這婦人的話,就撕裂了自己的衣服,─當他正在城牆上經過,民眾都看見了他貼身穿著苦衣,─
31 Kisha akasema, “Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo.”
說「如果沙法特的兒子厄里叟的頭,今天還留在他身上,願天主嚴厲,且加倍嚴厲地懲罰我! 」
32 Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, “Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivytumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?”
那時厄里叟正坐在屋裏,長老們同他坐在一起,君王派一個人在他以前去,但是這人還未來到,厄里叟就對長老們說:「你們看,這個兇手之子,竟派人來要斬我的頭。你們注意,使者來到時,你們要把門關上,把他關在門外;在他後面不就是他主上的腳步聲嗎﹖」
33 Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, “Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa Yahwe. Kwa nini nimsubiri Yahwe tena?”
先知還同他們說話的時候,君王就下到他那裏說:「這災難是由上主來的,我對上主還有什麼指望﹖」

< 2 Wafalme 6 >