< 2 Nyakati 10 >

1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa maana Isaraeli wote walikuwa wanakauja Shekemu kwa ajili ya kumfanya yeye mfalme.
Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme.
2 Ikatokea kwamba Yeroboamu mwana wa Nebati akasikia haya (kwa maana alikuwa katika Misiri, ambako alikuw amekimbilia kutoka kwenye uwepo wa Mfalme Selemanai, lakini Yeroboamu akarudi kutoka Misiri).
Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri.
3 Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema,
Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia,
4 “Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikia wewe.”
“Baba yako aliweka nira nzito, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.”
5 Rehoboamu akawaambia, “Njoni kwangu tena baada ya siku tatu.” Kwa hiyo watu wakaondoka.
Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao.
6 Mfalme Rehoboamu akaomba ushauri kwa wazee ambao walikuwa wamesimama mbele ya Selemani baba yake wakati alipokuwa hai; akasema, Mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?”
Kisha Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee ambao walimtumikia Solomoni baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri nini katika kuwajibu watu hawa?”
7 Wakasema kwake, Ikiwa wewe ni mwema kwa watu hawa na uwapendeze, na sema maneno mazuri kwao, basi siku zote watakuwa watumishi wako.”
Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.”
8 Lakini Rehoboamu akapuuza ushauri wa wazee ambao walimpa, na akashauriana na wanauame vijana ambao walikuwa wa rika lake, ambao walisimama mbele yake.
Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia.
9 Akawaamabia, “Mnanipa ushauri gani, ili kwamba niwajibu watu waliozungumza kwangu na kusema, “Ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu'?”
Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu?’”
10 Wanaume vijana mabaoa walikuwa rika la Yeroboamu wakasema kwake, wakisema, “Hivi ndivyo utakavyosema kwa watu waliokuambia kwamba baba yako Selemani aliifanya nira yao nzito, lakini kwamba lazima uifanye nyepesi. Hivi ndivyo utakavyosema kwao, 'Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Waambie watu hawa waliokuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ kuwa, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
11 Kwa hiyo sasa, ingawa babab yangu aliwatwika nira nzito, nitaiongeza nira yenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini nitawaadhibu kwa nge.”
Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi; mimi nitawachapa kwa nge.’”
12 Kwa hiyo Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu katika siku ya tatu, kama aliavyosema mfalme, “Rudini kwangu katika siku ya tatu,”
Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.”
13 Yeroboamu akasema kwa kwao kwa ukatili, akiupuuza aushauri wa wazee.
Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee,
14 Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, “Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.”
akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.”
15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa lilikuw tukio lililoletwa na Mungu, kwamba Yahwe aweze kulitimiza neno lake ambalo Ahiya Mshiloni alikuwa amemwambia Yeroboamu mwana wa Nebati.
Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa Mungu ili kutimiza neno ambalo Bwana alikuwa amenena kwa Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia Ahiya Mshiloni.
16 Israeli wote, walipoona kwamba mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu na kusema, “Tunasehemu gani katika Daudi? Hatuna urith katika wana wa Yese! Kila mmoja wenu anapaswa kwenda katika hema yake, Israeli. Sasa kila mtu aone nyumba yake, Daudi.” Kwa hiyo Israeli wote wakarudi kwenye hema zao.
Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme: “Tuna fungu gani kwa Daudi? Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese. Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli, angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!” Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao.
17 Lakini kwa watu wa Yuda walioishi katika miji ya Yuda, Yeroboamu akatawala juu yao.
Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado.
18 Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa wafanya kazi, lakini watu wa Israeli walimuua kwa kumpiga mawe. Mfalame Rehoboamu akaingia haraka ndani ya gari lake kwenda Yerusalemu.
Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu.
19 Kwa hiyo Israeli wakawa waasi dhidi ya nyumba ya Mungu hadi leo.
Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo.

< 2 Nyakati 10 >