< 2 Wakorintho 8 >
1 Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.
Basi sasa ndugu, nataka ninyi mjue kuhusu ile neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia.
2 Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu.
Pamoja na majaribu makali na taabu walizopata, furaha waliyokuwa nayo ilikuwa kubwa, ingawa walikuwa maskini kupindukia, kwa upande wao walifurika kwa wingi wa ukarimu.
3 Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza.
Kwa maana nashuhudia kwamba wao walitoa kwa kadiri wawezavyo, hata na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe,
4 Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini.
wakitusihi kwa bidii wapewe fursa ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watakatifu.
5 Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.
Wala hawakufanya tulivyotazamia, bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana kwanza na ndipo wakajitoa kwa ajili yetu, kufuatana na mapenzi ya Mungu.
6 Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu.
Kwa hiyo tulimsihi Tito, kwa kuwa ndiye alianzisha jambo hili, akamilishe tendo hili la neema kwa upande wenu.
7 Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu.
Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.
8 Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.
Siwaamrishi, lakini nataka kujaribu unyofu wa upendo wenu kwa kuulinganisha na bidii ya wengine.
9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.
Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri.
10 Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo. Lakini mlitamani kulifanya.
Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu juu ya jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo.
11 Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.
Sasa ikamilisheni kazi hii kwa shauku kama mlivyoanza, jitoleeni kulingana na uwezo wenu.
12 Kwa kuwa mnashauku ya kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.
Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kulingana na kile mtu alicho nacho, wala si kwa kile ambacho hana.
13 Kwa kuwa kazi hii siyo kwa ajili kwamba wengine waweze kupata nafuu na ninyi mweze kulemewa. Badala yake, kuwe na usawa.
Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano.
14 Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na usawa.
Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu.
15 Hii ni kama ilivyoandikwa; “Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote.”
Ndipo patakuwa na usawa, kama ilivyoandikwa: “Aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.”
16 Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.
Ninamshukuru Mungu ambaye amemtia Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali.
17 Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
Si kwamba Tito amekubali tu ombi letu, bali anakuja kwenu akiwa na shauku kuliko wakati mwingine, tena kwa hiari yake mwenyewe.
18 Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.
Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makanisa yote kwa huduma yake ya kuhubiri Injili.
19 Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.
Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makanisa ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana mwenyewe, na ili kuonyesha hisani yetu kuwasaidia.
20 Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.
Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu.
21 Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.
Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki si machoni mwa Bwana peke yake, bali pia machoni mwa watu wengine.
22 Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.
Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu.
23 Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.
Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtendakazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makanisa, na utukufu kwa Kristo.
24 Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.
Kwa hiyo waonyesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, mbele ya makanisa, ili yapate kuona.