< 2 Wakorintho 2 >
1 Kwa hiyo niliamua kwa sehemu yangu mwenyewe kwamba nisingekuja tena kwenu katika hali ya uchungu.
2 Kama niliwasababishia ninyi maumivu, ni nani angenifurahisha mimi, lakini ni yule ambaye aliumizwa na mimi?
3 Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote.
4 Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu.
5 Kama kuna yeyote amesababisha maumivu, hajasababisha tu kwangu, lakini kwa kiwango fulani - bila kuweka ukali zaidi - kwenu ninyi nyote.
6 Hii adhabu ya mtu huyo kwa wengi inatosha.
7 Kwa hiyo sasa badala ya adhabu, mnapaswa kumsamehe na kumfariji. Fanyeni hivi ili kwamba asiweze kushindwa na huzuni iliyozidi.
8 Kwa hiyo ninawatia moyo kuthibitisha upendo wenu hadharani kwa ajili yake.
9 Hii ndiyo sababu niliandika, ili kwamba niweze kuwajaribu na kujua kuwa kama ni watii katika kila kitu.
10 Kama mkimsamehe yeyote, na mimi pia namsamehe mtu huyo. Kile nilicho kisamehe - kama nimesamehe chochote-kimesamehewa kwa faida yenu katika uwepo wa Kristo.
11 Hii ni kwamba Shetani asije akatufanyia madanganyo. Kwa kuwa sisi sio wajinga kwa mipango yake.
12 Mlango ulifunguliwa kwangu na Bwana nilipokuja kwenye mji wa Troa kuhubiri injili ya Kristo pale.
13 Hata hivyo, sikuwa na amani ya moyo, kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito pale. Hivyo niliwaacha na nikarudi Makedonia.
14 Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye katika Kristo mara zote hutuongoza sisi katika ushindi. Kupitia sisi husambaza harufu nzuri ya maarifa yake mahala pote.
15 Kwa kuwa sisi kwa Mungu, ni harufu nzuri ya Kristo, wote kati ya wale waliookolewa na kati ya wale wanaoangamia.
16 Kwa watu ambao wanaangamia, ni harufu kutoka kifo hadi kifo. Kwa wale wanaookolewa, ni harufu nzuri kutoka uzima hadi uzima. Ni nani anayestahili vitu hivi?
17 Kwa kuwa sisi sio kama watu wengi wanaouza neno la Mungu kwa faida. Badala yake, kwa usafi wa nia, tunanena katika Kristo, kama vile tunavyotumwa kutoka kwa Mungu, mbele ya Mungu.