< 2 Wakorintho 8 >

1 Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.
Twataka mwenga muitange, ainja na alombo, kuhusu neema ya Nnongo ambayo ititolewa kwa makanisa ga Makedonia.
2 Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu.
Wakati wa lijaribu kolo lya mateso, wingi wa puraha yabe ni ongezeko lya umaskini wabe upambike utajiri nkolo wa ukarimu.
3 Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza.
Kwa naaba nashuhudia panga batitoa kwa kadiri ya balioweza, na hata zaidi ya balioweza.
4 Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini.
Na kwa hiari yabembe bene kwa kutusihi kwingi, batulobite kwa ajili ya shiriki katika huduma yee kwa baumini.
5 Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.
Ayee itokana kwaa mana yatubile twatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa bembe bene kwa Ngwana. Boka po kabajitoa bembe bene kwitu kwa mapenzi ya Nnongo.
6 Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu.
Nga twatimsihi Tito, ywaabile tayari atianzisha kazi yee, kuleta katika ukamilifu tendo lee lya ukarimu nnani yinu.
7 Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu.
Lakini mwenga mubile baingi katika kila kilebe-katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo winu kwa ajili yitu. Nga nyoo muhakikishe panga mwenga mwabile na wingi kae katika likowe lee lya ukarimu.
8 Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.
Nabaya lee kati amri kwaa. Badala yake, nabaya lee ili kupima uhalisi wa upendo winu kwa linganisha na shauku ya bandu benge.
9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.
Kwa mana mutangite neema ya Ngwana witu Yesu Kristo. Hata mana abile tajiri, kwa ajili yinu abile maskini. ili panga pitya umaskini wake muweze kuwa tajiri.
10 Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo. Lakini mlitamani kulifanya.
Katika likowe lee nalowa kuwapea ushauri ambao utabasaidia. Mwaka umo waupitike, mtumbwe kwaa panga likowe. Lakini mwatitamaniya kulipanga.
11 Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.
Nambeambe mulikamilishe, Mana ibile na shauku na nia ya kulipanga, boka po, je mwaweza kae kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mwamuweza.
12 Kwa kuwa mnashauku ya kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.
Kwa kuwa mubile na shauku ya kupanga likowe lee, ni likowe linoite na lyakubalika. Lazima liyemite nnani ya chelo chabile nacho mundu, nnani kwaa ya abile nacho kwaa mundu.
13 Kwa kuwa kazi hii siyo kwa ajili kwamba wengine waweze kupata nafuu na ninyi mweze kulemewa. Badala yake, kuwe na usawa.
Kwa mana kazi yee ibile kwaa kwa ajili panga benge baweze kupata nafuu ni mwenga muweze lemewa. Badala yake, kube ni usawa.
14 Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na usawa.
Baingi binu wa wakati wambeambe utasaidia kwa chelo watikihitaji. Ayee nga nyoo kae ili panga baingi wabe uweze kuasaidia mahitaji yinu, na panga kuwe ni usawa.
15 Hii ni kama ilivyoandikwa; “Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote.”
Ayee nga kati yaiandikilwe;”Ywembe ywabile ni vingi abile kwaa na kilebe chochote chakibakile ni ywembe ywabile na kichunu chabile kwaa ni uhitaji wowote,”
16 Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.
Lakini ashukuriwe Nnongo, ywabekite nkati ya mwoyo wa Tito mwoyo wowolo kwa bidii ya kujali ambavyo nibile navyo kwa ajili yinu.
17 Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
Kwa mana apokile kwaa kae maombi yitu, ila abile na bidii husiana na maombi ago. Abile kwinu kwa hiyari yake mwene.
18 Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.
Tumtumite pamope ni ywembe nongo ambaye atisifiwa nkati mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kuitangaza injili.
19 Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.
Hivi kwaa kae, lakini achauliwe kae na makanisa kusafiri nitwenga katika kulipotwa sehemu mbalembale tendo lee lya ukarimu. Alee ni kwa utukufu wa Ngwana mwene na kwa shauku yitu ya kusaidia.
20 Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.
Twaepuka uwezekano wa panga yoyote aplikwa lalamika kuhusiana na twenga kuhusiana na ukarimu woo ambao twaupapite.
21 Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.
Twautola uangalifu kupanga cakibile chaheshima, nnonye kwaa ya Ngwana, lakini nnonge ya bandu kae,
22 Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.
Twantuma nongo ywenge pamope nabo. Twatimpema mara zanyansima, na tumweni abile ni shauku kwa ajili ya kazi zanyansima. Hata nambeambe abile na bidii muno kwa sababu ya ujasiri nkolo waabile nao nkati yinu.
23 Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.
Kwa habari ya Tito, ywembe ni mshirika mwenza wango na mpanga kazi mwenzanu kwa ajili yinu. Kati kwa alongo bitu, watumwile na makanisa. Nabaishimiya kwa Kristo.
24 Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.
Nga nyo, mubaoneshe upendo winu, na mubonekeye kwa makanisa sababu ya maipuno yitu kwa ajili yinu.

< 2 Wakorintho 8 >