< 1 Timotheo 6 >
1 Wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote, wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe.
Robovi koji su god pod jarmom da pokazuju svaku èast svojijem gospodarima, da se ne huli na ime Božije i na nauku.
2 Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.
A koji imaju krštene gospodare, da ne postaju nemarljivi za njih što su braæa, nego još bolje da služe, jer su vjerni i ljubazni, zajednièari u blagodati. Ovo uèi i svjetuj.
3 Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa.
Ako li ko drukèije uèi, i ne pristaje na zdrave rijeèi Gospoda našega Isusa Hrista i na nauku pobožnu,
4 Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya,
Nadu se ne znajuæi ništa, nego bolujuæi od zapitkivanja i praznijeh prepiranja, oda šta postaje zavist, svaða, huljenje, zle misli,
5 na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiri”
Zaludna prepiranja onakovijeh ljudi koji imaju um izopaèen i nemaju istine, koji misle da je pobožnost trgovina. Kloni se takovijeh.
6 Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.
Ali jest velika trgovina pobožnost sa zadovoljstvom.
7 Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani.
Jer ništa ne donesosmo na ovaj svijet, dakle ne možemo ništa ni odnijeti.
8 Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.
A kad imamo hranu i odjeæu, ovijem da budemo dovoljni.
9 Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.
A koji hoæe da se obogate oni upadaju u napasti i zamke, i u mnoge lude škodljive želje, koje potapaju èovjeka u propast i pogibao.
10 Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.
Jer je korijen sviju zala srebroljublje kojemu neki predavši se zaðoše od vjere i na sebe navukoše muke velike.
11 Lakini wewe mtu wa Mungu, yakimbie mambo hayo. Fuata haki, utauwa, uaminifu, upendo, usitahimilivu, na upole.
A ti, o èovjeèe Božij! bjegaj od ovoga, a idi za pravdom, pobožnosti, vjerom, ljubavi, trpljenjem, krotosti.
12 Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema. (aiōnios )
Bori se u dobroj borbi vjere, muèi se za vjeèni život na koji si i pozvan, i priznao si dobro priznanje pred mnogijem svjedocima. (aiōnios )
13 Nakupa amri hii mbele za Mungu, anayesababisha vitu vyote kuishi, na mbele ya Yesu Kristo, aliyenena iliyo kweli kwa Pontio Pilato:
Zapovijedam ti pred Bogom koji sve oživljuje, i Hristom Isusom koji svjedoèi za vladanja Pontija Pilata dobro priznanje,
14 itunze amri kwa ukamilifu, pasipo mashaka, hadi ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Da držiš zapovijest èistu i nezazornu do dolaska Gospoda našega Isusa Hrista,
15 Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza.
Koji æe u svoje vrijeme pokazati blaženi i jedini silni car nad carevima i gospodar nad gospodarima,
16 Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiriwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina. (aiōnios )
Koji sam ima besmrtnost, i živi u svjetlosti kojoj se ne može pristupiti, kojega niko od ljudi nije vidio, niti može vidjeti, kojemu èast i država vjeèna. Amin. (aiōnios )
17 Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie. (aiōn )
Bogatima na ovome svijetu zapovijedaj da se ne ponose niti uzdaju u bogatstvo propadljivo, nego u Boga živoga, koji nam sve daje izobilno za užitak; (aiōn )
18 Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa.
Neka dobro èine, neka se bogate u dobrijem djelima, neka budu podašni, zajednièni,
19 Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.
Sabirajuæi sebi temelj dobar za unapredak, da prime život vjeèni.
20 Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yenye kujipinga ambayo kwa kwa uongo huitwamaarifa.
O Timotije! saèuvaj što ti je predano, kloni se poganijeh praznijeh razgovora i prepiranja lažno nazvanoga razuma,
21 Baadhi ya watu huyatangaza mambo haya, na hivyo wameikosa imani. Neema na iwe pamoja nawe.
Kojijem se neki hvaleæi otpadoše od vjere. Blagodat s tobom. Amin.