< 2 Nyakati 27 >
1 Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.
Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki.
2 Akafanya yaliyomema katika macho ya Yawe, akiufuta mfano wa baba yake, Uzia, katika mabo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.
Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Uzia baba yake alivyokuwa amefanya, lakini tofauti na yeye, hakuingilia huduma za hekaluni mwa Bwana. Lakini hata hivyo, watu wakaendelea na desturi zao mbaya.
3 Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.
Yothamu akajenga upya Lango la Juu la Hekalu la Bwana na kufanya kazi kubwa kwenye ukuta katika kilima cha Ofeli.
4 Vilevile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika mistu alijenga ngome na minara.
Akajenga miji katika vilima vya Yuda pamoja na ngome na minara mwituni.
5 Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
Yothamu akafanya vita na mfalme wa Waamoni na kumshinda. Mwaka ule Waamoni wakamlipa talanta 100 za fedha, kori 10,000 za ngano na kori 10,000 za shayiri. Waamoni wakamletea kiasi hicho hicho mwaka wa pili na wa tatu.
6 Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.
Yothamu akaendelea kuwa na nguvu kwa sababu alienenda kwa ukamilifu mbele za Bwana Mungu wake.
7 Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
Matukio mengine ya utawala wa Yothamu, pamoja na vita vyake vyote na vitu vingine alivyofanya, vimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita kataika Yerusalemu.
Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na sita.
9 Yothamu akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
Yothamu akalala na baba zake na akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akawa mfalme baada yake.