< 2 Wafalme 11 >
1 Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.
亞哈謝的母親亞她利雅見她兒子死了,就起來剿滅王室。
2 Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.
但約蘭王的女兒,亞哈謝的妹子約示巴,將亞哈謝的兒子約阿施從那被殺的王子中偷出來,把他和他的乳母都藏在臥房裏,躲避亞她利雅,免得被殺。
3 Alikuwa pamoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya Yahwe, kwa mda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.
約阿施和他的乳母藏在耶和華的殿裏六年;亞她利雅篡了國位。
4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta maamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya Yahwe. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya Yahwe. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.
第七年,耶何耶大打發人叫迦利人和護衛兵的眾百夫長來,領他們進了耶和華的殿,與他們立約,使他們在耶和華殿裏起誓,又將王的兒子指給他們看,
5 Akawaamuru, akisema, “Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,
吩咐他們說:「你們當這樣行:凡安息日進班的三分之一要看守王宮,
6 na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi.”
三分之一要在蘇珥門,三分之一要在護衛兵院的後門。這樣把守王宮,攔阻閒人。
7 Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya mfalme.
你們安息日所有出班的三分之二要在耶和華的殿裏護衛王;
8 Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.
各人手拿兵器,四圍護衛王。凡擅入你們班次的必當治死,王出入的時候,你們當跟隨他。」
9 Hivyo mamia ya maamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.
眾百夫長就照着祭司耶何耶大一切所吩咐的去行,各帶所管安息日進班出班的人來見祭司耶何耶大。
10 Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa maamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe.
祭司便將耶和華殿裏所藏大衛王的槍和盾牌交給百夫長。
11 Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.
護衛兵手中各拿兵器,在壇和殿那裏,從殿右直到殿左,站在王子的四圍。
12 Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpatia mikataba ya agano. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, “Mfalme na aishi!”
祭司領王子出來,給他戴上冠冕,將律法書交給他,膏他作王;眾人就拍掌說:「願王萬歲!」
13 Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya Yahwe.
亞她利雅聽見護衛兵和民的聲音,就到民那裏,進耶和華的殿,
14 Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na manahodha na wapiga mabaragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”
看見王照例站在柱旁,百夫長和吹號的人侍立在王左右,國中的眾民歡樂吹號;亞她利雅就撕裂衣服,喊叫說:「反了!反了!」
15 Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza maamri jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, “Mtoeni kwenye safu.” Atakayemfuata, muueni kwa upanga.” Kwa kuwa kuhani alisema, “Msimwache auawe kwenye nyumba ya Yahwe.”
祭司耶何耶大吩咐管轄軍兵的百夫長說:「將她趕出班外,凡跟隨她的必用刀殺死!」因為祭司說「不可在耶和華殿裏殺她」,
16 Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.
眾兵就閃開讓她去;她從馬路上王宮去,便在那裏被殺。
17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Yahwe na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa Yahwe, na pia kati ya mfalme na watu.
耶何耶大使王和民與耶和華立約,作耶和華的民;又使王與民立約。
18 Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuingusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la Yahwe.
於是國民都到巴力廟,拆毀了廟,打碎壇和像,又在壇前將巴力的祭司瑪坦殺了。祭司耶何耶大派官看守耶和華的殿,
19 Yehoyada akawachukua maamiri jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.
又率領百夫長和迦利人與護衛兵,以及國中的眾民,請王從耶和華殿下來,由護衛兵的門進入王宮,他就坐了王位。
20 Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.
國民都歡樂,閤城都安靜。眾人已將亞她利雅在王宮那裏用刀殺了。
21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.
約阿施登基的時候年方七歲。