< 2 Nyakati 4 >
1 Vivile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.
솔로몬이 또 놋으로 단을 만들었으니 장이 이십 규빗이요, 광이 이십 규빗이요 고가 십 규빗이며
2 Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.
또 바다를 부어 만들었으니 직경이 십 규빗이요, 그 모양이 둥글며 그 고는 다섯 규빗이요, 주위는 삼십 규빗 줄을 두를 만하며
3 Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,
그 가장자리 아래에는 돌아가며 소 형상이 있는데 매 규빗에 소가 열씩 있어서 바다 주위에 둘렸으니 그 소는 바다를 부어 만들 때에 두줄로 부어 만들었으며
4 Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
그 바다를 열두소가 받쳤으니 셋은 북을 향하였고, 셋은 서를 향하였고, 셋은 남을 향하였고, 셋은 동을 향하였으며 바다를 그 위에 놓았고 소의 뒤는 다 안으로 두었으며
5 Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
바다의 두께는 한 손넓이만 하고 그 가는 백합화의 식양으로 잔가와 같이 만들었으니 그 바다에는 삼천 밧을 담겠으며
6 Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanayia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makauhani kuoga humo.
또 물두멍 열을 만들어 다섯은 우편에 두고 다섯은 좌편에 두어 씻게 하였으며 그 바다는 제사장들의 씻기를 위한 것이더라
7 Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
또 정식을 따라 금으로 등대 열을 만들어 외소 안에 두었으니 좌편에 다섯이요, 우편에 다섯이며
8 Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.
또 상 열을 만들어 외소 안에 두었으니 좌편에 다섯이요, 우편에 다섯이며 또 금으로 대접 일백을 만들었고
9 Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.
또 제사장의 뜰과 큰 뜰과 뜰문을 만들고 놋으로 그 문짝에 입혔고
10 Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.
그 바다는 전 우편 동남방에 두었더라
11 Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Selemani katika nyumba ya Mungu:
후람이 또 솥과 부삽과 대접을 만들었더라 이와 같이 후람이 솔로몬 왕을 위하여 하나님의 전에서 하는 일을 마쳤으니
12 zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
곧 기둥 둘과 그 기둥 꼭대기의 공 같은 머리 둘과 또 기둥 꼭대기의 공 같은 기둥 머리를 가리우는 그물 둘과
13 Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
또 그 그물들을 위하여 만든 바 매 그물에 두 줄씩으로 기둥 위의 공 같은 두 머리를 가리우게 한 사백 석류와
14 Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
또 받침과 받침 위의 물두멍과
15 bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
한 바다와 그 바다 아래 열 두 소와
16 pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Selemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
솥과 부삽과 고기 갈고리와 여호와의 전의 모든 그릇들이라 후람의 아비가 솔로몬 왕을 위하여 빛난 놋으로 만들 때에
17 Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.
왕이 요단 평지에서 숙곳과 스레다 사이의 차진 흙에 그것들을 부어 내었더라
18 Hivyo ndivyo Selemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.
이와 같이 솔로몬이 이 모든 기구를 심히 많이 만들었으므로 그 놋 중수를 능히 측량할 수 없었더라
19 Selemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
솔로몬이 또 하나님의 전의 모든 기구를 만들었으니 곧 금단과 진설병 상들과
20 vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
내소 앞에서 규례대로 불을 켤 정금 등대와 그 등잔이며
21 na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
또 순정한 금으로 만든 꽃과 등잔과 화젓가락이며
22 Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlanago wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.
또 정금으로 만든 불집게와 주발과 숟가락과 불 옮기는 그릇이며 또 전 문 곧 지성소의 문과 외소의 문을 금으로 입혔더라