< 2 Nyakati 31 >
1 Sasa wakati haya yote yalipokwisha, watu wote wa Israeli waliokuwepo pale wakaenda huko kwenye mji wa Yuda na wakazivunja vipande vipande nguzo za mawe na wakazikata nchi za maashera, na wakazibomoa sehemu za juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, na katika Efraimu na Manase, hadi walipoziharibu zote. Kisha watu wote wa Israeli wakarudi, kila mtu kwenye mali zake na kwenye mji wake.
这事既都完毕,在那里的以色列众人就到犹大的城邑,打碎柱像,砍断木偶,又在犹大、便雅悯、以法莲、玛拿西遍地将邱坛和祭坛拆毁净尽。于是以色列众人各回各城,各归各地。
2 Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanaga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe.
希西家派定祭司利未人的班次,各按各职献燔祭和平安祭,又在耶和华殿门内事奉,称谢颂赞耶和华。
3 Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na sikukuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.
王又从自己的产业中定出分来为燔祭,就是早晚的燔祭和安息日、月朔,并节期的燔祭,都是按耶和华律法上所载的;
4 Vilevile, akawaamuru watu walioishi Yerusalemu kutoa fungu kwa ajili ya makuhani na Walawi, ili kwamba wawe makini katika kuitii sheria ya Yahwe.
又吩咐住耶路撒冷的百姓将祭司、利未人所应得的分给他们,使他们专心遵守耶和华的律法。
5 Mapema mara baada ya amri kutolewa, watu wa Israeli kwa ukarimu wakatoa malimbuko ya nafaka, divai mpya, mafuta. asali, na kila kitu kutoka kwenye mavuno ya shamba. Wakaleta ndani fungu la kumi la kila kitu; ambavyo vilikuwa kiasi kikubwa sana.
谕旨一出,以色列人就把初熟的五谷、新酒、油、蜜,和田地的出产多多送来,又把各物的十分之一送来的极多。
6 Watu wa Israeli na Yuda ambao waliishi katika mji wa Yuda pia wakaleta zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vitakatifu amabavyo vilikuwa vimewekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wao, na wakavifunga katika marundo.
住犹大各城的以色列人和犹大人也将牛羊的十分之一,并分别为圣归耶和华—他们 神之物,就是十分取一之物,尽都送来,积成堆垒;
7 Ilikuwa mwezi wa tatu wakati walipoanza kufunga michango yao katika marundo, na wakamaliza mwezi wa saba.
从三月积起,到七月才完。
8 Hezekia na viongozi walipokuja na kuyaona marundo, wakambariki Yahwe na watu wake Israeli.
希西家和众首领来,看见堆垒,就称颂耶和华,又为耶和华的民以色列人祝福。
9 Kisha Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu marundo.
希西家向祭司、利未人查问这堆垒。
10 Azaria, kuhani mkuu, wa nyumba ya Zadoki, akamjibu na akasema, “Tangu watu walipoanza kuleta matoleo katika nyumba ya Yahwe, tumekula na tulikuwa navyo vya kutosha, tulibakiza vingi, kwa maana Yahwe amewabariki watu wake. kilichokuwa kimebaki ni kiasi kikubwa hiki hapa.”
撒督家的大祭司亚撒利雅回答说:“自从民将供物送到耶和华殿以来,我们不但吃饱,且剩下的甚多;因为耶和华赐福给他的民,所剩下的才这样丰盛。”
11 Kisha Hezekia akaagiza vyumba vya kuhifadhia viandaliwe katika nyumba ya Yahwe, na wakaviandaa.
希西家吩咐在耶和华殿里预备仓房,他们就预备了。
12 Kisha kwa uaminifu wakayaleta ndani matoleo, zaka, na vitu ambavyo ni vya Yahwe. Konania, Mlawi, alikuwa meneja mkuu wa hivyo vitu, na Shimei, ndu yake, alikuwa wa pili kwake.
他们诚心将供物和十分取一之物,并分别为圣之物,都搬入仓内。利未人歌楠雅掌管这事,他兄弟示每为副管。
13 Yehieli, Azaria, Nahathi, Asaheli, na Yerimothi, Yazabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi, na Benania walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei ndu yake, kwa uteuzi wa Hezekia, mfalme, na Azaria mwanagalizi mkuu wa nyumba ya Mungu.
耶歇、亚撒细雅、拿哈、亚撒黑、耶利末、约撒拔、以列、伊斯玛基雅、玛哈、比拿雅都是督理,在歌楠雅和他兄弟示每的手下,是希西家王和管理 神殿的亚撒利雅所派的。
14 Kore mwana wa Imna Mlawi, bawabu katika mlango wa mashariki, alikuwa juu ya sadaka za hiari za Mungu, msimamizi wa kugawa sadaka kwa Yahwe na sadaka takatifu kuliko zote.
守东门的利未人音拿的儿子可利,掌管乐意献与 神的礼物,发放献与耶和华的供物和至圣的物。
15 Chini yake walikuwepo Edeni, Miniamini, Yoshua, Shemai, Amaaria, na Shekania, katika miji ya makuhani. Wakazijaza ofisi za uaminifu, ili kutoa sadaka hizi kwa ndugu zao fungu kwa fungu, kwa wote walio muhimu na wasiomuhimu.
在他手下有伊甸、珉雅珉、耶书亚、示玛雅、亚玛利雅、示迦尼雅,在祭司的各城里供紧要的职任,无论弟兄大小,都按着班次分给他们。
16 Pia wakatoa kwa wale wanaume wenye umri wa miaka mitatu na kuendelea, amabao walikuwa wameandikwa kataika kaitatu cha babu zao walioiingia nyumba ya Yahwe, kwa mujibu wa ratiba ya kila siku, kuifanya kazi katika ofisi zao na zamu zao. (Mandishi ya kale yanasema hivi: “badala ya wanaume wa umri wa miaka mitatu na kuendelea”, wanaume wa mika thelathini na kuendelea.”).
按家谱,三岁以外的男丁,凡每日进耶和华殿、按班次供职的,也分给他;
17 Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za babu zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamu zao.
又按宗族家谱分给祭司,按班次职任分给二十岁以外的利未人,
18 Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu.
又按家谱计算,分给他们会中的妻子、儿女;因他们身供要职,自洁成圣。
19 Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za babu zao kuwa miongoni mwa Walawi.
按名派定的人要把应得的分给亚伦子孙,住在各城郊野、祭司所有的男丁和一切载入家谱的利未人。
20 Hezekia alifanya haya katika Yuda yote. Akakamilisha kilichokuwa chema, haki, na uaminifu mbele za Yahwe Mungu wake.
希西家在犹大遍地这样办理,行耶和华—他 神眼中看为善为正为忠的事。
21 Katika kila jambo ambalo alianzisha katika ibada ya nyumba ya Mungu, sheria, na zile amri, kumtafuta Mungu, alikifanya kwa moyo wake wote, na alifanikiwa.
凡他所行的,无论是办 神殿的事,是遵律法守诫命,是寻求他的 神,都是尽心去行,无不亨通。