< 2 Wakorintho 1 >
1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, na kwa waumini wote walioko katika mkoa wote wa Akaya.
Paul, apostle of Jesus Christ by God's will, and the brother Timotheus, to the assembly of God which is in Corinth, with all the saints who are in the whole of Achaia.
2 Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Grace to you, and peace from God our Father, and [the] Lord Jesus Christ.
3 Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote.
Blessed [be] the God and Father of our Lord Jesus Christ, the Father of compassions, and God of all encouragement;
4 Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi.
who encourages us in all our tribulation, that we may be able to encourage those who are in any tribulation whatever, through the encouragement with which we ourselves are encouraged of God.
5 Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo huongezeka kwa ajili yetu, vile vile faraja yetu huongezeka kupitia Kristo.
Because, even as the sufferings of the Christ abound towards us, so through the Christ does our encouragement also abound.
6 Lakini kama tunataabishwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na kama tunafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu. Faraja yenu inafanya kazi kikamilifu mnaposhiriki mateso kwa uvumilivu kama sisi pia tunavyoteseka.
But whether we are in tribulation, [it is] for your encouragement and salvation, wrought in the endurance of the same sufferings which we also suffer,
7 Na ujasiri wetu juu yenu ni thabiti. Tunajua kwamba kama vile ambavyo mnashiriki mateso, vile vile mnashiriki faraja.
(and our hope for you [is] sure; ) or whether we are encouraged, [it is] for your encouragement and salvation: knowing that as ye are partakers of the sufferings, so also of the encouragement.
8 Kwa kuwa hatutaki ninyi muwe wajinga, ndugu, kuhusu matatizo tuliyokuwa nayo huko Asia. Tulionewa zaidi ya vile tuwezavyo kubeba, kana kwamba hatukuwa hata na tumaini la kuishi tena.
For we do not wish you to be ignorant, brethren, as to our tribulation which happened [to us] in Asia, that we were excessively pressed beyond [our] power, so as to despair even of living.
9 Kweli, tulikuwa na hukumu ya kifo juu yetu. Lakini hiyo ilikuwa ni kutufanya sisi tusiweke tumaini juu yetu wenyewe, badala yake tuweke tumaini katika Mungu, afufuaye wafu.
But we ourselves had the sentence of death in ourselves, that we should not have our trust in ourselves, but in God who raises the dead;
10 Alituokoa sisi kutoka hayo maafa ya mauti, na atatuokoa tena. Tumeweka ujasiri wetu katika yeye ya kwamba atatuokoa tena.
who has delivered us from so great a death, and does deliver; in whom we confide that he will also yet deliver;
11 Atafanya hivi kama vile ninyi pia mtusaidiavyo kwa maombi yenu. Hivyo wengi watatoa shukurani kwa niaba yetu kwa ajili ya upendeleo wa neema tuliyopewa sisi kupitia maombi ya wengi.
ye also labouring together by supplication for us that the gift towards us, through means of many persons, may be the subject of the thanksgiving of many for us.
12 Tunajivunia hili: ushuhuda wa dhamiri yetu. Kwa kuwa ni katika nia safi na usafi wa Mungu kwamba tulienenda wenyewe katika dunia. Tumefanya hivi hasa na ninyi, na sio katika hekima ya ulimwengu, lakini badala yake ni katika neema ya Mungu.
For our boasting is this, the testimony of our conscience, that in simplicity and sincerity before God, (not in fleshly wisdom but in God's grace, ) we have had our conversation in the world, and more abundantly towards you.
13 Hatuwaandikii chochote ambacho hamwezi kukisoma au kuelewa. Ninaujasiri
For we do not write other things to you but what ye well know and recognise; and I hope that ye will recognise to the end,
14 kwamba kwa sehemu mumekwisha kutuelewa. Na ninaujasiri kwamba katika siku ya Bwana Yesu tutakuwa sababu yenu kwa ajili ya kiburi chenu, kama vile mtakavyokuwa kwetu.
even as also ye have recognised us in part, that we are your boast, even as ye [are] ours in the day of the Lord Jesus.
15 Kwa sababu nilikuwa na ujasiri kuhusu hili, nilitaka kuja kwenu kwanza, ili kwamba muweze kupokea faida ya kutembelewa mara mbili.
And with this confidence I purposed to come to you previously, that ye might have a second favour;
16 Nilikuwa napanga kuwatembelea wakati nikielekea Makedonia. Tena nilitaka kuwatembelea tena wakati nikirudi kutoka Makedonia, na kisha ninyi kunituma mimi wakati nikielekea Uyahudi.
and to pass through to Macedonia by you, and again from Macedonia to come to you, and to be set forward by you to Judaea.
17 Nilipokuwa nafikiria namna hii, je, nilikuwa nasitasita? Je ninapanga mambo kulingana na viwango vya kibinadamu, ili kwamba niseme “Ndiyo, ndiyo” na “Hapana, hapana” kwa wakati mmoja?
Having therefore this purpose, did I then use lightness? Or what I purpose, do I purpose according to flesh, that there should be with me yea yea, and nay nay?
18 Lakini kama vile Mungu alivyo mwaminifu, hatusemi vyote “Ndiyo” na “Hapana.”
Now God [is] faithful, that our word to you is not yea and nay.
19 Kwa kuwa mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye Silvano, Timotheo na mimi tulimtangaza miongoni mwenu, siyo “Ndiyo” na “Hapana.” Badala yake, yeye wakati wote ni “Ndiyo.”
For the Son of God, Jesus Christ, he who has been preached by us among you (by me and Silvanus and Timotheus), did not become yea and nay, but yea is in him.
20 Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni “Ndiyo” katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema “Amina” kwa utukufu wa Mungu.
For whatever promises of God [there are], in him is the yea, and in him the amen, for glory to God by us.
21 Sasa ni Mungu ambaye hututhibitisha sisi pamoja nanyi katika Kristo, na alitutuma sisi.
Now he that establishes us with you in Christ, and has anointed us, [is] God,
22 Aliweka muhuri juu yetu na alitupa Roho katika mioyo yetu kama dhamana ya kile ambacho angetupatia baadaye.
who also has sealed us, and given the earnest of the Spirit in our hearts.
23 Badala yake, namsihi Mungu kunishuhudia mimi kwamba sababu iliyonifanya nisije Korintho ni kwamba nisiwalemee ninyi.
But I call God to witness upon my soul that to spare you I have not yet come to Corinth.
24 Hii sio kwa sababu tunajaribu kudhibiti jinsi imani yenu inavyotakiwa kuwa. Badala yake, tunafanya pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu, kama mnavyosimama katika imani yenu.
Not that we rule over your faith, but are fellow-workmen of your joy: for by faith ye stand.