< 2 Nyakati 9 >
1 Malikia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Selemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa
Malkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Solomoni, huyo malkia akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Alifika akiwa na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani, alikuja kwa Solomoni na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake.
2 Selemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Selemani akamjibu maswaali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Selemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
Solomoni akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake asiweze kumwelezea.
3 Malikia wa Sheba alipoiona hekima ya Selemani na ikulu aliyokuwa amejenga,
Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Solomoni na jumba la kifalme alilokuwa amejenga,
4 chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumisshi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.
chakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika Hekalu la Bwana alipatwa na mshangao.
5 Akasema kwa mfalme, “Ni kweli, taarifa ninioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.
Akamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli.
6 Sikuamini nilichokisika mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.
Lakini sikuamini yaliyosemwa hadi nilipokuja na kuona kwa macho yangu mwenyewe. Naam, sikuambiwa hata nusu yake; katika hekima na mali umezidi sana kuliko ile taarifa niliyoisikia.
7 Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. (Baadhi ya maandiko yanasema, “Wambarikiwa wake zako”, ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10: 8).
Heri watu wako! Heri hawa maafisa wako wasimamao mbele yako daima na kusikia hekima yako!
8 Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako inaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.
Ahimidiwe Bwana Mungu wako, ambaye amependezwa sana nawe, na akakuweka juu ya kiti chake cha ufalme utawale kwa niaba ya Bwana Mungu wako. Kwa sababu ya upendo wa Mungu wako kwa Israeli na shauku yake ya kuwadhibitisha milele, amekufanya wewe mfalme juu yao, ili kudumisha haki na uadilifu.”
9 Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vit vya thamani. Selemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki amabacho alipewa na malakia wa Sheba.
Naye akampa mfalme talanta 120 za dhahabu, kiasi kikubwa cha vikolezi na vito vya thamani. Haikuwahi kamwe kuletwa vikolezi vizuri kama vile Malkia wa Sheba alivyompa Mfalme Solomoni.
10 Watumishi wa Hiramau na wa mfalme Selemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali, na vito vya thamani.
(Watumishi wa Hiramu na wa Solomoni wakaleta dhahabu kutoka Ofiri, tena wakaleta shehena kubwa ya miti ya msandali na vito vya thamani.
11 Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Selemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.
Mfalme akatumia hiyo miti ya msandali kuwa ngazi kwa ajili ya Hekalu la Bwana na kwa jumba la kifalme, pia kwa kutengeneza vinubi na zeze kwa ajili ya waimbaji. Kiasi hicho kingi cha msandali hakijawahi kuingizwa Yuda tangu siku ile.)
12 Mfalme Selemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Selemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na wataumishsi wake.
Mfalme Solomoni akampa Malkia wa Sheba kila kitu alichotamani na kukiomba, zaidi ya vile alivyokuwa amemletea mfalme. Kisha malkia akaondoka na kurudi katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
13 Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Selemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,
Uzito wa dhahabu ambayo Solomoni alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666,
14 nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Walme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Selemanai dhahabu na fedha.
mbali na mapato yaliyoletwa na wafanyabiashara na wachuuzi. Wafalme wote wa Arabuni na watawala wa nchi wakamletea Solomoni dhahabu na fedha.
15 Mfalme Selemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.
Mfalme Solomoni akatengeneza ngao kubwa 200 kwa dhahabu iliyofuliwa. Kila ngao ilikuwa na dhahabu yenye uzito wa shekeli 600
16 Pia akatengeneza ngao mia tatu za shahabu iliyopigwa. Minas tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.
Akatengeneza pia ngao ndogo 300 za dhahabu iliyofuliwa, kila ngao ikiwa na uzito wa mane tatu za dhahabu. Mfalme akaziweka katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni.
17 Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.
Kisha mfalme akatengeneza kiti kikubwa cha kifalme kwa kutumia pembe za ndovu na kukifunika kwa dhahabu safi.
18 Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiti cha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.
Kiti hicho kilikuwa na ngazi sita na mahali pa kuwekea miguu vyote vya dhahabu. Pande zote za kiti kulikuwa na mahali pa kuegemeza mikono, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
19 Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.
Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote.
20 Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Selemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Selemani.
Vikombe vyote vya Mfalme Solomoni vya kunywea vilikuwa vya dhahabu na vyombo vyote vya nyumbani katika Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu kilichotengenezwa kwa fedha, kwa sababu fedha ilionekana ya thamani ndogo wakati wa Solomoni.
21 Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.
Mfalme alikuwa na meli nyingi za biashara baharini zilizoendeshwa na watu wa Hiramu. Kwa mara moja kila miaka mitatu zilirudi, zikiwa zimebeba dhahabu, fedha, pembe za ndovu na nyani wakubwa na wadogo.
22 Kwa hiyo Mfalme Selemani aliawazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.
Mfalme Solomoni alikuwa mkuu zaidi kwa utajiri na hekima kuliko wafalme wote wa dunia.
23 Dunia yote waliutafuta uwepo wa Selemanai ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
Wafalme wote wa dunia wakatafuta kukutana na Solomoni ili kusikia hekima ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
24 Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na anyumbu, mwaka baada ya mwaka.
Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.
25 Selemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
Solomoni alikuwa na mabanda 4,000 kwa ajili ya farasi na magari ya vita, farasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji ya magari ya vita na katika Yerusalemu pamoja naye.
26 Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.
Solomoni akatawala juu ya wafalme wote kuanzia Mto Frati mpaka kwenye nchi ya Wafilisti na kuendelea hadi mpaka wa Misri.
27 Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya aridhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.
Mfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani.
28 Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Selemani.
Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka nchi nyingine zote.
29 Kwa mambo mengine kuhusu Selemani, mwanzo na mwisho, hayajandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati?
Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati?
30 Selemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu.
31 Akalala na babu zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.
Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.