< 2 Nyakati 1 >

1 Selemani mwana wa Daudi, aliimariswa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.
ויתחזק שלמה בן דויד על מלכותו ויהוה אלהיו עמו ויגדלהו למעלה׃
2 Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.
ויאמר שלמה לכל ישראל לשרי האלפים והמאות ולשפטים ולכל נשיא לכל ישראל ראשי האבות׃
3 Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.
וילכו שלמה וכל הקהל עמו לבמה אשר בגבעון כי שם היה אהל מועד האלהים אשר עשה משה עבד יהוה במדבר׃
4 Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko katika Yerusalemu.
אבל ארון האלהים העלה דויד מקרית יערים בהכין לו דויד כי נטה לו אהל בירושלם׃
5 Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa. (Maandiko ya zamani yanasema
ומזבח הנחשת אשר עשה בצלאל בן אורי בן חור שם לפני משכן יהוה וידרשהו שלמה והקהל׃
6 Selemani akaenda huko kwenye kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutamia, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
ויעל שלמה שם על מזבח הנחשת לפני יהוה אשר לאהל מועד ויעל עליו עלות אלף׃
7 Mungu akamtokea Selemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?”
בלילה ההוא נראה אלהים לשלמה ויאמר לו שאל מה אתן לך׃
8 Selemani akasema kwa Mungu, “Umeonesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.
ויאמר שלמה לאלהים אתה עשית עם דויד אבי חסד גדול והמלכתני תחתיו׃
9 Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.
עתה יהוה אלהים יאמן דברך עם דויד אבי כי אתה המלכתני על עם רב כעפר הארץ׃
10 Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”
עתה חכמה ומדע תן לי ואצאה לפני העם הזה ואבואה כי מי ישפט את עמך הזה הגדול׃
11 Mungu akasema kwa Selemani, “Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maish marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfame, na hivi ndivyo nitafanya.
ויאמר אלהים לשלמה יען אשר היתה זאת עם לבבך ולא שאלת עשר נכסים וכבוד ואת נפש שנאיך וגם ימים רבים לא שאלת ותשאל לך חכמה ומדע אשר תשפוט את עמי אשר המלכתיך עליו׃
12 Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo.”
החכמה והמדע נתון לך ועשר ונכסים וכבוד אתן לך אשר לא היה כן למלכים אשר לפניך ואחריך לא יהיה כן׃
13 Kwa hiyo Selemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.
ויבא שלמה לבמה אשר בגבעון ירושלם מלפני אהל מועד וימלך על ישראל׃
14 Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1, 400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
ויאסף שלמה רכב ופרשים ויהי לו אלף וארבע מאות רכב ושנים עשר אלף פרשים ויניחם בערי הרכב ועם המלך בירושלם׃
15 Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
ויתן המלך את הכסף ואת הזהב בירושלם כאבנים ואת הארזים נתן כשקמים אשר בשפלה לרב׃
16 Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
ומוצא הסוסים אשר לשלמה ממצרים ומקוא סחרי המלך מקוא יקחו במחיר׃
17 Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.
ויעלו ויוציאו ממצרים מרכבה בשש מאות כסף וסוס בחמשים ומאה וכן לכל מלכי החתים ומלכי ארם בידם יוציאו׃

< 2 Nyakati 1 >