< 2 Wafalme 24 >

1 Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
Wakati wa utawala wa Yehoyakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoyakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza.
2 Yahwe akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la Yahwe ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
Bwana akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la Bwana lililosemwa na watumishi wake manabii.
3 Ilikuwa baada ya mda mfupi kwenye kinywa cha Yahwe kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sabau ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
Hakika mambo haya yalitokea Yuda kulingana na agizo la Bwana, ili kuwaondoa kutoka machoni pake kwa sababu ya dhambi za Manase na yote aliyoyafanya,
4 na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. Yahwe hakuwa tayari kusamehe hilo.
ikiwa ni pamoja na kumwaga damu isiyo na hatia. Kwa kuwa aliijaza Yerusalemu kwa damu isiyo na hatia, naye Bwana hakuwa radhi kusamehe.
5 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
6 Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
Yehoyakimu akalala pamoja na baba zake. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake.
7 Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kitabu cha Misri mpaka Mto wa Frati.
Mfalme wa Misri hakutoka tena katika nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa ameitwaa himaya yake yote, kuanzia Kijito cha Misri hadi Mto Frati.
8 Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani kutoka Yerusalemu.
9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
Akafanya maovu machoni pa Bwana, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.
10 Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
Wakati huo, maafisa wa Nebukadneza mfalme wa Babeli walikuja ili kuishambulia Yerusalemu, nao wakaizunguka kwa jeshi.
11 Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
Nebukadneza mwenyewe akaupandia mji wakati maafisa wake walipokuwa wameuzunguka kwa jeshi.
12 na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.
13 Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya Yahwe, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Suleimani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la Yahwe, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
Kama vile Bwana alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la Bwana na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la Bwana.
14 Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu maskini katika nchi.
Akawachukua watu wa Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi.
15 Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi.
16 Wapiganaji wote, elfu saba kwa hesabu, na mafundi elfu moja na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga- mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
Mfalme wa Babeli pia akawahamishia Babeli mashujaa elfu saba, wenye nguvu na wanaofaa kupigana vita, na watu wenye ustadi na mafundi elfu moja.
17 Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
Akamfanya Matania, ndugu wa baba yake Yehoyakini, kuwa mfalme mahali pake, na akalibadilisha jina lake kuwa Sedekia.
18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna.
19 Alifanya yaliyo maovu machoni mwa Yahwe; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
Alifanya maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Yehoyakimu.
20 Kupitia hasira ya Yahwe, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya Bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

< 2 Wafalme 24 >