< 2 Wafalme 1 >
1 Moabu aliasi dhidi ya Israeli baada ya kifo cha Ahabu.
Prævaricatus est autem Moab in Israel, postquam mortuus est Achab.
2 Baada hapo Ahazi akaanguka chini ya dirisha lenye waya zinazikinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, “Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha.”
Ceciditque Ochozias per cancellos cœnaculi sui, quod habebat in Samaria, et ægrotavit: misitque nuncios, dicens ad eos: Ite, consulite Beelzebub deum Accaron, utrum vivere queam de infirmitate mea hac.
3 Lakini malaika wa Yahwe wakamwambia Eliya Mtishbi, “Inuka, nenda ukaonane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, na uwaulize, 'Je ni kwasababu hakuna Mungu katika israeli ambaye mnayekwenda kuuliza pamoja na Zebebu, mungu wa Ekroni?
Angelus autem Domini locutus est ad Eliam Thesbiten, dicens: Surge, et ascende in occursum nunciorum regis Samariæ, et dices ad eos: Numquid non est Deus in Israel, ut eatis ad consulendum Beelzebub deum Accaron?
4 Kwa hiyo Yahwe anasema, “Hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ambacho ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika."”” Baada ya hapo Eliya akaondoka.
Quam ob rem hæc dicit Dominus: De lectulo, super quem ascendisti, non descendes, sed morte morieris. Et abiit Elias.
5 wakati wale wajumbe waliporudi kwa Ahazia, akawaambia, “Kwa nini mmerudi?”
Reversique sunt nuncii ad Ochoziam. Qui dixit eis: Quare reversi estis?
6 Wakamwambia, “mtu amekuja kuonana na sisi ambaye ametuambia, 'Turudi kwa mfalme ambaye aliyewatuma, na mkamwambie, Yahwe amesema hivi: 'Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli mpaka mmewatuma watu kwenda kumuuliza kwa Baal Zabubu, mungu wa Ekron? Kwa hiyo hutashuka kutoka kitanda ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika."””
At illi responderunt ei: Vir occurrit nobis, et dixit ad nos: Ite, et revertimini ad regem, qui misit vos, et dicetis ei: Hæc dicit Dominus: Numquid, quia non erat Deus in Israel, mittis ut consulatur Beelzebub deus Accaron? Idcirco de lectulo, super quem ascendisti, non descendes, sed morte morieris.
7 Ahazi akawaambia wajumbe wake, “'Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana na ninyi na akasema haya maneno kwenu?”
Qui dixit eis: Cuius figuræ et habitus est vir ille, qui occurrit vobis, et locutus est verba hæc?
8 Wakamjibu, “Alikuwa amevaa kanzu yenye manyaya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunanoni kwake.'” Hivyo mfalme akajibu, '“Yule alikuwa Eliya Mtishbi.”
At illi dixerunt: Vir pilosus, et zona pellicea accinctus renibus. Qui ait: Elias Thesbites est.
9 Ndipo mfalme akatuma nahodha wa askari hamsini kwa Elya. Nahodha akaenda mpaka kwa Eliya ambapo alipokuwa amekaa juu ya mlima. Nahodha akamwambia Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme amesema, 'shuka chini.'”
Misitque ad eum quinquagenarium principem, et quinquaginta qui erant sub eo. Qui ascendit ad eum: sedentique in vertice montis, ait: Homo Dei, rex præcepit ut descendas.
10 Eliya akajibu na kusema kwa nahodha, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke chini kutoka mbinguni na kukula wewe na watu wako hamsini.” Kisha moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
Respondensque Elias, dixit quinquagenario: Si homo Dei sum, descendat ignis de cælo, et devoret te, et quinquaginta tuos. Descendit itaque ignis de cælo, et devoravit eum, et quinquaginta qui erant cum eo.
11 Tena Mfalme Ahazi akamtuma nahodha mwingine pamoja na maaskari wengine hamsini. Huyu nahodha pia akasema kwa Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme anasema, teremka chini haraka.”'
Rursumque misit ad eum principem quinquagenarium alterum, et quinquaginta cum eo. Qui locutus est illi: Homo Dei, hæc dicit rex: Festina, descende.
12 Eliya akajibu na kuwaambia, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, ngoja moto ushuke kutoka mbinguni na ukule wewe na watu wako hamsini.” Moto wa Mungu ukashuka chini tena kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
Respondens Elias ait: Si homo Dei ego sum, descendat ignis de cælo, et devoret te, et quinquaginta tuos. Descendit ergo ignis de cælo, et devoravit illum, et quinquaginta eius.
13 Bado tena mfalme alituma kundi la tatu la wapiganaji hamsini. Huyu nahodha akaenda, akaanguka mbele ya miguu ya Eliya, na kumsihi na kumwambia, “Wewe, mtu wa Mungu, Nakuomba, acha uzima wangu na uzima wa hawa watumishi wako hamsini uwe na thamani machoni kwako.
Iterum misit principem quinquagenarium tertium, et quinquaginta qui erant cum eo. Qui cum venisset, curvavit genua contra Eliam, et precatus est eum, et ait: Homo Dei, noli despicere animam meam, et animas servorum tuorum qui mecum sunt.
14 Ndipo, moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kuwala wale manahodha wawili wa kwanza pamoja na watu wao, bali sasa acha uzima wangu uwe na thamani machoni kwako.”
Ecce descendit ignis de cælo, et devoravit duos principes quinquagenarios primos, et quinquagenos, qui cum eis erant: sed nunc obsecro ut miserearis animæ meæ.
15 Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, “'Nenda chini pamoja naye. Usimwogope.”' Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme.
Locutus est autem Angelus Domini ad Eliam, dicens: Descende cum eo, ne timeas. Surrexit igitur, et descendit cum eo ad regem,
16 Baadye Eliya akamwambia Ahazia, '“Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Umewatuma wajumbe kuzungumza pamoja na Baal-Zebubu, mungu wa Ekron. Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ambaye unayeweza kumuuliza habari? Kwa hiyo sasa, hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ulichokipanda; utakufa hakika.'”
et locutus est ei: Hæc dicit Dominus: Quia misisti nuncios ad consulendum Beelzebub deum Accaron, quasi non esset Deus in Israel, a quo posses interrogare sermonem, ideo de lectulo, super quem ascendisti, non descendes, sed morte morieris.
17 Hivyo Mfalme Ahazia alikufa kulingana na neno la Yahwe ambalo Eliya alilisema. Yoramu alianza kutawala katika eneo lake, katika mwaka wa pili Yoramu mwana wa Yohoshafati mfalme wa Yuda, kwa sababu Ahazia hakuwa na mtoto.
Mortuus est ergo iuxta sermonem Domini, quem locutus est Elias, et regnavit Ioram frater eius pro eo, anno secundo Ioram filii Iosaphat regis Iudæ: non enim habebat filium.
18 Kama mambo mengine yanayomuhusu Ahazia, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
Reliqua autem verborum Ochoziæ, quæ operatus est, nonne hæc scripta sunt in Libro sermonum dierum regum Israel?