< 2 Nyakati 21 >

1 Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na akizikwa pamoaja nao katika mji wa Daudi;
Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.
2 Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli.
Ndugu zake Yehoramu, wana wa Yehoshafati walikuwa: Azaria, Yehieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli na Shefatia. Hawa wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli
3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.
Baba yao alikuwa amewapa zawadi nyingi za fedha na dhahabu na vitu vya thamani, pamoja na miji yenye ngome huko Yuda, bali ufalme akampa Yehoramu kwa sababu alikuwa mwanawe mzaliwa wa kwanza.
4 Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongizi wengine mbali mbali wa Israeli.
Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli.
5 Yehoramu alikuwa na umri wa mika thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.
Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane.
6 Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.
Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Bwana.
7 Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.
Hata hivyo, kwa sababu ya Agano ambalo Bwana alikuwa amefanya na Daudi, Bwana hakuwa radhi kuangamiza nyumba ya Daudi. Mungu alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili yake na wazao wake milele.
8 Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.
Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe.
9 Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.
Basi Yehoramu akaenda huko pamoja na maafisa wake na magari yake ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu.
10 Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna pia aliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zake.
Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo kwa sababu Yehoramu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake.
11 Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milma ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu.
Alikuwa pia ametengeneza mahali pa juu pa kuabudia miungu katika vilima vya Yuda na akawa amewasababisha watu wa Yerusalemu kufanya uzinzi na akawa amewapotosha watu wa Yuda.
12 Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,
Yehoramu akapokea barua kutoka kwa nabii Eliya iliyosema: “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Daudi baba yako, asemalo: ‘Hukuenenda katika njia za Yehoshafati baba yako au za Asa mfalme wa Yuda.
13 bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe—
Lakini umeenenda katika njia za wafalme wa Israeli, nawe umewaongoza Yuda na watu wa Yerusalemu kuzini, kama vile nyumba ya Ahabu ilivyofanya. Pia umewaua ndugu zako mwenyewe, watu wa nyumbani mwa baba yako, watu waliokuwa bora kuliko wewe.
14 ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote.
Hivyo basi Bwana yu karibu kuwapiga watu wako, wanao, wake zako na kila kitu kilicho chako, kwa pigo zito.
15 Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa kataika katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku.
Wewe mwenyewe utaugua sana kwa ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu, hadi ugonjwa utakaposababisha matumbo yako kutoka nje.’”
16 Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethipia.
Bwana akaamsha chuki ya Wafilisti na ya Waarabu walioishi karibu na Wakushi dhidi ya Yehoramu.
17 Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo.
Wakaishambulia Yuda, wakaivamia na kuchukua mali zote zilizopatikana katika jumba la mfalme pamoja na wanawe na wake zake. Hakubakiziwa mwana yeyote isipokuwa Ahazia aliyekuwa mdogo wa wote.
18 Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona.
Baada ya mambo haya yote, Bwana akampiga Yehoramu kwa ugonjwa usioponyeka wa matumbo.
19 Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia babu zake.
Ikawa baada ya muda, mwisho wa mwaka wa pili, matumbo yake yakatoka nje kwa sababu ya ugonjwa, naye akafa katika maumivu makali sana. Watu wake hawakuwasha moto kwa heshima yake, kama walivyokuwa wamewafanyia baba zake.
20 Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umrai wa miaka thelatahini na mbaili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuaombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.
Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipokuwa mfalme, naye akatawala huko Yerusalemu miaka minane. Akafa, bila kusikitikiwa na mtu yeyote, naye akazikwa katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

< 2 Nyakati 21 >