< 2 Yohana 1 >

1 Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake, ambao niwapendao katika kweli na si mimi tu, bali na wote wale wanao ifahamu kweli,
The Elder to the Elect Lady and her children, whom I love in truth, and not only I, but also all those who have come to know the truth.
2 kwa sababu ya kweli iliyomo ndani yetu na itakayodumu pamoja nasi milele. (aiōn g165)
I love you for the sake of the truth which is abiding in us and will be with us forever. (aiōn g165)
3 Neema, rehema, amani zitakuwa nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, katika kweli na pendo.
Grace, mercy, and peace will be with us from God the Father, and from Jesus Christ the Father’s Son, in truth and love.
4 Ninafurahi sana kwamba nimegundua baadhi ya watoto wanaenenda katika kweli, kama vile tu tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba.
I am greatly rejoiced to find some of your children leading their lives in truth, even as we received commandment from the Father.
5 Na sasa nakusihi wewe, mwanamke, siyo kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. Na huu ndiyo upendo, tunaopaswa kuenenda, kulingana na amri yake.
And now I am entreating you, Lady, not as though I were writing some new commandment to you, but one which we have had from the beginning, let us love one another.
6 Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo.
And this is love, that we should lead our lives according to his commandments. This is the commandment, even as you heard from the beginning, that you should pass your life in love.
7 Kwa kuwa wadanganyifu wengi wamesambaa katika ulimwengu, na hawakiri kwamba Yesu Kristo alikuja katika mwili. Huyu ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo.
I say this because many deceivers are gone forth into the world, those who deny the coming of Jesus Christ in the flesh. This is the deceiver and the Antichrist.
8 Jiangalieni wenyewe kwamba hampotezi mambo yale tuliyokwisha fanyia kazi, lakini ili kwamba mweze kuipokea tuzo kamili.
Watch yourselves, that you do not lose what we have wrought, but that you receive a full reward.
9 Yeyote aendeleae mbele na hadumu katika fundisho la Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana pia.
Whoever is going ahead, and is not abiding in the teachings of Christ, does not possess God; but he who is abiding in the teaching possesses both the Father and the Son.
10 Kama mtu anakuja kwenu na haleti fundisho hili, msimkaribishe katika nyumba zenu na msimsalimie.
If any one come to you and does not bring this teaching, do not receive him into your house, nor give him any greeting.
11 Kwa kuwa amsalimuye hushiriki katika matendo yake maovu.
For the man who greets him shares in his wicked work.
12 Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, na sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino. Lakini natumaini kuja kwenu na kuongea uso kwa uso, kwamba furaha yetu ipate kufanywa kamili.
I have many things to write to you, but I would not write them with paper and ink. I hope to come to you and to talk with you face to face, so that your joy may be full.
13 Watoto wa dada yenu mteule wanawasalimia.
The children of your elect sister send you greeting.

< 2 Yohana 1 >