< 2 Nyakati 8 >

1 Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Selemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye,
[撒羅滿的其他建設]撒羅滿建造上主的殿和自己的王宮歷時二十年;二十年過後,
2 kwamba Selemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli.
撒羅滿又重建了希蘭還給他的城邑,令以色列子民住在那裏。
3 Selemani akauavamia Hamathzoba, akaushinda.
此後,撒羅滿到了哈瑪特祚巴,征服了那地。
4 Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi.
又修建了在曠野裏的塔德摩爾,在哈瑪特四周修築了儲藏城。
5 Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji iliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo.
又修築了上貝特曷龍和下貝特曷龍,作為有牆有門有閂的設防城。
6 Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake.
又建築了巴阿拉特和所屬於撒羅滿的儲藏城,以及一切屯車城和騎兵城;凡撒羅滿願意在耶路撒冷、黎巴嫩以及他所管轄的境內所要建設的,都已建設了。
7 Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli,
至於其餘的人民,即那些不屬以色列的赫特人、阿摩黎人、培黎齊人、希威人和耶步斯人,
8 watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambaoa watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Selemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo.
以色列子民沒有消滅,而他們凡留在此地的子孫,撒羅滿都徵來充作苦役,直到今天仍是如此。
9 Vile vile, Selemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshsi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake.
撒羅滿並沒有使以色列子民為他的工作擔任苦役,因為他們是他的戰士、將官、戰車長和騎兵長。
10 Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Selemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi.
撒羅滿的監察官,共有二百五十人,監管百姓。
11 Selemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, “Mke wangu lazima asiishi kataika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni takatifu”.
撒羅滿又將法郎的女兒,從達味城搬到為她建築的宮中,因為他說:「連我的妻子,也不可住在以色列王達味的宮中,因為上主約櫃所到的地方是聖地。」
12 Kisha Selemani akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi.
那時,撒羅滿在上主的祭壇上,即他在門廊前所築的祭壇上,向上主獻了全燔祭;
13 Akatoa sadaka kama ilivyohitaka katika ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amari ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.
並按梅瑟的吩咐,在安息日、新月和每年的三個節期:無酵節、七七節和帳棚節,奉獻每日應獻的祭品。
14 Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Selemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsisfu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia.
它又照他父親達味的規定,為司祭派定了班次,各盡其職;又規定了肋未人的任務,令他們負責讚頌;照每日的定例,在司祭前服務;又派定了門丁,按照他們的班次守衛各門,因為天主的人達味是如此命令的。
15 Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina.
君王對司祭和肋未人所吩咐的任何職務,以及管理府庫的事,他們都沒有違抗。
16 Kazi yote aliyoagizwa na Selemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika.
由上主的殿奠基之日起,以迄完成,撒羅滿的一切工作完備無缺;上主的殿於是告成。
17 Kisha Selemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu.
此後,撒羅滿往厄東地,到了濱海的厄茲雍革貝爾及厄拉特。
18 Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na Selemani na watumishi wa Semani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Selemani.
希蘭派遣自己的臣僕給他送來了船隻和善於航海的人;他們與撒羅滿的僕人同往敖非爾去,從那裏裝載了黃金四百五十「塔冷通,」運到撒羅滿王那裏。

< 2 Nyakati 8 >