< 2 Nyakati 35 >
1 Yosia asherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
2 Akawaweka makauhuni katika nafasi zao na akawatia moyo katika hudumza za nyumba ya Yahwe.
3 Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakifu kwa Yahwe. “Liwekeni sanduka takatifu katika nyumba ambayo Selemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Msilibebe kuzunguka nalo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.
4 Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za babu zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Selemani, mwaye.
5 Simeni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa bdugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.
6 Chinjeni wanakondoo wa Paska, jitakaseni wenyewe, andaeni wankondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa”.
7 Yosia akawapa watu wote wanakondoo elfu thelathini na wanambuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote walikuwepo. Pia akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalame.
8 Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilki, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2, 600 na maksai mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Paska.
9 Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi ndama elfu tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.
10 Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mjibu wa agizo la mfalme.
11 Wakawachinja wanakondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wanakondoo.
12 Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababu wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.
13 Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wayapeleka kwa watu.
14 Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametingwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.
15 Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagiwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuviacha vituo vyao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizi kwa ajili yao.
16 Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.
17 Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaishika Sabato wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.
18 Pasika kama hiyo haijafanyika tena katika Israeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.
19 Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na nane ya utawala wa Yosia.
20 Baada ya haya yote, baada ya Yosia kuliweka hekalu katika utaratibu, Neko, mfalme wa Misiri, akaenda juu kupigana dhidi ya Karkemist karibu na mto Frati, na Yosia akaenda kupigana juu yake.
21 Lakini Niko akatuma wajumbe kwake, akisema, “Nikufanye nini, mfalme wa Yuda? Leo siji kinyume nawe, lakini dhidi ya nyumba ambayo nafanya vita nayo. Mungu ameniamuru kuwahi, hivyo acha kumwingilia Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”
22 Hata hivyo, Yosia alipuuzia kurudi nyuma. Akajibadili ili apigane naye. Hakusikiliza maneno ya Neko ambayo yalikuja kutoka kwenye kinywa cha Mungu; hivyo akaenda kupigana kataika bonde la Megido.
23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, “Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya.”
24 Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alzikwa katika makaburi ya babu zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.
25 Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.
26 Kwa mambao mengine kuhusu Yosia, na matendo yake mema aliyoyafanya katika utii kwa kile kilichoandikwa katika sheria ya Yahwe—
27 na matendo yake, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.