< 1 Samweli 22 >
1 Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko.
大卫就离开那里,逃到亚杜兰洞。他的弟兄和他父亲的全家听见了,就都下到他那里。
2 Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye.
凡受窘迫的、欠债的、心里苦恼的都聚集到大卫那里;大卫就作他们的头目,跟随他的约有四百人。
3 Kisha Daudi alitoka huko akaenda Mispa huko Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, “Tafadhali waruhusu baba na mama yangu wakae kwako hadi hapo nitakapojua kitu gani ambacho Mungu atafanya kwa ajili yangu.”
大卫从那里往摩押的米斯巴去,对摩押王说:“求你容我父母搬来,住在你们这里,等我知道 神要为我怎样行。”
4 Basi akawaacha kwa Mfalme wa Moabu. Baba na mama yake wakakaa na mfalme kwa muda wote ambao Daudi alikuwa kwenye ngome yake.
大卫领他父母到摩押王面前。大卫住山寨多少日子,他父母也住摩押王那里多少日子。
5 Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae tena katika ngome yako. Ondoka na uende katika nchi ya Yuda.” Kwa hiyo Daudi akatoka hapo na akaenda katika msitu wa Harethi.
先知迦得对大卫说:“你不要住在山寨,要往犹大地去。”大卫就离开那里,进入哈列的树林。
6 Sauli akasikia kwamba Daudi amepatikana, akiwa pamoja na watu aliokuwa nao. Wakati huo Sauli alikuwa akikaa Gibea chini ya mti wa mkwaju huko Rama, akiwa na mkuki wake mkononi mwake, na watumishi wake wote walikuwa wamesimama wamemzunguka.
扫罗在基比亚的拉玛,坐在垂丝柳树下,手里拿着枪,众臣仆侍立在左右。扫罗听见大卫和跟随他的人在何处,
7 Sauli akawaambia watumishi wake, Sasa sikilizeni, watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya nyote kuwa majemedari wa maelfu na majemedari wa mamia,
就对左右侍立的臣仆说:“便雅悯人哪,你们要听我的话!耶西的儿子能将田地和葡萄园赐给你们各人吗?能立你们各人作千夫长百夫长吗?
8 hata ninyi nyote mnapanga njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anafanya agano na mwana wa Yese. Hakuna hata mmoja wenu anayenionea huruma. Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anamchochea mtumishi wangu Daudi awe kinyume changu. Leo mejificha na ananisubiri ili anishambulie.”
你们竟都结党害我!我的儿子与耶西的儿子结盟的时候,无人告诉我;我的儿子挑唆我的臣子谋害我,就如今日的光景,也无人告诉我,为我忧虑。”
9 Kisha Doegi Mwedomu, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akajibu, Nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu.
那时以东人多益站在扫罗的臣仆中,对他说:“我曾看见耶西的儿子到了挪伯,亚希突的儿子亚希米勒那里。
10 Alimwomba BWANA ili apate kumsaidia, na alimpatia mahitaji na upanga wa Goliathi, Mfilisti”
亚希米勒为他求问耶和华,又给他食物,并给他杀非利士人歌利亚的刀。”
11 Kisha Mfalme akamtuma mtu amwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu na watu wote wa nyumba ya baba yake, makuhani waliokuwa huko Nobu. Wote walifika mbele ya mfalme.
王就打发人将祭司亚希突的儿子亚希米勒和他父亲的全家,就是住挪伯的祭司都召了来;他们就来见王。
12 Sauli akasema, “Sasa sikiliza, mwana wa Ahitubu,” Naye akajibu, “Niko hapa, bwana wangu.”
扫罗说:“亚希突的儿子,要听我的话!”他回答说:“主啊,我在这里。”
13 Sauli akamwambia, “Kwa nini unapanga njama dhidi yangu, wewe pamoja na mwana wa Yese, kwa kumpatia mikate, na upanga, na umemwomba Mungu kusudi amsaidie Daudi, kusudi aniasi mimi, na kujificha sehemu ya siri, kama alivyofanya leo?”
扫罗对他说:“你为什么与耶西的儿子结党害我,将食物和刀给他,又为他求问 神,使他起来谋害我,就如今日的光景?”
14 Ndipo Ahimeleki akamjibu mfalme na kusema, “Je, ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliyemwaminifu kama Daudi, ni nani mkwe wa mfalme na yuko juu ya walinzi wako, na mwenye heshima nyumbani mwako?
亚希米勒回答王说:“王的臣仆中有谁比大卫忠心呢?他是王的女婿,又是王的参谋,并且在王家中是尊贵的。
15 Je, leo ni mara ya kwanza kwangu kumuomba Mungu apate kumsaidia? Hapana! Mfalme usinilaumu mimi mtumishi wako kwa jambo lolote wala jamaa zangu wote. Maana mimi mtumishi wako sijui lolote kuhusu kadhia hii.”
我岂是从今日才为他求问 神呢?断不是这样!王不要将罪归我和我父的全家;因为这事,无论大小,仆人都不知道。”
16 Mfalme akamjibu, “Hakika utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya nyumba ya baba yako.”
王说:“亚希米勒啊,你和你父的全家都是该死的!”
17 Mfalme akamwambia mlinzi aliyesimama karibu naye, “Geuka na uwauwe makuhani wa BWANA. Kwa sababu wanamuunga mkono Daudi, na sababu walijua kwamba alikimbia, lakini hawakunijulisha.” Lakini watumishi wa mfalme hawakunyoosha mkono wao kuwaua makuhani wa BWANA.
王就吩咐左右的侍卫说:“你们去杀耶和华的祭司;因为他们帮助大卫,又知道大卫逃跑,竟没有告诉我。”扫罗的臣子却不肯伸手杀耶和华的祭司。
18 Ndipo mfalme akamwambia Doegi, “Geuka na uwauwe makuhani.” Hivyo Doegi Mwedomu akageuka na kuwapiga makuhani; akawaua watu themanini na watano waliovaa naivera ya kitani siku hiyo.
王吩咐多益说:“你去杀祭司吧!”以东人多益就去杀祭司,那日杀了穿细麻布以弗得的八十五人;
19 Kwa ncha ya upanga, aliupiga Nobu, mji wa makuhani, akiwaua wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na punda na kondoo. Wote aliwaua kwa ncha ya upanga.
又用刀将祭司城挪伯中的男女、孩童、吃奶的,和牛、羊、驴尽都杀灭。
20 Lakini mmoja wa wana wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari, aliponyoka na kukimbilia kwa Daudi.
亚希突的儿子亚希米勒有一个儿子,名叫亚比亚他,逃到大卫那里。
21 Abiathari akamwambia Daudi kwamba Sauli amewaua manabii wa BWANA.
亚比亚他将扫罗杀耶和华祭司的事告诉大卫。
22 Daudi akamwambia Abiathari, “Nilifahamu kuwa siku hiyo, Doegi Mwedomu alikuwa mahali pale, kwamba hakika angemwambia Sauli. Nina wajibika kwa kifo cha kila mtu katika familia ya baba yako!
大卫对亚比亚他说:“那日我见以东人多益在那里,就知道他必告诉扫罗。你父的全家丧命,都是因我的缘故。
23 Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami.”
你可以住在我这里,不要惧怕。因为寻索你命的就是寻索我的命;你在我这里可得保全。”