< 2 Nyakati 12 >

1 Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe—na Waisraeli wote pamoja naye.
ויהי כהכין מלכות רחבעם וכחזקתו עזב את תורת יהוה וכל ישראל עמו׃
2 Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalelemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe.
ויהי בשנה החמישית למלך רחבעם עלה שישק מלך מצרים על ירושלם כי מעלו ביהוה׃
3 Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapand farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamaoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia.
באלף ומאתים רכב ובששים אלף פרשים ואין מספר לעם אשר באו עמו ממצרים לובים סכיים וכושים׃
4 Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu.
וילכד את ערי המצרות אשר ליהודה ויבא עד ירושלם׃
5 Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, “Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki”.
ושמעיה הנביא בא אל רחבעם ושרי יהודה אשר נאספו אל ירושלם מפני שישק ויאמר להם כה אמר יהוה אתם עזבתם אתי ואף אני עזבתי אתכם ביד שישק׃
6 Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, “Yahwe ni mtakatifu.”
ויכנעו שרי ישראל והמלך ויאמרו צדיק יהוה׃
7 Yaahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, “Wamejinyenyekeza. Stawaadhibu; nitawaokoa kwa hataua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.
ובראות יהוה כי נכנעו היה דבר יהוה אל שמעיה לאמר נכנעו לא אשחיתם ונתתי להם כמעט לפליטה ולא תתך חמתי בירושלם ביד שישק׃
8 Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine.”
כי יהיו לו לעבדים וידעו עבודתי ועבודת ממלכות הארצות׃
9 Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Selemani. Mfalme
ויעל שישק מלך מצרים על ירושלם ויקח את אצרות בית יהוה ואת אצרות בית המלך את הכל לקח ויקח את מגני הזהב אשר עשה שלמה׃
10 Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikoni mwa maamrijeshi wa walinzi, amabao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.
ויעש המלך רחבעם תחתיהם מגני נחשת והפקיד על יד שרי הרצים השמרים פתח בית המלך׃
11 Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.
ויהי מדי בוא המלך בית יהוה באו הרצים ונשאום והשבום אל תא הרצים׃
12 Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda.
ובהכנעו שב ממנו אף יהוה ולא להשחית לכלה וגם ביהודה היה דברים טובים׃
13 Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka aroabaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa mika kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina lake aliitwa Naama, Mwamoni.
ויתחזק המלך רחבעם בירושלם וימלך כי בן ארבעים ואחת שנה רחבעם במלכו ושבע עשרה שנה מלך בירושלם העיר אשר בחר יהוה לשום את שמו שם מכל שבטי ישראל ושם אמו נעמה העמנית׃
14 Akafanya yaliyokuwa uovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe.
ויעש הרע כי לא הכין לבו לדרוש את יהוה׃
15 Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayakuandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu?
ודברי רחבעם הראשנים והאחרונים הלא הם כתובים בדברי שמעיה הנביא ועדו החזה להתיחש ומלחמות רחבעם וירבעם כל הימים׃
16 Rehoboamu akalala pamoja na babu zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanye akawa mfalme katika nafasi yake.
וישכב רחבעם עם אבתיו ויקבר בעיר דויד וימלך אביה בנו תחתיו׃

< 2 Nyakati 12 >