< 2 Nyakati 33 >

1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.
בן שתים עשרה שנה מנשה במלכו וחמשים וחמש שנה מלך בירושלם׃
2 Akafanya yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.
ויעש הרע בעיני יהוה כתועבות הגוים אשר הוריש יהוה מפני בני ישראל׃
3 Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanaamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.
וישב ויבן את הבמות אשר נתץ יחזקיהו אביו ויקם מזבחות לבעלים ויעש אשרות וישתחו לכל צבא השמים ויעבד אתם׃
4 Manase akajenga madhbahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa amemwamuru, “Ni katika Yerusalemu ambamo jina langu litawekwa milele”.
ובנה מזבחות בבית יהוה אשר אמר יהוה בירושלם יהיה שמי לעולם׃
5 Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.
ויבן מזבחות לכל צבא השמים בשתי חצרות בית יהוה׃
6 Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanaye katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akassoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na wale waliozungumza na na roho. Akafanaya maaovu mengi katika mcho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.
והוא העביר את בניו באש בגי בן הנם ועונן ונחש וכשף ועשה אוב וידעוני הרבה לעשות הרע בעיני יהוה להכעיסו׃
7 Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaipeleka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Selemani mwanaye; alikuwa amesema, “Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchangua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.
וישם את פסל הסמל אשר עשה בבית האלהים אשר אמר אלהים אל דויד ואל שלמה בנו בבית הזה ובירושלם אשר בחרתי מכל שבטי ישראל אשים את שמי לעילום׃
8 Sitawaondoa tena watu wa Israeli katina nchi hii ambayo niliitoa kwa babu zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa.”
ולא אוסיף להסיר את רגל ישראל מעל האדמה אשר העמדתי לאבתיכם רק אם ישמרו לעשות את כל אשר צויתים לכל התורה והחקים והמשפטים ביד משה׃
9 Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.
ויתע מנשה את יהודה וישבי ירושלם לעשות רע מן הגוים אשר השמיד יהוה מפני בני ישראל׃
10 Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.
וידבר יהוה אל מנשה ואל עמו ולא הקשיבו׃
11 Kwa hiyo Yahwe akaleta juu yao maamri jeshsi wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.
ויבא יהוה עליהם את שרי הצבא אשר למלך אשור וילכדו את מנשה בחחים ויאסרהו בנחשתים ויוליכהו בבלה׃
12 Manase alipokuwa katika dhika, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa babu zake.
וכהצר לו חלה את פני יהוה אלהיו ויכנע מאד מלפני אלהי אבתיו׃
13 Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.
ויתפלל אליו ויעתר לו וישמע תחנתו וישיבהו ירושלם למלכותו וידע מנשה כי יהוה הוא האלהים׃
14 Baada ya hayo, manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.
ואחרי כן בנה חומה חיצונה לעיר דויד מערבה לגיחון בנחל ולבוא בשער הדגים וסבב לעפל ויגביהה מאד וישם שרי חיל בכל הערים הבצרות ביהודה׃
15 Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.
ויסר את אלהי הנכר ואת הסמל מבית יהוה וכל המזבחות אשר בנה בהר בית יהוה ובירושלם וישלך חוצה לעיר׃
16 Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.
ויכן את מזבח יהוה ויזבח עליו זבחי שלמים ותודה ויאמר ליהודה לעבוד את יהוה אלהי ישראל׃
17 Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao pekee.
אבל עוד העם זבחים בבמות רק ליהוה אלהיהם׃
18 Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.
ויתר דברי מנשה ותפלתו אל אלהיו ודברי החזים המדברים אליו בשם יהוה אלהי ישראל הנם על דברי מלכי ישראל׃
19 Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maomabi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kambla ya kujinyenyekesha mwenyewe — na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. (Maandishi ya kale yanasema hivi, “tarehe ya Hozai,” ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka “tarehe ya waonaj” Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema “tarehe ya waonaji”.).
ותפלתו והעתר לו וכל חטאתו ומעלו והמקמות אשר בנה בהם במות והעמיד האשרים והפסלים לפני הכנעו הנם כתובים על דברי חוזי׃
20 Kwa hiyo Manase akalala na babu zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
וישכב מנשה עם אבתיו ויקברהו ביתו וימלך אמון בנו תחתיו׃
21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu.
בן עשרים ושתים שנה אמון במלכו ושתים שנים מלך בירושלם׃
22 Akafanya yaliyokuwa uovu katika macho ya Yaahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka katika sanamau zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu.
ויעש הרע בעיני יהוה כאשר עשה מנשה אביו ולכל הפסילים אשר עשה מנשה אביו זבח אמון ויעבדם׃
23 Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni huyu huyu alifanya makosa zaidi na zaidi.
ולא נכנע מלפני יהוה כהכנע מנשה אביו כי הוא אמון הרבה אשמה׃
24 Watumishi wake wakapanga njama wa zidi yake na wakamua katika nyumba yake mwenyewe.
ויקשרו עליו עבדיו וימיתהו בביתו׃
25 Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya njama zidi ya Mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia, mwanaye, mfalme katika nafasi yake.
ויכו עם הארץ את כל הקשרים על המלך אמון וימליכו עם הארץ את יאשיהו בנו תחתיו׃

< 2 Nyakati 33 >