< 2 Wakorintho 4 >

1 Kwa hiyo, kwa sababu tuna huduma hii, na kama ambavyo tumeipokea rehema, hatukati tamaa.
Wherefore, having this ministry, inasmuch as we have received mercy, we faint not;
2 Badala yake, tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika. Hatuishi kwa hila, na hatulitumii vibaya neno la Mungu. Kwa kuwasilisha iliyo kweli, tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu.
but we have renounced the secret works of shame, not walking in craftiness, nor adulterating the word of God; but, by the manifestation of the truth, commending ourselves to every man’s conscience in the sight of God.
3 Lakini kama injili yetu imefichika, imefichika kwa wale tu wanaoangamia.
But if our gospel is vailed, it is vailed among the lost,
4 Katika uchaguzi wao, mungu wa ulimwengu huu amewapofusha fahamu zao zisizoamini. Matokeo yake, hawawezi kuona nuru ya injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu. (aiōn g165)
whose unbelieving minds the god of this age has darkened, so that the light of the glorious gospel of Christ, who is the image of God, should not shine to them. (aiōn g165)
5 Kwa kuwa hatujitangazi wenyewe, bali Kristo Yesu kama Bwana, na sisi wenyewe kama watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
For we preach not ourselves, but Christ Jesus the Lord, and ourselves your servants, for Jesus sake.
6 Kwa kuwa Mungu ndiye ambaye aliyesema, “Mwanga utaangaza toka gizani.” Ameangaza katika mioyo yetu, kutoa mwanga wa maarifa ya utukufu wa Mungu katika uwepo wa Yesu Kristo.
Because God, who commanded the light to shine out of darkness, has shined in our hearts, to give the light of the glorious knowledge of God in the person of Jesus Christ.
7 Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kwamba ieleweke kuwa nguvu kuu sana ni ya Mungu na sio yetu.
But we have this treasure in earthen vessels, that the exceeding greatness of the power may be God’s and not our own.
8 Tunataabika katika kila hali, lakini hatusongwi. Twaona shaka lakini hatujawi na kukata tamaa.
We are pressed on all sides, yet not restrained; perplexed, but not in despair;
9 Tunateswa lakini hatujatelekezwa. Twatupwa chini lakini hatuangamizwi.
persecuted, but not forsaken; cast down, but not destroyed;
10 Siku zote tunabeba katika mwili wetu kifo cha Yesu, ili kwamba uzima wa Yesu uonekane pia katika miili yetu.
always bearing about in our body the violent death of the Lord Jesus, that the life also of Jesus may be made manifest in our body.
11 Sisi tulio hai siku zote tumetolewa kufa kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uhai wa Yesu uonekane katika miili yetu ya kibinadamu.
For we who live are continually delivered up to death for Jesus sake, that the life also of Jesus may be made manifest in our mortal flesh.
12 Kwa sababu hii, kifo kinafanya kazi ndani yetu, bali uzima unafanya kazi ndani yenu.
So, then, death is active in us, but life in you.
13 Lakini tuna roho ileile ya imani kulingana na kile kilicho andikwa: “Niliamini, na hivyo nilinena.” Sisi pia tunaamini, na hivyo pia tunanena.
But, having the same spirit of faith, according to that which is written, I believed, and for this reason I have spoken; we also believe, and for this reason we speak,
14 Tunajua kuwa yule aliye mfufua Bwana Yesu pia atatufufua sisi pamoja naye. Tunajua kuwa atatuleta sisi pamoja nanyi katika uwepo wake.
knowing that he who raised up the Lord Jesus will raise us up also by Jesus, and present us together with you.
15 Kila kitu ni kwa ajili yenu ili kwamba, kwa kadri neema inavyo enea kwa watu wengi, shukurani zizidi kuongezeka kwa utukufu wa Mungu.
For all these afflictions are for your sakes, that the favor which abounds to me, may, through the thanksgiving of the many, abound richly to the glory of God.
16 Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku.
For this reason we faint not: but though our outward man perish, yet the inward man is renewed day by day.
17 Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote. (aiōnios g166)
For our present light affliction works out for us an eternal fullness of glory, excelling all excellence, (aiōnios g166)
18 Kwa kuwa hatutazami kwa ajili ya vitu ambavyo vinaonekana, bali kwa ajili ya vitu visivyoonekana. Vitu tunavyoweza kuviona ni vya muda tu, bali vitu ambayo havionekani ni vya milele. (aiōnios g166)
while we look not at the things that are seen, but at the things that are not seen: for the things seen are temporal; but the things not seen are eternal. (aiōnios g166)

< 2 Wakorintho 4 >