< 2 Wakorintho 7 >

1 Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu.
Having therefore these promises, beloved, let us cleanse ourselves from every filthiness of flesh and spirit, perfecting holiness in fear of God.
2 Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote.
Make room for us. We wronged no man, we corrupted no man, we exploited no man.
3 Nasema hili siyo kwa kuwalaumu. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja.
I speak not for condemnation, for I have said before that ye are in our hearts to die together and to live together.
4 Nina ujasiri mwingi ndani yenu, na ninajivuna kwa ajili yenu. Nimejawa na faraja. Ninajawa na furaha hata katikati ya mateso yetu yote.
Great is my boldness toward you, great is my pride for you. I have been filled with encouragement. I over-abound with joy in all our affliction.
5 Tulikuja Makedonia, miili yetu haikuwa na pumziko. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani.
For even when we came into Macedonia our flesh had not one relief, but being oppressed in everything: battles outside, fears within.
6 Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito.
Nevertheless God, who encourages the lowly, encouraged us by the arrival of Titus.
7 Haikuwa kwa ujio wake tu kwamba Mungu alitufariji. ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na mlivyokuwa na wasiwasi kwa ajili yangu. Hivyo nimezidi kuwa na furaha zaidi.
And not only by his presence, but also by the encouragement with which he was encouraged by you, reporting to us your earnest desire, your mourning, your zeal for me, so that I rejoiced the more.
8 Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. lakini ninaujutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni. lakini mlikuwa na huzuni kwa muda mfupi.
Because even though I grieved you in the letter, I am not remorseful (even though I was remorseful), for I perceive that that letter grieved you, even though for an hour.
9 Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na shida, lakini kwa sababu huzuni zenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hivyo mliteswa si kwa hasara kwa sababu yetu.
Now I rejoice, not that ye were grieved, but that ye were grieved for repentance. For ye were grieved toward God, so that ye might suffer loss from us in nothing.
10 Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.
For sorrow toward God works repentance for salvation without regret, but the sorrow of the world works death.
11 Angalieni huzuni hii ya kiungu ilizalisha azma gani kubwa ndani yenu. Jinsi gani azma ilikuwa kubwa ndani yenu kuthibitisha kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia.
For behold this same thing-your grieving toward God. How much eagerness it worked in you, even a defense, even indignation, even fear, even longing, even zeal, even vengeance! In everything ye demonstrated yourselves to be pure in the matter.
12 Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu.
And so then, although I wrote to you, it was not because of the man who did wrong, nor because of the man who was wronged, but in order to reveal to you your eagerness for us in the sight of God.
13 Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote.
Because of this we have been encouraged. And from your encouragement, we rejoiced to a greater degree more at the joy of Titus, because his spirit has been refreshed by you all.
14 Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, Majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli.
Because, if I have boasted anything to him about you, I am not ashamed, but as we spoke all things in truth to you, so also our boast to Titus became truth.
15 Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka.
And his bowels are more abundant toward you, remembering the obedience of you all, how ye received him with fear and trembling.
16 Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.
I rejoice that I have confidence in you in everything.

< 2 Wakorintho 7 >