< 2 Wafalme 22 >
1 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
約史雅登基時才八歲,在耶路撒冷作王凡三十一年,他的母親名叫耶狄達,是波茲卡特人阿達雅的女兒。
2 Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa Yahwe. Alitembea kwenye njia zote za Daudi babu yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
他行了上主視為正義的事,在一切事上,走了他祖先達味的路。不偏左也不偏右。
3 Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya Yahwe, akisema,
約史雅為王十八年時,派默叔藍的孫子,沙番書記到上主的殿裏去,吩咐他說:「
4 “Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
你去見大司祭希耳克雅,請他將獻於上主聖殿,和守門人由人民收來的銀錢結算清濋,
5 Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya Yahwe, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya Yahwe, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
交給那些在上主殿內監工的人,叫他們發給那些在上主殿內工作和修理聖殿破壞地方的工人,
6 Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya Yahwe.”
即木匠、工人和泥水匠,或購買修理聖殿的木料和鑿好的石頭。
7 Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
銀子交給他們之後,不必再同他們算帳,因為他們都是辦事很忠信的人。」
8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.” Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
大司祭希耳克雅對沙番書記說:「我在上主殿內發現了法律書。」希耳克雅將這卷書交給了沙番,沙番讀了。
9 Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, “Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya Yahwe.”
沙番書記遂來見君王,向君王報告說:「你的僕人已將聖殿內所有的銀錢倒出來,交給了那些在上主殿內監工的人。」
10 Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, “Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu.” Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
沙番書記繼而又向君王報告說:「大司祭希耳克雅交給我一卷書。」沙番就在君王面前朗讀了那書。
11 Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
君王一聽了法律書上的話,就撕裂了自己的衣服,
12 Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
即刻吩咐大司祭希耳克雅,沙番的兒子阿希甘,米加的兒子阿革波爾,沙番書記和君王的臣僕阿撒雅說:「
13 Nenda na ukaongee pamoja na Yahwe kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya Yahwe ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu babu zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
你們為我,為人民,為全猶大,去求問上主關於所發現的書上的話;因為我們的祖先沒有聽從這卷書上的話,也沒有按造這卷書上所記載的去實行,所以上主對我們大發忿怒。」
14 Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
大司祭希耳克雅、阿希甘、阿革波爾、沙番和阿撒雅,於是去見住在耶路撒冷新市區,哈爾哈斯的孫子,提刻瓦的兒子,管理祭衣的沙隆的妻子,女先知胡耳達,向她說明了來意以後,
15 Akawaambia, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, asemavyo: 'Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
她就回答他們說:「上主以色列的天主這樣說:你們去回報那派你們來見我的人說說:
16 “Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: 'Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
上主這樣說:看,我必要依照猶大王所讀的那卷書上的一切話:使災禍降在這地方和這地方的居民身上,
17 Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya-kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika.”'
因為他們捨棄了我,向別的神焚香。凡他們所做的,無不惹我動怒;所以我的怒火要向這地方發作,總不熄滅。
18 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya Yahwe, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: “Yahwe, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,
至於那派你們來求問上主的猶大王,你們要這樣對他說:上主以色列的天主這樣說:你既然聽了這些話,
19 kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za Yahwe, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwasaabu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
既然一聽見我指著這地和這地上的居民,說他們必要成為令人驚駭和詛咒的對象,你就動了心,在我面前自卑自賤,撕裂了自己的衣服,在我面前痛哭,因此我也應允了你:上主的斷語。
20 Tazama, nitakukusanya na babu zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu. “"” Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.
我要使你與你的祖先團聚,你要平安歸到你的墳墓裏,你的眼睛也不會見到我要在這地方所降的一切災禍。」他們回去向君王報告了這話。