< 2 Wafalme 25 >
1 Ilitokea kwamba katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya huo mwezi, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote kwa ajili ya kupigana dhidi ya Yerusalemu. Akaweka kambi kuelekeana nayo, na wakajenga ukuta kuizunguka.
Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli, akiwa na jeshi lake lote, alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzunguka mji pande zote.
2 Hivyo mji huo ulizungukwa mpaka miaka kumi na moja ya utawala wa Sedekia.
Mji ulizungukwa na jeshi mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Mfalme Sedekia.
3 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
Ilipowadia siku ya tisa ya mwezi wa nne, njaa ikazidi kuwa kali sana ndani ya mji, hadi hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu.
4 Wakati huo ule mji ulikuwa umebomoka ndani, na wapiganaji wote wakakimbia usiku kwa njia ya lango kati ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wote wameuzunguka mji. Mfalme akaenda kuelekea upande wa Araba.
Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba.
5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuata mfalme Sedekia na kumchukua katika tambarare ya bonde la Mto Yoradani karibu na Yeriko. Jeshi lake lote lilitawanyika wakamwacha.
Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata katika sehemu tambarare za Yeriko. Askari wake wote wakatengwa naye na kutawanyika,
6 Wakamkamata mfalme na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo walipitisha hukumu juu yake.
naye akakamatwa. Akapelekwa kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, mahali ambapo hukumu yake ilitangazwa.
7 Kama kwa watoto wa Sedekia, wakawachinja mbele ya macho yake. Kisha akamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.
Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake. Kisha wakayangʼoa macho yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
8 Basi katika mwezi wa tano, katika siku ya saba ya mwezi, ambapo ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, mtumishi wa mfalme wa Babeli na amrijeshi wa walinzi wake, wakaja hadi Yerusalemu.
Mnamo siku ya saba ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme, afisa wa mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu.
9 Akaichoma moto nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme, na nyumba zote za Yeruselemu; pia kila jengo la muhimu katika mji akayachoma.
Alichoma moto Hekalu la Bwana, jumba la kifalme, na nyumba zote za Yerusalemu. Aliteketeza kila jengo muhimu.
10 Kama kwa kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli ambao walikuwa chini ya amrishi wa walinzi wakaziharibu.
Jeshi lote la Wakaldayo, chini ya jemadari wa askari walinzi wa mfalme, walivunja kuta zilizoizunguka Yerusalemu.
11 Basi watu waliokuwa wamebaki ambao walikuwa wameondoka katika mji, wale waliokuwa wameasi kwa mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu-Nebuzadani, amiri jeshi wa mlinzi, wakachukuliwa kwenda utumwani.
Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli.
12 Lakini amiri jeshi wa mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi ili wafanye kazi kwenye shamba la mizabibu na kulima.
Lakini yule jemadari wa askari walinzi akawaacha baadhi ya wale watu maskini kabisa ili watunze mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.
13 Na zile nguzo za shaba ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, na misimamio na bahari ya chuma ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakazivunja vipande vipande na kubeba shaba kuirudisha Babeli.
Wakaldayo walivunja vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Bwana. Hivyo wakaichukua hiyo shaba na kuipeleka Babeli.
14 Masufuria, mabeleshi, makasi, vijiko, na vyombo vyote vya shaba ambavyo kuhani alivyokuwa amevitunza kwenye hekalu-Wakaldayo wakavichukua vyote.
Wakachukua pia vyungu, masepetu, mikasi ya kusawazishia tambi, sahani na vyombo vyote vya shaba vilivyotumika katika huduma ya Hekalu.
15 Masufuria ya kuhamisha majivu na mabakuli ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu, na yale yaliyotengenezwa kwa fedha-yule nahodha wa mlinzi wa mfalme akavichukua pia.
Jemadari wa askari walinzi wa mfalme akachukua vile vyetezo na yale mabakuli ya kunyunyizia, vitu vyote vile vilivyokuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi au fedha.
16 Zile nguzo mbili, ile bahari, na vile vitako ambavyo Suleimani alivitengeneza kwa ajili ya nyumba ya Yahwe shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika.
17 Urefu wa ile nguzo ya kwanza ulikuwa ridhaa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Na urefu wa kichwa ulikuwa ridhaa tatu, pamoja na mapambo ya wavu na makomamanga yote yakizunguka kwenye hicho kichwa, vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Na ile nguzo nyingine ilikuwa vivyo hivyo kama ile ya kwanza pamoja na wavu wake.
Kila nguzo ilikuwa na urefu wa dhiraa kumi na nane. Sehemu ya shaba juu ya nguzo moja ilikuwa na urefu wa dhiraa tatu na ilikuwa imepambwa kwa wavu na makomamanga ya shaba kuizunguka kote. Ile nguzo nyingine pamoja na wavu wake ilifanana na hiyo ya kwanza.
18 Yule amiri jeshi wa mlinzi akamchukua Seraya kuhani mkuu, pamoja za Sefania, yule kuhani wa pili, na walinzi watatu wa kwenye lango.
Yule jemadari wa askari walinzi akawachukua kama wafungwa Seraya kuhani mkuu, kuhani Sefania aliyefuata kwa cheo, na mabawabu watatu.
19 Kutoka mjini akamchukua mlinzi, afisa mmoja ambaye aliyekuwa msimamizi wa maaskari, na watu watano ambao walikuwa wakimshauri mfalme, ambao walikuwa bado katika mji. Pia alimchukua mfungwa wa afisa jeshi la mfalme, kwa ajili ya kuandika watu kwenye jeshi, pamoja na watu sitini muhimu kutoka hiyo nchi ambao walikuwa katika mji.
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri watano wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
20 Kisha Nebuzaradani, amiri wa mlinzi, akawachukua na kuwapeleka kwa mfalme Babeli huko Ribla.
Nebuzaradani jemadari akawachukua hao wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.
21 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaiacha nchi yake kwenda utumwani.
Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao.
22 Na wale watu waliokuwa wamebakia katika nchi ya Yuda, wale ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwaacha, akamuweka Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, msimamizi wao.
Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda.
23 Kisha wakati maamiri wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemfanya Gedalia kuwa liwali, wakaenda kwa Gedalia huko Mispa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kuwa mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.
24 Gedalia akafanya kiapo kwa watu wake na kuwaambia, “Msiwaogope Wakaldayo. Muishi katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vema kwenu.”
Gedalia akaapa ili kuwatia moyo wao na watu wao. Akasema, “Msiwaogope maafisa wa Kikaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu.”
25 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.
Hata hivyo, katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi, nao wakamuua Gedalia, na pia watu wa Yuda, pamoja na Wakaldayo waliokuwa naye huko Mispa.
26 Kisha wale watu wote, kutoka chini kwenda juu, na maamiri wa jeshi, wakainuka na kwenda Misri, kwasababu walikuwa wanawaogopa Wababeli.
Baada ya haya, watu wote kuanzia aliye mdogo sana hadi aliye mkubwa kabisa, pamoja na maafisa wa jeshi, wakakimbilia Misri kwa kuwaogopa Wakaldayo.
27 Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.
Katika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili.
28 Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.
Alizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima zaidi kuliko wale wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli.
29 Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
Hivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya mfungwa, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme.
30 na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.
Siku kwa siku mfalme alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake.