< 2 Nyakati 23 >
1 Katika mwaka wa sa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
第七年にいたりヱホヤダ力を強してヱロハムの子アザリヤ、ヨハナンの子イシマエル、オベデの子アザリア、アダヤの子マアセヤ、ジクリの子エシヤパテなどいふ百人の長等を招きて己と契約を結ばしむ
2 Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.
是において彼らユダを行めぐりてユダの一切の邑よりレビ人を集めまたイスラエルの族長を集めてヱルサレムに歸り
3 Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, “Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.
而してその會衆みな神の家において王と契約を結べり時にヱホヤダかれらに言けるけるはダビデの子孫の事につきてヱホバの宣まひしごとく王の子位に即べきなり
4 Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.
然ば汝ら斯なすべし汝ら祭司およびレビ人の安息日に入きたる者は三分の一は門を守り
5 Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
三分の一は王の家に居り三分の一は基礎の門に居り民はみなヱホバの室の庭に居べし
6 Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaoatumika. Wao wanaweza kuingia kwa sababu inawahusu.
祭司と奉事をするレビ人の外は何人もヱホバの家に入べからず彼らは聖者なれば入ことを得るなり民はみなヱホバの殿を守るべし
7 Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje.”
レビ人はおのおの手に武器を執て王を繞りて立べし家に入る者をば凡て殺すべし汝らは王の出る時にも入る時にも王とともに居れと
8 Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana
是においてレビ人およびユダの人衆は祭司ヱホヤダが凡て命じたる如くに行ひ各々その手の人の安息日に入來べき者と安息日に出ゆくべき者とを率ゐ居れり祭司ヱホヤダ班列の者を去せざればなり
9 Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.
祭司ヱホヤダすなはち神の家にあるダビデ王の鎗および大楯小楯を百人の長等に交し
10 Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.
一切の民をして各々武器を手に執て王の四周に立ち殿の右の端より殿の左の端におよびて壇と殿にそふて居しむ
11 Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, “Aishi maisha marefu mfalme.”
斯て人衆王の子を携へ出し之に冠冕を戴かせ證詞をわたして王となし祭司ヱホヤダおよびその子等これに膏をそそげり而して皆王長壽かれと言ふ
12 Athalia aliposikia kele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.
茲にアタリヤ民と近衛兵と王を讃る者との聲を聞きヱホバの室に入て民の所に至り
13 na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!”
視に王は入口にてその柱の傍に立ち王の側に軍長と喇叭手立をり亦國の民みな喜びて喇叭を吹き謳歌者樂を奏し先だちて讃美を歌ひをりしかばアタリヤその衣を裂き叛逆なり叛逆なりと言り
14 Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, “Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga.” kwa maana kuhani alikwishasema, “Msimuue katika nyumba ya Yahwe.”
時に祭司ヱホヤダ軍兵を統る百人の長等を呼出してこれに言ふ彼をして列の間を通りて出しめよ凡て彼に從がふ者をば劍をもて殺すべしと祭司は彼をヱホバの室に殺すべからずとて斯いへるなり
15 Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.
是をもて之がために路をひらき王の家の馬の門の入口まで往しめて其處にて之を殺せり
16 kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.
斯てヱホヤダ己と一切の民と王との間にわれらは皆ヱホバの民とならんことの契約を結べり
17 Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.
是において民みなバアルの室にゆきて之を毀ちその壇とその像を打碎きバアルの祭司マツタンを壇の前に殺せり
18 Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.
ヱホヤダまたヱホバの室の職事を祭司レビ人の手に委ぬ昔ダビデ、レビ人を班列にわかちてヱホバの室におきモーセの律法に記されたる所にしたがひて歓喜と謳歌とをもてヱホバの燔祭を献げしめたりき今このダビデの例に傚ふ
19 Yehoyada akaweka walinzi katika malango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.
彼またヱホバの室の門々に看守者を立せ置き身の汚れたる者には何によりて汚れたるにもあれ凡て入ことを得ざらしむ
20 Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme. (Baadhi ya maandiko ya ya kisasa yanasema, “wakamshusha chini mfalme”)
斯てヱホヤダ百人の長等と貴族と民の牧伯等および國の一切の民を率ゐてヱホバの家より王を導きくだり上の門よりして王の家にいり王を國の位に坐せしめたり
21 Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.
斯りしかば國の民みな喜こびて邑は平穩なりきアタリヤは劍にて殺さる