< 2 Nyakati 36 >
1 Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.
국민이 요시야의 아들 여호아하스를 세워 그 부친을 대신하여 예루살렘에서 왕을 삼으니
2 Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.
여호아하스가 위에 나아갈 때에 나이 이십 삼세더라 저가 예루살렘에서 치리한지 석달에
3 Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akaitoza nchi faini ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.
애굽 왕이 예루살렘에서 그 위를 폐하고 또 그 나라로 은 일백 달란트와 금 한 달란트를 벌금으로 내게하며
4 Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadili jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.
애굽 왕 느고가 또 그 형제 엘리아김을 세워 유다와 예루살렘 왕을 삼고 그 이름을 고쳐 여호야김이라 하고 그 형제 여호아하스를 애굽으로 잡아 갔더라
5 Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya ambayao yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
여호야김이 위에 나아갈 때에 나이 이십 오세라 예루살렘에서 십 일년을 치리하며 그 하나님 여호와 보시기에 악을 행하였더라
6 Kisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.
바벨론 왕 느부갓네살이 올라와서 치고 저를 쇠사슬로 결박하여 바벨론으로 잡아가고
7 Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.
느부갓네살이 또 여호와의 전 기구들을 바벨론으로 가져다가 바벨론에 있는 자기 신당에 두었더라
8 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana zidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yehoyakimu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
여호야김의 남은 사적과 그 행한 모든 가증한 일과 그 심술이 이스라엘과 유다 열왕기에 기록되니라 그 아들 여호야긴이 대신하여 왕이 되니라
9 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miezi mitatu na siku kumi katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe.
여호야긴이 위에 나아갈 때에 나이 팔세라 예루살렘에서 석달 열흘을 치리하며 여호와 보시기에 악을 행하였더라
10 Katika kipindi cha mwisho wa mwaka, mfalme Nebukadreza akatuma watu na wakampelekea Babeli, vitu vya thamani kutoka katika anyumba ya Yahwe, na kumfanya Sedekia ndugu yake, mfalame juu ya Yuda na Yerusalemu.
세초에 느부갓네살이 보내어 여호야긴을 바벨론으로 잡아가고 여호와의 전의 귀한 기구도 함께 가져가고 그 아자비 시드기야를 세워 유다와 예루살렘 왕을 삼았더라
11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka isshirini na moja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliokuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
시드기야가 위에 나아갈 때에 나이 이십 일세라 예루살렘에서 십 일년을 치리하며
12 Hakujinyenyekesha mwenyewe mbele za Yeremia nabii, ambaye alisema kutoka kwenye kinywa cha Yahwe.
그 하나님 여호와 보시기에 악을 행하고 선지자 예레미야가 여호와의 말씀으로 일러도 그의 앞에서 겸비치 아니하였으며
13 Sedekia pia akaasi zidi ya Mfalme Nebukadreza, ambaye alikuwa amemfanya aape uaminifu kwake kupitia Mungu. Lakini Sedekia aliishupaza shingo yake na kuufanya moyo wake mgumu usigeuke kwa Yahwe, Mungu wa Israeli.
느부갓네살왕이 저로 그 하나님을 가리켜 맹세케 하였으나 저가 배반하고 목을 곧게 하며 마음을 강퍅케 하여 이스라엘 하나님 여호와께로 돌아오지 아니하였고
14 Vilevile, viongozi wote wa makauhanai na wa watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Waliigoshi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu.
제사장의 어른들과 백성도 크게 범죄하여 이방 모든 가증한 일을 본받아서 여호와께서 예루살렘에 거룩하게 두신 그 전을 더럽게 하였으며
15 Yahwe, Mungu wa babu zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi.
그 열조의 하나님 여호와께서 그 백성과 그 거하시는 곳을 아끼사 부지런히 그 사자들을 그 백성에게 보내어 이르셨으나
16 Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwackeka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka zidi ya watu wake, hadi pailipokosekana msaada.
그 백성이 하나님의 사자를 비웃고 말씀을 멸시하며 그 선지자를 욕하여 여호와의 진노로 그 백성에게 미쳐서 만회할 수 없게 하였으므로
17 Hivyo Mungu alimpeleka juu yao mfalme wa Wakaldayo, ambaye aliwaua vijana wao kwa upanga ndani ya patakatifu, na hakuwa na huruma juu ya vijana au mabikra, watu wazee au wenye mvi. Mungu akawatoa wote mikononi mwake.
하나님이 갈대아 왕의 손에 저희를 다 붙이시매 저가 와서 그 성전에서 칼로 청년을 죽이며 청년 남녀와 노인과 백발노옹을 긍휼히 여기지 아니하였으며
18 Vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za nyumba ya Yahwe, na hazina za mfalme na watumishi wake—vyote hivi akavipeleka Babeli.
또 하나님의 전의 대소 기명들과 여호와의 전의 보물과 왕과 방백들의 보물을 다 바벨론으로 가져가고
19 Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaharibu vitu vizuri vyote ndani yake.
또 하나님의 전을 불사르며 예루살렘 성을 헐며 그 모든 궁실을 불사르며 그 모든 귀한 기명을 훼파하고
20 Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi kwa ajili yake na wanawe hadi utawala wa Waajemi.
무릇 칼에서 벗어난 자를 저가 바벨론으로 사로잡아가매 무리가 거기서 갈대아 왕과 그 자손의 노예가 되어 바사국이 주재할 때까지 이르니라
21 Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii.
이에 토지가 황무하여 안식년을 누림 같이 안식하여 칠십년을 지내었으니 여호와께서 예레미야의 입으로 하신 말씀이 응하였더라
22 Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho ya Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika uflme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema,
바사 왕 고레스 원년에 여호와께서 예레미야의 입으로 하신 말씀을 응하게 하시려고 바사 왕 고레스의 마음을 감동시키시매 저가 온 나라에 공포도 하고 조서도 내려 가로되
23 “Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumbaa kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambao upo Yuda. Yeyote aliyemiongoni mwenu kutoma katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Aende kwenye ile nchi.”
바사 왕 고레스는 말하노니 하늘의 신 여호와께서 세상 만국으로 내게 주셨고 나를 명하여 유다 예루살렘에 전을 건축하라 하셨나니 너희 중에 무릇 그 백성 된 자는 다 올라갈찌어다 너희 하나님 여호와께서 함께하시기를 원하노라 하였더라