< 2 Wafalme 12 >

1 Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa mda wa miaka arobaini huko Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.
Katika mwaka wa saba wa utawala wa Yehu, Yoashi alianza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka arobaini. Jina la mama yake aliitwa Sibia, kutoka Beer-Sheba.
2 Yoashi akafanya yaliyo mema usoni mwa Yahwe siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha.
Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza.
3 Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu.
Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko.
4 Yoashi akamwambia kuhani, “Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya Yahwe, pesa ya matumizi pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya Yahwe-
Yoashi akawaambia makuhani, “Kusanyeni fedha zote ambazo zitaletwa kama sadaka takatifu kwenye Hekalu la Bwana, yaani fedha zilizokusanywa kama kodi, fedha zilizopokelewa kutokana na nadhiri za watu binafsi, na fedha zilizoletwa kwa hiari hekaluni.
5 makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu.”
Kila kuhani na apokee fedha kutoka kwa mmoja wa watunza hazina, nazo zitumike kukarabati uharibifu wowote unaoonekana katika Hekalu.”
6 Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu.
Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu.
7 Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, “Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatia wale wanaoweza kufanya matengenezo.
Kwa hiyo Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na makuhani wengine, akawauliza, “Kwa nini hamtengenezi uharibifu uliofanyika hekaluni? Msichukue fedha zaidi kutoka kwa watunza hazina wenu kwa ajili ya matumizi yenu, lakini kuanzia sasa ni lazima fedha yote itumike kwa ajili ya kukarabati Hekalu.”
8 Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe.
Makuhani wakakubali kuwa hawatakusanya tena fedha kutoka kwa watu na kwamba hawatakarabati Hekalu wenyewe.
9 Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya Yahwe. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe.
Yehoyada kuhani akachukua kisanduku na akatoboa tundu kwenye kifuniko chake. Akakiweka kando ya madhabahu upande wa kulia unapoingia hekaluni mwa Bwana. Makuhani waliolinda ingilio wakaweka ndani ya kisanduku fedha zote ambazo zililetwa katika Hekalu la Bwana.
10 Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwadishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya Yahwe.
Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la Bwana, na kuziweka katika mifuko.
11 Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya Yahwe. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya Yahwe,
Wakiisha kuthibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu la Bwana: yaani, maseremala na wajenzi,
12 na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya Yahwe, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza.
waashi na wakata mawe. Walinunua mbao na mawe ya kuchongwa kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana, na kulipia gharama nyingine zote za kulitengeneza.
13 Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo.
Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la Bwana;
14 Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya Yahwe.
zililipwa kwa wafanyakazi, ambao walizitumia kwa kukarabati Hekalu.
15 Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.
Wao hawakudai kupewa hesabu ya fedha kutoka kwa wale waliowapa ili kuwalipa wafanyakazi, kwa sababu walifanya kwa uaminifu wote.
16 Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu la Bwana; zilikuwa mali ya makuhani.
17 Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambuliwa na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.
Wakati huu Hazaeli mfalme wa Aramu akapanda kuishambulia Gathi, akaiteka. Kisha akageuka ili kuishambulia Yerusalemu.
18 Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye gala la nyumba ya Yahwe na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.
Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, wafalme wa Yuda, zawadi ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameziweka wakfu pamoja na dhahabu yote iliyokutwa katika hazina za Hekalu la Bwana na katika jumba la kifalme, akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu.
19 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
Kwa matukio mengine ya utawala wa Yoashi na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
20 Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.
Maafisa wake wakafanya shauri baya dhidi yake, nao wakamuulia Yoashi huko Beth-Milo, kwenye barabara iteremkayo kuelekea Sila.
21 Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.
Maafisa waliomuua walikuwa Yozabadi mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri. Akafa na akazikwa pamoja na baba zake katika Mji wa Daudi. Naye Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

< 2 Wafalme 12 >