< 2 Wakorintho 6 >
1 Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo.
Adjuvantes autem exhortamur ne in vacuum gratiam Dei recipiatis.
2 Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu.
Ait enim: Tempore accepto exaudivi te, et in die salutis adjuvi te. Ecce nunc tempus acceptabile, ecce nunc dies salutis.
3 Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya.
Nemini dantes ullam offensionem, ut non vituperetur ministerium nostrum:
4 Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
sed in omnibus exhibeamus nosmetipsos sicut Dei ministros in multa patientia, in tribulationibus, in necessitatibus, in angustiis,
5 kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,
in plagis, in carceribus, in seditionibus, in laboribus, in vigiliis, in jejuniis,
6 katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi.
in castitate, in scientia, in longanimitate, in suavitate, in Spiritu Sancto, in caritate non ficta,
7 Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
in verbo veritatis, in virtute Dei, per arma justitiæ a dextris et a sinistris,
8 Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli.
per gloriam, et ignobilitatem, per infamiam, et bonam famam: ut seductores, et veraces, sicut qui ignoti, et cogniti:
9 Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa.
quasi morientes, et ecce vivimus: ut castigati, et non mortificati:
10 Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
quasi tristes, semper autem gaudentes: sicut egentes, multos autem locupletantes: tamquam nihil habentes, et omnia possidentes.
11 Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.
Os nostrum patet ad vos, o Corinthii; cor nostrum dilatatum est.
12 mioyo yenu haizuiliwi na sisi, bali mnazuiliwa na hisia zenu wenyewe.
Non angustiamini in nobis: angustiamini autem in visceribus vestris:
13 Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - fungueni mioyo yenu kwa upana.
eamdem autem habentes remunerationem, tamquam filiis dico, dilatamini et vos.
14 Msifungamanishwe pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna uhusiano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Nolite jugum ducere cum infidelibus. Quæ enim participatio justitiæ cum iniquitate? aut quæ societas luci ad tenebras?
15 Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?
quæ autem conventio Christi ad Belial? aut quæ pars fideli cum infideli?
16 Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
qui autem consensus templo Dei cum idolis? vos enim estis templum Dei vivi, sicut dicit Deus: [Quoniam inhabitabo in illis, et inambulabo inter eos, et ero illorum Deus, et ipsi erunt mihi populus.
17 Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.
Propter quod exite de medio eorum, et separamini, dicit Dominus, et immundum ne tetigeritis:
18 Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi.
et ego recipiam vos: et ero vobis in patrem, et vos eritis mihi in filios et filias, dicit Dominus omnipotens.]