< 1 Petro 4 >
1 Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni silaha za nia ile ile. Yeye aliyeteseka katika mwili ameondokana na dhambi.
Christo igitur passo in carne, et vos eadem cogitatione armamini: quia qui passus est in carne, desiit a peccatis:
2 Mtu huyu haendelei tena kuishi katika tamaa za mwili, bali kwa mapenzi ya Mungu, kwa maisha yake yaliyosalia.
Ut iam non desideriis hominum, sed voluntati Dei, quod reliquum est in carne vivat temporis.
3 Kwa kuwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo.
Sufficit enim præteritum tempus ad voluntatem Gentium consummandam his, qui ambulaverunt in luxuriis, desideriis, vinolentiis, comessationibus, potationibus, et illicitis idolorum cultibus.
4 Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu.
In quo admirantur non concurrentibus vobis in eamdem luxuriæ confusionem, blasphemantes.
5 Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu.
Qui reddent rationem ei, qui paratus est iudicare vivos et mortuos.
6 Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho.
Propter hoc enim et mortuis evangelizatum est: ut iudicentur quidem secundum homines in carne, vivant autem secundum Deum in Spiritu.
7 Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu.
Omnium autem finis appropinquavit. Estote itaque prudentes, et vigilate in orationibus.
8 Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.
Ante omnia autem, mutuam in vobismetipsis charitatem continuam habentes: quia charitas operit multitudinem peccatorum.
9 Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika.
Hospitales invicem sine murmuratione:
10 Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu.
Unusquisque, sicut accepit gratiam, in alterutrum illam administrantes, sicut boni dispensatores multiformis gratiæ Dei.
11 Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina. (aiōn )
Si quis loquitur, quasi sermones Dei: si quis ministrat, tamquam ex virtute, quam administrat Deus: ut in omnibus honorificetur Deus per Iesum Christum: cui est gloria, et imperium in sæcula sæculorum: Amen. (aiōn )
12 Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu.
Charissimi, nolite peregrinari in fervore, qui ad tentationem vobis fit, quasi novi aliquid vobis contingat:
13 Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.
sed communicantes Christi passionibus gaudete, ut et in revelatione gloriæ eius gaudeatis exultantes.
14 Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.
Si exprobramini in nomine Christi, beati eritis: quoniam quod est honoris, gloriæ, et virtutis Dei, et qui est eius Spiritus, super vos requiescit.
15 Lakini asiwepo yeyote mwenye kuteswa kama muuaji, mwizi, mtenda maovu, au ajishughulishaye na mambo ya wengine.
Nemo autem vestrum patiatur ut homicida, aut fur, aut maledicus, aut alienorum appetitor.
16 Lakini ikiwa mtu anateswa kama Mkristo, asione aibu, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Si autem ut Christianus, non erubescat: glorificet autem Deum in isto nomine.
17 Kwa kuwa wakati umefika kwa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Na kama inaanzia kwetu, itakuwaje kwa wale wasioitii injili ya Mungu?
Quoniam tempus est ut incipiat iudicium a domo Dei. Si autem primum a nobis: quis finis eorum, qui non credunt Dei Evangelio?
18 Na kama “mwenye haki anaokolewa kupitia magumu, itakuwaje kwa mtu asiyehaki na mwenye dhambi?”
Et si iustus vix salvabitur, impius, et peccator ubi parebunt?
19 Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.
Itaque et hi, qui patiuntur secundum voluntatem Dei, fideli Creatori commendent animas suas in benefactis.