< 2 Nyakati 26 >
1 Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na aumri wa mika kumi na sita, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake Amazia.
유다 온 백성이 웃시야로 그 부친 아마샤를 대신하여 왕을 삼으니 때에 나이 십륙세라
2 Ndiye aliuyeijenga tena Elathi na kuurejesha kwa Yuda. Baada ya hapo mfalme akalala pamoja na babu zake.
왕이 그 열조와 함께 잔 후에 웃시야가 엘롯을 건축하여 유다에 돌렸더라
3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala. Akatawala miaka ishirini na mabili katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yekolia; alikuwa wa Yerusalemu.
웃시야가 위에 나아갈 때에 나이 십륙세라 예루살렘에서 오십 이년을 치리하니라 그 모친의 이름은 여골리아라 예루살렘 사람이더라
4 Akafanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, katika kila jamabo.
웃시야가 그 부친 아마샤의 모든 행위대로 여호와 보시기에 정직히 행하며
5 Alijitoa kumtafuta Mungu katiaka siku za Zekaria, ambaye alimpa maelekezo kwa ajili ya kumtii Mungu. Kadri alivyomtafuta Yaahwe, Mungu alimfanikisha.
하나님의 묵시를 밝히 아는 스가랴의 사는 날에 하나님을 구하였고 저가 여호와를 구할 동안에는 하나님이 형통케 하셨더라
6 Uzia akaenda na kupigana zidi ya Wafilisti. Akaubomoa ukuta wa mji wa Gathi, Yabne, na Ashdodi; akajenga miji katika nchi ya Ashdodi na miongoni mwa Wafilisti.
웃시야가 나가서 블레셋 사람과 싸우고 가드성과 야브네성과 아스돗성을 헐고 아스돗 땅과 블레셋 사람 가운데 성읍들을 건축하매
7 Mungu aakaamsaidia zidi ya Wafilist, zidi ya Waarabu waliokuwa wakiishi Gur - baali, na zidi ya Wameuni.
하나님이 도우사 블레셋 사람과 구르바알에 거한 아라비아 사람과 마온 사람을 치게 하신지라
8 Waamoni wakalipa kodi kwa Uzia, na umaarufu wake ukaenea, hata kufika maingilio ya Misiri, kwa sababu alikuwa ameanza kuwa maarufu.
암몬 사람이 웃시야에게 조공을 바치매 웃시야가 심히 강성하여 이름이 애굽 변방까지 퍼졌더라
9 Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na pa kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome.
웃시야가 예루살렘에서 성 모퉁이 문과 골짜기 문과 성굽이에 망대를 세워 견고하게 하고
10 Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
또 거친 땅에 망대를 세우고 물웅덩이를 많이 팠으니 평야와 평지에 육축을 많이 기름이며 또 여러 산과 좋은 밭에 농부와 포도원을 다스리는 자를 두었으니 농사를 좋아함이더라
11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi la wanaume wa kupigana vita ambao walienda vitani katika makundi ambayo idadi yake ilikuwa imehesabiwa na Yeieli, mwandishi. na Maaseya, afisa, chini ya mamlaka ya Hanania, mmoja wa maamri jeshi wa mfalme.
웃시야에게 또 싸우는 군사가 있으니 서기관 여이엘과 영장 마아세야의 조사한 수효대로 왕의 장관 하나냐의 수하에 속하여 떼를 지어 나가서 싸우는 자라
12 Jumla ya wakuu wa nyumba za mababu, watu wa kupigana vita, walikuwa 2, 600.
족장의 총수가 이천 육백명이니 모두 큰 용사요
13 Chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la watu 307, 500 ambao walifanya vita kwa nguvu ili kumsaidia mfalme idi ya maadui.
그 수하의 군대가 삼십만 칠천 오백명이라 건장하고 싸움에 능하여 왕을 도와 대적을 치는 자며
14 Uzia akaandaa kwa ajili yao—kwa ajili ya jeshi lote — ngao, mikuki, chapeo, deraya za majini, nyuta, na mawe ya kurusha.
웃시야가 그 온 군대를 위하여 방패와 창과 투구와 갑옷과 활과 물매 돌을 예비하고
15 Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makaubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na ngavu sana.
또 예루살렘에서 공교한 공장으로 기계를 창작하여 망대와 성곽 위에 두어 살과 큰 돌을 발하게 하였으니 그 이름이 원방에 퍼짐은 기이한 도우심을 얻어 강성하여짐이더라
16 Lakini Uzia alipokuwa amekuwa na nguvu nyingi, moyo wake ulijiinua akatenda kwa uovu; akafanya makosa zidi ya Yahwe, Mungu wake, kwa maana alienda kwenye nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
저가 강성하여지매 그 마음이 교만하여 악을 행하여 그 하나님 여호와께 범죄하되 곧 여호와의 전에 들어가서 향단에 분향하려 한지라
17 Azaria, kuhani, akamfuata, na pamoja naye makuhanai themanini wa Yahwe, ambao walikuwa watu wenye ujasiri.
제사장 아사랴가 여호와의 제사장 용맹한 자 팔십인을 데리고 그 뒤를 따라 들어가서
18 Walimzuia Uzia, mfalme, na wakasema kwake, “Siyo jukumu lako, Uzia, kumtolea Yahwe uvumba, bali ni kazi ya makuhani, wana wa Haruni, amabao wametengwa kwa ajili ya kutoa sadaka za uvumba. Toka nje ya sehemu takatifu, kwa maana huna uaminifu na hautaheshimiwa na Yahwe Mungu.”
웃시야왕을 막아 가로되 웃시야여 여호와께 분향하는 일이 왕의 할바가 아니요 오직 분향하기 위하여 구별함을 받은 아론의 자손 제사장의 할바니 성소에서 나가소서 왕이 범죄하였으니 하나님 여호와께 영광을 얻지 못하리이다
19 Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.
웃시야가 손으로 향로를 잡고 분향하려 하다가 노를 발하니 저가 제사장에게 노할 때에 여호와의 전 안 향단 곁 제사장 앞에서 그 이마에 문둥병이 발한지라
20 Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwanagalia, na, tazama, alikuwa amepatwa ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.
대제사장 아사랴와 모든 제사장이 왕의 이마에 문둥병이 발하였음을 보고 전에서 급히 쫓아내고 여호와께서 치시므로 왕도 속히 나가니라
21 Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maan alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa anyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.
웃시야왕이 죽는 날까지 문둥이가 되었고 문둥이가 되매 여호와의 전에서 끊어졌고 별궁에 홀로 거하였으므로 그 아들 요담이 왕궁을 관리하며 국민을 치리하였더라
22 Mambo mengine kuhusu Uzia, mwanzo na mwisho, yako katika kile ambacho Isaya, mwana wa Amozi, nabii, aliandika.
이 외에 웃시야의 시종 행적은 아모스의 아들 선지자 이사야가 기록하였더라
23 Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na babu zake; walimzka pamoja na babu zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma”. Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
웃시야가 그 열조와 함께 자매 저는 문둥이라 하여 열왕의 묘실에 접한 땅 곧 그 열조의 곁에 장사하니라 그 아들 요담이 대신하여 왕이 되니라