< 2 Nyakati 24 >

1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala kwa mika arobaini katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
Joasz [miał] siedem lat, kiedy zaczął królować, i królował czterdzieści lat w Jerozolimie. Jego matka miała na imię Sibia, [była] z Beer-Szeby.
2 Yoashi alifanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe siku zote za Yehoyada, yule kuhani.
I Joasz czynił [to, co] dobre w oczach PANA, przez wszystkie dni kapłana Jehojady.
3 Yehoyada akajichukulia wake wawili kwa ajili yake, na akawa baba wa wana na mabinti.
A Jehojada dał mu dwie żony; i spłodził synów i córki.
4 Ikawa baada ya haya, kwamba Yoashi aliamua kuitengeneza nyumba ya Yahwe.
Potem w sercu Joasza powstał zamiar, aby odnowić dom PANA.
5 Akawakusanya pamoja makuhani na Walawi, na kusema kwao, “Nendeni nje kila mwaka kwenye miji ya Yuda na kukusanya fedha kutoka Israeli yote kwa ajili ya kuikarabati nyumba ya Mungu wenu. Hakikisheni kwamba mnaanza haraka.” Walawi hawakufanya kitu kwanza.
Zebrał więc kapłanów i Lewitów i powiedział do nich: Wyjdźcie do miast Judy i zbierajcie od całego Izraela pieniądze na coroczną naprawę domu waszego Boga. Pospieszcie się z tym. Lewici jednak nie spieszyli się.
6 Kwa hiyo mfalme akamuita Yehoyada, yule kuhani, na kumwambia, “Kwa nini hukuwaagiza Walawi kuleta kutoka Yud na Yerusalemu kodo iliyoagizwa na Musa mtumishi wa Yahwe na kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya amri za hema ya agano?”
Wówczas król wezwał najwyższego [kapłana] Jehojadę i zapytał go: Czemu nie pilnujesz Lewitów, aby przynosili z Judy i Jerozolimy ofiarę na Namiot Świadectwa [ustanowioną] przez Mojżesza, sługę PANA, i zgromadzenie Izraela?
7 Kwa maana wana wa Athalia, yule mwanamke muovu, walikuwa wameivunja nyumba ya Mungu na kuwapa Mabaali vitu vyote vitakatifu vya nyumba ya Yahwe.
Bezbożna Atalia i jej synowie złupili bowiem dom Boży, a wszystkie rzeczy poświęcone z domu PANA oddali Baalom.
8 Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe.
Król więc rozkazał, aby wykonano skrzynię i umieszczono ją przed bramą domu PANA.
9 Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani.
I ogłoszono w Judzie i Jerozolimie, aby przynoszono PANU ofiarę [nałożoną] na Izraela [przez] Mojżesza, sługę Bożego, na pustyni.
10 Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza.
I radowali się wszyscy książęta oraz cały lud. Przynosili [ją] i rzucali do tej skrzyni, aż ją napełnili.
11 Ikatokea kwamba kila lilipoletwa kasha kwa mikono ya Walawi kwa wakuu wa mfalme, na kila walipoona kwamba kulikuwa na fedha nyingi sana ndani yake, waandishi wa mfalme na mkuu wa kuhani mkuu walikuja, kulihamishia fedha kasha, na kulirudisha sehemu yake. Walifanya hivyo siku baada siku, wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha.
A kiedy Lewici przynosili skrzynię do urzędu królewskiego i gdy widzieli, że [było] już wiele pieniędzy, przychodził pisarz królewski oraz pełnomocnik najwyższego kapłana i wypróżniali skrzynię, a potem ją odnosili z powrotem na swoje miejsce. Tak czynili codziennie i zebrali bardzo dużo pieniędzy.
12 Mfalme na Yehoyada akawapa zile fedha wale waliofanya kazi ya kuhudumu katika nyumba ya Yahwe, Watu hawa waliwaajiri waashi na maseremala ili waijenge nyumba ya Yahwe, na pia wale waliofanya kazi katika chuma na shaba.
Król i Jehojada dawali je kierownikom robót domu PANA, a ci najmowali kamieniarzy i cieśli do naprawy domu PANA, a także kowali i brązowników – do umocnienia domu PANA.
13 Kwa hiyo wafanya kazi wakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; waakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha.
Tak więc robotnicy pracowali i dzięki nim dzieło zostało wykonane. Doprowadzili dom Boży do właściwego stanu i umocnili go.
14 Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukomaa katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada.
A gdy skończyli, przynieśli przed króla i Jehojadę resztę pieniędzy, za które sporządzono naczynia do domu PANA: naczynia do służby i składania ofiar, czasze oraz [inne] naczynia złote i srebrne. I nieustannie składali całopalenia w domu PANA przez wszystkie dni Jehojady.
15 Yehoyada akazeeka na alaaikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.
Potem Jehojada zestarzał się i umarł, będąc syty dni. Miał sto trzydzieści lat, gdy umarł.
16 Wakamzika katika aamji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu,
I pogrzebano go w mieście Dawida razem z królami, dlatego że czynił dobrze w Izraelu: i względem Boga, i względem jego domu.
17 Sasa baada ya kifo cha Yehoyada, kiongozi wa Yuda akaja na kutoa heshima kwa mfalme. Kisha mfalme akawasikiliza.
Po śmierci Jehojady przyszli książęta Judy i pokłonili się królowi. Wtedy król ich usłuchał.
18 Wakaiacha nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zao, na kuwaabudu miungu na maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababau ya hili kosa lao.
Opuścili dom PANA, Boga swoich ojców, i służyli gajom oraz posągom. Spadł więc gniew na Judę i Jerozolimę z powodu tego występku.
19 Bado akatuma manabii kwao ili kuwaleta tena kwake, Yahwe, manabii wakatangaza juu ya watu, lakini walipuuza kusikiliza.
I posyłał do nich proroków, żeby ich nawrócić do PANA. A [choć] świadczyli przeciwko nim, nie usłuchali ich.
20 Roho wa Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada, yule kuhani; Zekaria akasimama juu ya watu na kusema kwao, “Mungu anasema hivi: Kwa nini mnazivunja amri za Yahwe, ili kwamba msifanikiwe? Kwa kuwa mmemsahau Yahwe, pia amewasahau ninyi.”
Wówczas Duch Boży zstąpił na Zachariasza, syna kapłana Jehojady, który stanął przed ludem i powiedział im: Tak mówi Bóg: Czemu przekraczacie przykazania PANA? Nie powodzi się wam. Skoro wy opuściliście PANA, [on] też was opuścił.
21 Lakini wakapanga njama dhidi yake; kwa amri ya mfalme, wakampiga kwa mawe katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
Wtedy sprzysięgli się przeciwko niemu i ukamienowali go na rozkaz króla na dziedzińcu domu PANA.
22 Katika namna hii hii, Yoashi, yule mfalme, akapuuza ukarimu ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alikuwa amemfanyia.
I nie pamiętał król Joasz o dobrodziejstwie, jakie wyświadczył mu jego ojciec Jehojada, ale zabił jego syna. Kiedy ten umierał, powiedział: Niech PAN [to] zobaczy i zemści się.
23 Ikawa karibu mwisho wa mwaka, kwamba jeshi la Aramu wakaja juu yake Yoashi. Wakaja Yuda na Yerusalemu; wakawaua viongozi wote wa watu na kupeleka nyara zote kutoka kwao kwa mfalme wa Dameski.
A po upływie roku przeciwko niemu nadciągnęło wojsko Syrii. Przybyło do Judy i Jerozolimy i wyniszczyło z ludu wszystkich książąt, a wszystkie jego łupy posłano królowi Damaszku.
24 Jeshsi la Waaramu walikuwa wamekuja na jeshi dogo, lakini Yahwe akawapa ushindi juu ya jeshi kubwa, kwa sababu Yuda alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. Katika namna hii Waaramu wakaleta hukumu juu ya Yoashi.
Przybyło bowiem wojsko Syrii z niewielką liczbą ludzi, a PAN wydał w ich ręce bardzo liczne wojsko, dlatego że opuścili PANA, Boga swoich ojców. I tak dokonano sądu nad Joaszem.
25 Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme.
A gdy się od niego oddalili, zostawiając go w ciężkiej chorobie, jego słudzy sprzysięgli się przeciwko niemu, z powodu krwi synów kapłana Jehojady, i zabili go na jego łożu. [Tak więc] umarł i pogrzebano go w mieście Dawida, ale nie w grobach królewskich.
26 Hawa walikuwa watu waliopanaga njama dhidi yake: Zabadi mwana wa Shimeathi, Mwamoni; na Yehozabadi mwana wa Shimrithi, Mwanamke Mmoabu.
A oto są ci, którzy sprzysięgli się przeciw niemu: Zabad, syn Szimeata, Ammonitki, i Jehozabad, syn Szimrit, Moabitki.
27 Sasa matukio kuhusu wanaye, unabii muhimu uliokuwa umesemwa kumhusu yeye, na kujengwa tena kwa nyumba ya Mungu, ona, yameandikwa katika Kamusi ya kitabu cha wafalme. Amazia mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
O jego synach zaś, o wielkim ciężarze nałożonym na niego i o naprawie domu Bożego, jest zapisane w księdze królewskiej. I królował jego syn Amazjasz w jego miejsce.

< 2 Nyakati 24 >