< 2 Nyakati 32 >
1 Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake.
Efter disse Tildragelser og disse Vidnesbyrd om Troskab kom Assyrerkongen Sankerib og rykkede ind i Juda og belejrede de befæstede Byer i det Øjemed at bemægtige sig dem.
2 Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana zidi ya Yerusalemu,
Da Ezekias så, at Sankerib kom, og at han havde i Sinde at angribe Jerusalem,
3 aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo.
rådførte han sig med sine Hærførere og tapre Folk om at stoppe for Vandet i Kilderne uden for Byen, og de tilsagde ham deres Hjælp.
4 Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. wakasema, “Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?”
Så samledes en Mængde Folk, og de stoppede for alle Kilderne og for Bækken, som løber midt igennem Landet, idet man sagde: "Hvorfor skulde Assyrerkongerne finde rigeligt Vand, når de kommer?"
5 Hezekia akijipa ujasiri na kuujeenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Dudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. (Maanshi ya kale yanasema hivi: “Badala ya, “akajenga minara amirefu”, baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, “akajenga minara mirefu juu yake”, Hii ni juu ya ukuta).
Derpå tog han Mod til sig og byggede Muren op, overalt hvor den var brudt ned, og byggede Tårne på den, og han byggede den anden Mur udenfor og befæstede Millo i Davidsbyen og lod lave en Mængde Kastevåben og Skjolde.
6 Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema,
Tillige indsatte han Hærtørere over Krigsfolket, samlede dem om sig på den åbne Plads ved Byporten og talte opmuntrende Ord til dem og sagde:
7 “Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko
"Vær frimodige og slærke; frygt ikke og forfærdes ikke for Assyrerkongen og hele den Menneskemængde, han har med sig; thi en større er med os end med ham!
8 walio naye mfalme wa Ashuru. walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupiagana vita vyetu.” Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
Med ham er en Arm at Kød, men med os er HERREN vor Gud, der vil hjælpe os og føre vore Krige!" Og Folket satte sin Lid til Kong Ezekias af Judas Ord.
9 Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yetusalemu (sasa alikuwa mbe ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema,
Derefter sendte Assyrerkongen Sankerib, der selv med hele sin Krigsmagt lå foran Lakisj, sine. Tjenere til Kong Ezekias af Juda og alle Judæerne i Jerusalem og lod sige:
10 “Hivi ndivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu?
"Således siger Assyrerkongen Sankerib: Hvad er det, I fortrøster eder til, nu I sidder indesluttet i Jerusalem?
11 Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, “Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?
Mon ikke Ezekias lokker eder til at dø af Hunger og Tørst, når han siger: HERREN vor Gud vil frelse os af Assyrerkongens Hånd!
12 Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu?
Har ikke samme Ezekias skaffet hans Offerhøje og Altre bort og sagt til Juda og Jerusalem: Kun foran et eneste Alter må I tilbede, og på det skal I tænde Offerild!
13 Je, hamjui mimi na babu zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa inchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao zidi ya nguvu zangu?
Ved I ikke, hvad jeg og mine Fædre har gjort ved alle Landenes Folkeslag? Mon Landenes Folks Guder kunde frelse deres Land af min Hånd?
14 Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo amabayo babu zangu waliwatekeza, je, kulikuwa na muungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi zidi ya nguvu zangu?
Hvilken af alle de Guder, som dyrkedes af disse Folk, på hvilke mine Fædre lagde Band, har kunnet frelse sit Folk af min Hånd? Og så skutlde eders Gud kunne frelse eder af min Hånd!
15 Sasa msimuruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna muungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa babu zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?
Lad derfor ikke Ezekias vildlede eder og lokke eder på den Måde! Tro ham ikke, thi ikke et eneste Folks eller Riges Gud har kunnet frelse sit Folk af min Hånd eller af mine Fædres Hånd; hvor meget mindre kan da eders Gud frelse eder af min Hånd!"
16 Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia.
Og hans Tjenere talte endnu flere Ord mod Gud HERREN og mod hans Tjener Ezekias.
17 Senakeribu pia akandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, “Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu.”
Han skrev også et Brev for at smæde HERREN, Israels Gud, og tale imod ham; heri stod der: "Så lidt som Landenes Folks Guder har frelst deres Folk af min Hånd, skal Ezekias's Gud frelse sit Folk af min Hånd!"
18 Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji.
Og de råbte med høj Røst på Judæisk til Folkene i Jerusalem, som stod på Muren, for at indjage dem Angst og Skræk, i Håb om at kunne tage Byen.
19 Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu wa Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu.
Og de talte om Jerusalems Gud på samme Måde som om Jordens Folkeslags Guder, der er Værker af Menneskehænder!
20 Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni.
Derfor bad Kong Ezekias og Profeten Esajas, Amoz's Søn, og råbte til Himmelen.
21 Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya muungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.
Og HERREN sendte en Engel, der tilintetgjorde alle Krigere, Høvedsmænd og Hærførere i Assyrerkongens Lejr, så han med Spot og Spe måtte vende hjem til sit Land. Og da han gik ind i sin Guds Hus, fældede nogle af hans kødelige Frænder ham der med Sværdet.
22 Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. (Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande”, baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande”).
Således frelste HERREN Ezekias og Jerusalems Indbyggere af Assyrerkongen Sankeribs Hånd og at alle andres og skaffede dem Ro på alle Kanter.
23 Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea.
Og mange bragte Gaver til Jerusalem til HERREN og kostbare Ting til Kong Ezekias af Juda, så han siden blev højt anset blandt alle Hedningefolk.
24 Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpa ishara kwamba angeponywa.
Ved den Tid blev Ezekias dødssyg. Da bad han til HERREN, og han svarede ham og gav ham et Tegn.
25 Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu.
Men Ezekias gengældte ikke den Velgerning, der var vist ham; hans Hjerte blev hovmodigt, og derfor kom der Vrede over ham og over Juda og Jerusalem.
26 Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa jali ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia.
Men da Ezekias ydmygede sig og vendte om fra sit Hovmod sammen med Jerusalems Indbyggere, kom HERRENs Vrede ikke over dem i Ezekias's Dage.
27 Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia.
Ezekias var overmåde rig og æret. Han byggede sig Skatkamre til Sølv, Guld, Ædelsten, Høgelsestoffer, Skjolde og alle Hånde kostelige Ting
28 Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama.
og Forrådskamre til Afgrøden af Horn, Most og Olie, Stalde til alle Slags Kvæg og Folde til Hjordene;
29 Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alaikuwa amempa afya tele. (Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadji ya matoleo ya kisasa yanasema “punda”, na baadhi mengine ya kisasa yanaacaha neno nzima)
Byer byggede han sig også, og han havde Hjorde i Mængde af Hornkvæg og Småkvæg, thi Gud gav ham såre meget Gods.
30 Alikuwa ni Hezekia huyu huyu ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliye ileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote.
Samme Ezekias tilstoppede Gihons øvre Kilde og ledede Vandet mod Vest nedad til Davidsbyen. Alt, hvad Ezekias tog sig for, lykkedes for ham.
31 Hata hivyo, katika jambo la mabolozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake.
Derfor var det også, at Gud gav ham til Pris for Sendebudene, der var sendt til ham fra Babels Fyrster for at høre om det Under, der var sket i Landet; det var for at sætte ham på Prøve og således få Kendskab til alt, hvad der var i hans Hjerte.
32 Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
Hvad der ellers er at fortælle om Ezekias og hans fromme Gerninger, står jo optegnet i Profeten Esajas's, Amoz's Søns, Åbenbaring og i Bogen om Judas og Israels Konger.
33 Hezekia akalala pamaoja na babu zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.
Så lagde Ezekias sig til Hvile hos sine Fædre, og man jordede ham på Skråningen op til Davids Efterkommeres Grave; og hele Juda og Jerusalems Indbyggere viste ham stor Ære ved hans Død; og hans Søn Manasse blev Konge i hans Sted.