< 1 Wathesalonike 3 >
1 Kwa hiyo, tulipo kuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuwa vema kubaki kule Athene peke yetu.
Kwa hivyo tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliamua tubaki Athene peke yetu.
2 Tulimtuma Timotheo, ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika injili ya Kristo, kuwaimalisha na kuwafariji kuhusiana na imani yenu.
Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi mwenzetu wa Mungu katika kuieneza Injili ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo katika imani yenu,
3 Tulifanya haya ili kusudi asiwepo yeyote wa kuteteleka kutokana na mateso haya, kwa kuwa wenyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili.
ili mtu yeyote asifadhaishwe na mateso haya. Mnajua vyema kwamba tumewekewa hayo mateso.
4 Kwa kweli, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitangulia kuwaeleza ya kuwa tulikuwa karibu kupata mateso, na hayo yalitokea kama mjuavyo.
Kwa kweli, tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa na imekuwa hivyo kama mjuavyo.
5 Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma ilikusudi nipate kujua juu ya imani yenu. Huenda mjaribu alikuwa angalau amewajaribu, na kazi yetu ikawa ni bure.
Kwa sababu hii nilipokuwa siwezi kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.
6 Lakini Timotheo alikuja kwetu kutokea kwenu na akatuletea habari njema juu ya imani na upendo wenu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu yetu, na kuwa mnatamani kutuona kama ambavyo nasi twatamani kuwaona ninyi.
Lakini sasa Timotheo ndiyo tu amerejea kwetu kutoka kwenu na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.
7 Kwa sababu hii, ndugu tulifarijika sana na ninyi kwa sababu ya imani yenu, katika taabu na mateso yetu yote.
Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu.
8 Kwa sasa tunaishi, kama mkisimama imara kwa Bwana,
Sasa kwa kuwa hakika tunaishi, kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana.
9 Kwani ni shukurani zipi tumpe Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tuliyonayo mbele za Mungu juu yenu?
Je, tutawezaje kumshukuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu?
10 Tunaomba sana usiku na mchana ili tuweze kuziona nyuso zenu na kuwaongezea kinachopungua katika imani yenu.
Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tupate kuwaona tena na kujaza kile kilichopungua katika imani yenu.
11 Mungu wetu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia yetu tufike kwenu.
Basi Mungu wetu na Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Yesu atengeneze njia ya sisi kuja kwenu.
12 Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi katika pendo, mkipendana na kuwapenda watu wote, kama tunavyowafanyia ninyi.
Bwana na auongeze upendo wenu na kuuzidisha kati yenu na kwa wengine wote, kama vile tulivyo na upendo mwingi kwenu.
13 Na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu na Baba yetu katika ujio wa Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
Tunamwomba Mungu aimarishe mioyo yenu ili msiwe na lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu aliye Baba yetu wakati wa kuja kwake Bwana Yesu pamoja na watakatifu wote.