< 2 Nyakati 20 >

1 Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. (Mandishi, “baadhi ya Wameuni” yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, “baadhi ya Waamoni”. Inadhaniwa kwamba “Wameuni” ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa “baadhi ya Waamoni”. Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstri huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mabli mbali)
Ikawa baada ya jambo hili, Wamoabu na Waamoni, pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja ili wapigane vita na Yehoshafati.
2 Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, “Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari”, ambayo ndiyo En-gedi. (Badala ya “Edomu” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, “Aramu.”
Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Edomu tokea ngʼambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).
3 Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
Yehoshafati akaogopa, akaazimu kumtafuta Bwana, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga.
4 Yuda wakakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.
Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Bwana. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta.
5 Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.
Kisha Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu la Bwana, mbele ya ua mpya,
6 Akasema, “Yahwe, Mungu wa babau zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falame zote za mataiafa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyao hakuna anayeweza akukupinga wewe.
akasema: “Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe ndiwe uliye Mungu mbinguni? Si wewe ndiwe utawalaye juu ya falme zote za mataifa? Uweza na nguvu viko mkononi mwako, wala hakuna yeyote awezaye kushindana nawe.
7 Munagu wetu, Hukuwafuaakuja nje wakaaji wa nchi hii mbe ya watau watau wakop Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzaoa wa Abrahamu?
Je, si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Abrahamu, rafiki yako, hata milele?
8 Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,
Wameishi ndani yake na humo wamekujengea mahali patakatifu kwa ajili ya Jina lako, wakisema:
9 'Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa.' (Badala ya “hukumu” baadhi ya maandiko ya zamani yanasema “mafuriko”).
‘Kama maafa yakitujia, ikiwa ni upanga, hukumu, tauni, au njaa, tutasimama mbele zako, mbele ya Hekalu hili ambalo limeitwa kwa Jina lako na kukulilia katika shida yetu, nawe utatusikia na kutuokoa.’
10 Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige waalipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.
“Lakini sasa hawa watu wa kutoka Amoni, Moabu na Mlima Seiri, ambao hukuwaruhusu Israeli wazivamie nchi zao wakati walitoka Misri, hivyo wakageukia mbali nao na hawakuwaangamiza,
11 Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kutotoa nje ya nchi yako mbayo umetupa kuirithi.
tazama jinsi wanavyotulipa kwa kuja kututupa nje ya milki uliyotupa sisi kuwa urithi.
12 Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.
Ee Mungu wetu, je, wewe hutawahukumu? Kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa linalokuja kutushambulia. Sisi hatujui la kufanya, bali macho yetu yanakutazama wewe.”
13 Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.
Watu wote wa Yuda pamoja na wake zao, watoto wao na wadogo wao wakasimama pale mbele za Bwana.
14 Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.
Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya mtu mmoja jina lake Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, Mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi mzao wa Asafu alipokuwa amesimama katika kusanyiko.
15 Yahazieli akasema, “Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, 'Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshsi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.
Akasema: “Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mkaao Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndilo Bwana asemalo kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu.
16 Lazima muende chini juu ya yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupia njia ya Sisi. Mtawakuta mwishono mwa bondo, mbele ya jangwa la Yerueli.
Kesho shukeni kukabiliana nao. Watakwea kwa kupandia Genge la Sisi, nanyi mtawakuta mwisho wa bonde, kabla ya Jangwa la Yerueli.
17 Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi.”
Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Bwana atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Bwana atakuwa pamoja nanyi.’”
18 Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamaoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.
Yehoshafati akainamisha uso wake chini, nao watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakaanguka chini ili kuabudu mbele za Bwana.
19 Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.
Ndipo baadhi ya Walawi kutoka kwa Wakohathi na kwa wana wa Kora wakasimama na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.
20 Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, “Nisikilizeni, Yuda, na nnyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.
Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Bwana Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.
21 Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagaua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, “Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa aganao lake unadumu milele.”
Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Bwana na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni Bwana kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”
22 Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakauja dhidi ya Yuda. Walishindwa.
Walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa.
23 Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.
Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakaangamizana wao kwa wao.
24 Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.
Yuda walipofika katika mnara wa ulinzi wa jangwani, wakaliangalia lile jeshi kubwa, wakaona ni maiti tupu zimetapakaa ardhini, wala hakuna yeyote aliyenusurika.
25 Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. (Badala ya “miongoni mwao”, baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa”).
Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, nguo na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.
26 Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, Huko wakamsifu Yaahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni “Bonde la Baraka”.
Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka kwa maana huko ndiko walikomsifu Bwana. Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka mpaka leo.
27 Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.
Kisha watu wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kwa kuwa Bwana alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.
28 Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi na matarumbeta.
Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwa Bwana wakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta.
29 Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.
Hofu ya Mungu ikazipata falme zote za nchi waliposikia jinsi Bwana alivyokuwa amepigana dhidi ya adui za Israeli.
30 Kwa hiyo ufaleme wa Yehoshafati ulikuwa mtivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzungunga pande zake zote.
Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amemstarehesha pande zote.
31 Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yke aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.
Hivyo Yehoshafati akatawala Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi.
32 Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macaho ya Yahwe.
Alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakwenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana.
33 Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.
Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, na watu wakawa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa baba zao.
34 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.
Matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Yehu mwana wa Hanani, ambazo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.
35 Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.
Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya urafiki na Ahazia mfalme wa Israeli ambaye alifanya maovu sana.
36 Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.
Akaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi, nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi.
37 Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.
Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, Bwana ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kungʼoa nanga ili kwenda Tarshishi.

< 2 Nyakati 20 >