< 2 Nyakati 16 >
1 Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, akatenda kwa ukatili dhidi ya Yuda na akaujenga Rama, ili kwamba asimruhusu mtu yeyote kutoka wala kuingia katika nchi ya Asa, mfalme wa Yuda.
Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Mfalme Baasha wa Israeli akashambulia Yuda na kuweka ngome mji wa Rama ili kumzuia yeyote asitoke wala kuingia nchi ya Mfalme Asa wa Yuda.
2 Kisha Asa akaitoa fedha na dhahabu nje ya vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Yahwe na nje ya nyumba ya mfalme, na akaituma kwa Ben Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye aliishi Dameski. Akasema, pawe na agano kati yako na mimi, kama palivyokuwa na agano kati ya baba yangu na baba yako. Angalia, nimekutumia fedha na dhahabu.
Ndipo Asa akachukua fedha na dhahabu kutoka hazina ya Hekalu la Bwana na kutoka jumba lake mwenyewe la kifalme na kumpelekea Ben-Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye alikuwa anatawala huko Dameski.
3 Livunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”
Akasema, “Pawepo na mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekuletea fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniondokee mimi.”
4 Ben Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma maakida wa majeshsi dhidi ya miji ya Israeli. Wakavamia Iyoni, Dani, Abelimaimu, na miji yoye ya kuhifadhia ya Naftali.
Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na kutuma majemadari wa majeshi yake dhidi ya miji ya Israeli. Wakashinda Iyoni, Dani, Abel-Maimu na miji yote ya hazina ya Naftali.
5 Ikawa kwamba Baasha aliposikia hili, akaacha kuujenga Rama, na akaistisha kazi yake.
Baasha aliposikia jambo hili, akasimamisha kujenga Rama na kuacha kazi yake.
6 Kisha Asa mfalme akawachukua Yuda wote pamoja naye. Wakayabeba mawe na mbao za Rama ambazo Baasha alikuwa anajengea ule mji. Kisha Mfalme Asa alitumia vifaa hivyo vya ujenzi kwa ajili ya kuijenga Gaba na Mispa.
Ndipo Mfalme Asa akawaleta watu wote wa Yuda, nao wakachukua mawe na miti ambayo Baasha alikuwa anavitumia huko Rama. Kwa vitu hivyo akajenga Geba na Mispa.
7 Wakati huo Hanani mwonaji akaenda kwa Asa, mfalme wa Yuda, na akamwambia, “Kwa sababu umemtegemea mfalme wa Aramu, na hukumtegemea Yahwe Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limetoroka nje ya mikono yako.
Ikawa wakati huo mwonaji Hanani akamjia Mfalme Asa wa Yuda na kumwambia: “Kwa sababu ulimtegemea mfalme wa Aramu nawe hukumtegemea Bwana Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limeponyoka mkononi mwako.
8 Waethiopia na Walubi hawakuwa jesi kubwa, wenye magari mengi na wapanda farasi wengi? Na bado, kwa sababau ulimtegemea Yahwe, alikupa ushindi juu yao.
Je, hukumbuki lililotendeka kwa Wakushi na Walibia, hawakuwa jeshi lenye nguvu na magari mengi ya vita na wapanda farasi? Hata hivyo, ulipomtegemea Bwana yeye aliwatia mkononi mwako.
9 Kwa maana macho ya Yahwe hukimbia kila mahali katika dunia yote, ili kwamba ajioneshe mwenyewe shujaa kwa niaba ya wale amabao mioyo yao ni mikamilifu kumwelekea yeye. Lakini umetenda kipumbavu katika jambo hili. Kwa maana tangu sasa na kuendelea, utakuwa na vita.” Kisha Asa akamkasirikia mwonaji, akamuweka gerezani, kwa maana alikuwa na hasira naye juu ya jambao
Kwa kuwa macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu. Umefanya jambo la upumbavu na kuanzia sasa na kuendelea utakuwa na vita.”
10 hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu
Asa akamkasirikia mwonaji kwa sababu ya jambo hili. Alikuwa ameghadhibika sana hata akamweka gerezani. Wakati huo huo Asa akaanza kuwatesa na kuwaonea baadhi ya watu kwa ukatili.
11 Tazma, matendo ya Asa, kutoka mwanzo hadi mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
Matukio ya utawala wa Asa, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
12 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipata ugnjwa kwenye miguu yake; ugonjwa wake ulikuwa mkali sana. Hata hivyo, hakutafuta msaada kutoka kwa Yahwe, lakini kutoka kwa waganga tu.
Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa Bwana bali kwa matabibu tu.
13 Asa akalala pamoja na babu zake; alikufa katika mwaka wa arobaiani na moja wa utawala wake. Wakamzika katika kaburi lake, ambalo alilichimba mwenyewe katika mji wa Daudi.
Katika mwaka wa arobaini na moja wa utawala wa Asa, alikufa na kulala na baba zake.
14 Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.
Nao wakamzika katika kaburi lile alilokuwa amejichongea mwenyewe katika Mji wa Daudi. Wakamzika kwa jeneza lililowekwa vikolezi na mchanganyiko wa manukato ya aina mbalimbali yaliyotengenezwa kwa utaalamu wa mtengeneza marashi, nao wakawasha moto mkubwa kwa heshima yake.