< 2 Nyakati 3 >
1 Kisha Selemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.
Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu la Bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi.
2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.
3 Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Selemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.
Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa ishirini.
4 Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Selemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi.
Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini. Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
5 Akailitengeneza paa la ukumbi mkuu kwa miti ya miberoshi, ambayo aliifunika kwa dhahabu halisi, na ambayo aliifunika kwa miti ya mitende na minyororo.
Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo.
6 Akaipamba nyumba kwa vito vya thamani; dhahabu ilikuwa dhahabu kutoka Parvaimu.
Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu.
7 Pia akazifunika boriti zake, vizingiti, kuta, na milango kwa dhahabu; akachonga makerubi juu ya kuta zake.
Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta.
8 Akaijenga sehemu ya patakatifu pa patakatifu. Urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono ishirini, na upana wake pia ulikuwa mikono ishirini. Aliifunika kwa dhahabu halisi, thamani yake ilikuwa talanta mia sita.
Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 120 za dhahabu safi.
9 Uzito wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alizifunika sehemu za juu kwa dhahabu.
Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.
10 Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu za patakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. (Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao).
Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akafanyiza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu.
11 Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia.
Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano, nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine.
12 Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza.
Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu na bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza.
13 Mabawa ya makerubi hawa yalienea jumla ya mikono mitano. Makerubi yalisimama kwa miguu yake, na nyuso zake zikiuelekea ukumbi mkuu.
Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa.
14 Akatengeneza pazia la samawati, dhambarau, na sufu nyekundu, na kitani safi, na akachora makerubi juu yake.
Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake.
15 Selemani pia akatengeneza nguzo mbili, kila moja ikiwa na urefu wa mikono thelathini na tano kwenda juu, kwa maana mbele ya nyumba; taji ambazo zilikuwa juu ya nguzo zilikuwa na urefu wa mikono mitano kwenda juu.
Mbele ya Hekalu Solomoni akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake, na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano.
16 Akatengeneza minyororo kwa ajili ya nguzo na akaiweka juu yake, pia akatengeneza maakomamanga mia moja na akayaunganisha kwenye minyororo.
Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga 100, na kuyashikamanisha kwenye minyororo.
17 Akazisimamisha nguzo mbele ya hekalu, mkono wa kulia, na nyingine mkono wa kushoto; akaiita nguzo ya kulia Yakini, na nguzo ya kushoto akaiita Boazi.
Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.