< 2 Wafalme 15 >

1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
בשנת עשרים ושבע שנה לירבעם מלך ישראל מלך עזריה בן אמציה מלך יהודה
2 Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.
בן שש עשרה שנה היה במלכו וחמשים ושתים שנה מלך בירושלם ושם אמו יכליהו מירושלם
3 Alifanya yaliyo mema machoni pa Yahwe, kama baba yake Amazia alivyofanya.
ויעש הישר בעיני יהוה ככל אשר עשה אמציהו אביו
4 Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.
רק הבמות לא סרו עוד העם מזבחים ומקטרים בבמות
5 Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
וינגע יהוה את המלך ויהי מצרע עד יום מתו וישב בבית החפשית ויותם בן המלך על הבית שפט את עם הארץ
6 Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
ויתר דברי עזריהו וכל אשר עשה הלא הם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי יהודה
7 Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.
וישכב עזריה עם אבתיו ויקברו אתו עם אבתיו בעיר דוד וימלך יותם בנו תחתיו
8 Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.
בשנת שלשים ושמנה שנה לעזריהו מלך יהודה מלך זכריהו בן ירבעם על ישראל בשמרון--ששה חדשים
9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alisababisha Israeli kuasi
ויעש הרע בעיני יהוה כאשר עשו אבתיו לא סר מחטאות ירבעם בן נבט אשר החטיא את ישראל
10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
ויקשר עליו שלם בן יבש ויכהו קבל עם וימיתהו וימלך תחתיו
11 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
ויתר דברי זכריה הנם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי ישראל
12 Hili ndilo lililokuwa neno la Yahwe ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea.
הוא דבר יהוה אשר דבר אל יהוא לאמר בני רביעים ישבו לך על כסא ישראל ויהי כן
13 Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.
שלום בן יביש מלך בשנת שלשים ותשע שנה לעזיה מלך יהודה וימלך ירח ימים בשמרון
14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
ויעל מנחם בן גדי מתרצה ויבא שמרון ויך את שלום בן יביש בשמרון וימיתהו וימלך תחתיו
15 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafle wa Israeli.
ויתר דברי שלום וקשרו אשר קשר הנם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי ישראל
16 Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwasababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.
אז יכה מנחם את תפסח ואת כל אשר בה ואת גבוליה מתרצה--כי לא פתח ויך את כל ההרותיה בקע
17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.
בשנת שלשים ותשע שנה לעזריה מלך יהודה מלך מנחם בן גדי על ישראל עשר שנים--בשמרון
18 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.
ויעש הרע בעיני יהוה לא סר מעל חטאות ירבעם בן נבט אשר החטיא את ישראל--כל ימיו
19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.
בא פול מלך אשור על הארץ ויתן מנחם לפול אלף ככר כסף--להיות ידיו אתו להחזיק הממלכה בידו
20 Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
ויצא מנחם את הכסף על ישראל על כל גבורי החיל לתת למלך אשור חמשים שקלים כסף לאיש אחד וישב מלך אשור ולא עמד שם בארץ
21 Kama kwa mabo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli?
ויתר דברי מנחם וכל אשר עשה הלוא הם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי ישראל
22 Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
וישכב מנחם עם אבתיו וימלך פקחיה בנו תחתיו
23 Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.
בשנת חמשים שנה לעזריה מלך יהודה מלך פקחיה בן מנחם על ישראל בשמרון--שנתים
24 Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.
ויעש הרע בעיני יהוה לא סר מחטאות ירבעם בן נבט אשר החטיא את ישראל
25 Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
ויקשר עליו פקח בן רמליהו שלישו ויכהו בשמרון בארמון בית מלך (המלך) את ארגב ואת האריה ועמו חמשים איש מבני גלעדים וימתהו וימלך תחתיו
26 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
ויתר דברי פקחיה וכל אשר עשה הנם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי ישראל
27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.
בשנת חמשים ושתים שנה לעזריה מלך יהודה מלך פקח בן רמליהו על ישראל בשמרון--עשרים שנה
28 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.
ויעש הרע בעיני יהוה לא סר מן חטאות ירבעם בן נבט אשר החטיא את ישראל
29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.
בימי פקח מלך ישראל בא תגלת פלאסר מלך אשור ויקח את עיון ואת אבל בית מעכה ואת ינוח ואת קדש ואת חצור ואת הגלעד ואת הגלילה כל ארץ נפתלי ויגלם אשורה
30 Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
ויקשר קשר הושע בן אלה על פקח בן רמליהו ויכהו וימיתהו וימלך תחתיו--בשנת עשרים ליותם בן עזיה
31 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
ויתר דברי פקח וכל אשר עשה הנם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי ישראל
32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
בשנת שתים לפקח בן רמליהו מלך ישראל מלך יותם בן עזיהו מלך יהודה
33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.
בן עשרים וחמש שנה היה במלכו ושש עשרה שנה מלך בירושלם ושם אמו ירושא בת צדוק
34 Yotahmu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.
ויעש הישר בעיני יהוה ככל אשר עשה עזיהו אביו עשה
35 Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitio sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.
רק הבמות לא סרו--עוד העם מזבחים ומקטרים בבמות הוא בנה את שער בית יהוה--העליון
36 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
ויתר דברי יותם אשר עשה הלא הם כתובים על ספר דברי הימים--למלכי יהודה
37 Katika zamani hizo Yahwe akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.
בימים ההם--החל יהוה להשליח ביהודה רצין מלך ארם ואת פקח בן רמליהו
38 Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akwa mfalme katika mhali pake.
וישכב יותם עם אבתיו ויקבר עם אבתיו בעיר דוד אביו וימלך אחז בנו תחתיו

< 2 Wafalme 15 >