< 2 Wafalme 3 >
1 Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ta Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili.
ユダの王ヨシャパテの第十八年にアハブの子ヨラムはサマリヤでイスラエルの王となり、十二年世を治めた。
2 Alifanya yaliyo maovo usoni kwa Yahwe, lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza.
彼は主の目の前に悪をおこなったが、その父母のようではなかった。彼がその父の造ったバアルの石柱を除いたからである。
3 Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao.
しかし彼はイスラエルに罪を犯させたネバテの子ヤラベアムの罪につき従って、それを離れなかった。
4 Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100, 000 na manyoya ya kondoo dume 100, 000.
モアブの王メシャは羊の飼育者で、十万の小羊と、十万の雄羊の毛とを年々イスラエルの王に納めていたが、
5 Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.
アハブが死んだ後、モアブの王はイスラエルの王にそむいた。
6 Hivyo Mfalme Joramu alikaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita.
そこでヨラム王はその時サマリヤを出て、イスラエルびとをことごとく集め、
7 Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Yehoshafati akajibu, “Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”
また、人をユダの王ヨシャパテにつかわし、「モアブの王はわたしにそむきました。あなたはモアブと戦うために、わたしと一緒に行かれませんか」と言わせた。彼は言った、「行きましょう。わたしはあなたと一つです。わたしの民はあなたの民と一つです。わたしの馬はあなたの馬と一つです」。
8 Ndipo akasema, “Tutawashambulia kwa njia gani?” Yehoshafati akajibu, “Kwa njia ya jangwa la Edemu.
彼はまた言った、「われわれはどの道を上るのですか」。ヨラムは答えた、「エドムの荒野の道を上りましょう」。
9 Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa mda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama.
こうしてイスラエルの王はユダの王およびエドムの王と共に出て行った。しかし彼らは回り道をして、七日の間進んだが、軍勢とそれに従う家畜の飲む水がなかったので、
10 Basi mfalme wa Israeli akasema, “Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?”
イスラエルの王は言った、「ああ、主は、この三人の王をモアブの手に渡そうとして召し集められたのだ」。
11 Lakini Yehoshafati akasema, “je hakuna nabii wa Yahwe, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu Yahwe kupitia yeye?” Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya.”
ヨシャパテは言った、「われわれが主に問うことのできる主の預言者はここにいませんか」。イスラエルの王のひとりの家来が答えた、「エリヤの手に水を注いだシャパテの子エリシャがここにいます」。
12 Yehoshafati akasema, “Neno la Yahwe liko pamoja nami.” Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshaphati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake.
ヨシャパテは言った、「主の言葉が彼にあります」。そこでイスラエルの王とヨシャパテとエドムの王とは彼のもとへ下っていった。
13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako.” Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, “Hapana, kwa sababu Yahwe amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke.”
エリシャはイスラエルの王に言った、「わたしはあなたとなんのかかわりがありますか。あなたの父上の預言者たちと母上の預言者たちの所へ行きなさい」。イスラエルの王は彼に言った、「いいえ、主がこの三人の王をモアブの手に渡そうとして召し集められたのです」。
14 Elisha akajibu, “Kama Yawhe wa majeshi aishivo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yeda, Nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama.
エリシャは言った、「わたしの仕える万軍の主は生きておられます。わたしはユダの王ヨシャパテのためにするのでなければ、あなたを顧み、あなたに会うことはしないのだが、
15 Lakini sasa niletee mwanamuziki.” Ndipo alipokuja mpiga muziki alipocheza, mkono wa Yahwe ukaja juu ya Elisha.
いま楽人をわたしの所に連れてきなさい」。そこで楽人が楽を奏すると、主の手が彼に臨んで、
16 Akasema, “'Yahwe asema hivi, 'Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.'
彼は言った、「主はこう仰せられる、『わたしはこの谷を水たまりで満たそう』。
17 Kwa kuwa Yahwe asema hivi, 'Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.'
これは主がこう仰せられるからである、『あなたがたは風も雨も見ないのに、この谷に水が満ちて、あなたがたと、その家畜および獣が飲むであろう』。
18 Hiki ni kitu rahisi usoni mwa Yahwe. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu.
これは主の目には小さい事である。主はモアブびとをも、あなたがたの手に渡される。
19 Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba.”
そしてあなたがたはすべての堅固な町と、すべての良い町を撃ち、すべての良い木を切り倒し、すべての水の井戸をふさぎ、石をもって地のすべての良い所を荒すであろう」。
20 Hivyo asubuhi karibia na mda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji.
あくる朝になって、供え物をささげる時に、水がエドムの方から流れてきて、水は国に満ちた。
21 Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani.
さてモアブびとは皆、王たちが自分たちを攻めるために上ってきたのを聞いたので、よろいを着ることのできる者を、老いも若きもことごとく召集して、国境に配置したが、
22 Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu.
朝はやく起きて、太陽がのぼって水を照したとき、モアブびとは目の前に血のように赤い水を見たので、
23 Wakatamka kwa hasira, “Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuna wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!”
彼らは言った、「これは血だ、きっと王たちが互に戦って殺し合ったのだ。だから、モアブよ、ぶんどりに行きなさい」。
24 Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua.
しかしモアブびとがイスラエルの陣営に行くと、イスラエルびとは立ちあがってモアブびとを撃ったので、彼らはイスラエルの前から逃げ去った。イスラエルびとは進んで、モアブびとを撃ち、その国にはいって、
25 Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia.
町々を滅ぼし、おのおの石を一つずつ、地のすべての良い所に投げて、これに満たし、水の井戸をことごとくふさぎ、良い木をことごとく切り倒して、ただキル・ハラセテはその名を残すのみとなったが、石を投げる者がこれを囲んで撃ち滅ぼした。
26 Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga mia saba pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa.
モアブの王は戦いがあまりに激しく、当りがたいのを見て、つるぎを抜く者七百人を率い、エドムの王の所に突き入ろうとしたが、果さなかったので、
27 Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.
自分の位を継ぐべきその長子をとって城壁の上で燔祭としてささげた。その時イスラエルに大いなる憤りが臨んだので、彼らは彼をすてて自分の国に帰った。