< 2 Wakorintho 9 >
1 Kuhusiana na huduma kwa ajili ya waumini, ni bora zaidi kwangu kuwaandikia.
Hakuna haja yangu kuwaandikia kuhusu huduma hii itolewayo kwa ajili ya watakatifu.
2 Ninajua kuhusu shauku yenu, ambayo nilijivunia kwa watu wa Makedonia. Niliwaambia kwamba Akaya imekuwa tayari tangu mwaka uliopita. Hamu yenu imewatia moyo wengi wao kutenda.
Kwa kuwa ninajua mlivyo na shauku ya kusaidia, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili ya jambo hilo kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana na shauku yenu imewachochea wengi wao katika kutoa.
3 Sasa, nimewatuma ndugu ili kwamba majivuno yetu kuhusu ninyi yasiwe ya bure, na ili kwamba mngekuwa tayari, kama nilivyosema mngekuwa.
Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusiwe maneno matupu, bali mpate kuwa tayari kama nilivyosema mngekuwa tayari.
4 Vinginevyo, kama mtu yeyote wa Makedonia akija pamoja nami na kuwakuta hamjawa tayari, tungeona haya — sisemi chochote kuhusu ninyi—kwa kuwa jasiri sana katika ninyi.
Kwa maana kama nikija na Mmakedonia yeyote na kuwakuta hamjawa tayari, tutaona aibu kusema chochote juu yenu katika matoleo.
5 Hivyo niliona ilikuwa muhimu kuwasihi ndugu kuja kwenu na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi mlizoahidi. Hii ni hivyo ili kwamba ziwe tayari kama baraka, na si kama kitu kilichoamriwa.
Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.
6 Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.
Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu.
7 Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha.
Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.
8 Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema.
Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.
9 Ni kama ilivyoandikwa: “Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele.” (aiōn )
Kama ilivyoandikwa: “Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele.” (aiōn )
10 Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu.
Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.
11 Mtatajirishwa kwa kila namna ili kwamba muweze kuwa wakarimu. Hii italeta shukrani kwa Mungu kupitia sisi.
Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.
12 Kwa kufanya huduma hii sio tu inagusa mahitaji ya waumini. Pia huzidisha katika matendo mengi ya shukrani kwa Mungu.
Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.
13 Kwa sababu ya kupimwa kwenu na kuthibitishwa kwa huduma hii, pia mtamtukuza Mungu kwa utii kwa ukiri wenu wa injili ya Kristo. Pia mtamtukuza Mungu kwa ukarimu wa karama yenu kwao na kwa kila mmoja.
Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.
14 Wanawatamani, na wanaomba kwa ajili yenu. Wanafanya hivi kwa sababu ya neema kubwa ya Mungu iliyo juu yenu.
Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu.
15 Shukrani ziwe kwa Mungu kwa karama yake isiyoelezeka!
Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.