< 2 Nyakati 19 >
1 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi salama nyumbani kwake Yerusalemu.
2 Kisha Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kukutana naye na akasema kwa mfalme Yehoshafati, “Unapaswa kuwa unawasaidia waovu? Unapaswa kuwapenda wanaomchukia Yahwe? Kwa ajili ya tendo hili, ghadhabu toka kwa Yahwe iko juu yako.
3 Aidha, kuna baadhi ya mema ya kuonekana ndani yako, kwamba umeziondosha Maashera nje ya nchi, na umeukaza moyo wako kumtafuta Mungu.”
4 Yehoshafati akaishi katika Yerusalemu; na akaenda nje tena miongoni mwa watu wa Beer- sheba hadi nchi ya kilima ya Efraimu na akawarudisha kwa Yahwe, Mungu wa baba zao.
5 Akaweka waamuzi katika nchi katika miji yote ya Yuda yenye angome, mji kwa mji.
6 Akawaambia waamuzi, “Zingatieni mnachopaswa kufanya, kwa sababu hamuamui kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Yahwe; yuko pamoja nanyi katika kazi ya kuamua,
7 Basi sas iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangaliafu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo.”
8 Vile vile, katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na baahdhi ya viongozi wa nyumba za mababu wa Israeli, kwa ajili ya kufanya hukumu kwa ajili ya Yahwe, na kwa ajili ya migogoro. Wakaishi katika Yerusalemu.
9 Akawaelekeza, akisema, “Lazima mtumike kwa heshima kwa ajaili ya Yahwe, kwa uaminifu, na na kwa moyo wenu wote.
10 Kila mgogoro wowote utakapokuja kwenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji yao, iwe inahusu mauji, iwe inhusu torati na amri, lazim muwaonye, ili kwamba wasiwe na hatia mbele za Yahwe, la sivyo ghadhabu itakuja juu yenu na juu ya ndugu zenu. Mnapaswa kufanya hivyo na hamtakuwa na hatia
11 Ona, Amaria kuhani mkuu yuko juu yenu katika mambo yote ya Yahwe. Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa nyumba ya Yuda, ni kiongozi katika yote katika mambo yote ya mfalme. Pia, Walawi watakuwa wasimamizi wakiwatumikia ninyi. Muwe hodari na tiini maelekezo yenu, na Yahwe awe moja nao walio wema.”