< 1 Petro 3 >
1 Kwa njia hii, ninyi ambao ni wake mnapaswa kujitoa kwa waume zenu wenyewe, ili, hata kama baadhi yao hawajalitii neno, kupitia tabia za wake zao wanaweza kuvutwa pasipo neno,
LIKEWISE, ye wives, be in subjection to your own husbands; that, if any obey not the word, they also may without the word be won by the conversation of the wives;
2 kwa sababu wao wenyewe watakuwa wameiona tabia yenu njema pamoja na heshima.
While they behold your chaste conversation coupled with fear.
3 Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.
Whose adorning let it not be that outward adorning of plaiting the hair, and of wearing of gold, or of putting on of apparel;
4 Lakini badala yake ifanyike kwa utu wa ndani wa moyo, na kuzidi katika uzuri wa unyenyekevu na utulivu wa moyo, ambao ni wa thamani mbele za Mungu.
But let it be the hidden man of the heart, in that which is not corruptible, even the ornament of a meek and quiet spirit, which is in the sight of God of great price.
5 Kwa kuwa wanawake watakatifu walijipamba wenyewe kwa njia hii. Walikuwa na imani katika Mungu na waliwatii waume zao wenyewe.
For after this manner in the old time the holy women also, who trusted in God, adorned themselves, being in subjection unto their own husbands:
6 Kwa njia hii Sara alimtii Ibrahamu na kumwita yeye “bwana” wake. Ninyi sasa ni watoto wake kama mtafanya yaliyo mazuri na kama hamwogopi mabaya.
Even as Sara obeyed Abraham, calling him lord: whose daughters ye are, as long as ye do well, and are not afraid with any amazement.
7 Kwa njia hiyo hiyo, ninyi wanaume mnapaswa kuishi na wake zenu mkijua kuwa wao ni wenzi wa kike dhaifu, mkiwatambua wao kama wapokeaji wenzenu wa zawadi ya uzima. Fanyeni hivi ili kwamba maombi yenu yasizuiliwe.
Likewise, ye husbands, dwell with them according to knowledge, giving honour unto the wife, as unto the weaker vessel, and as being heirs together of the grace of life; that your prayers be not hindered.
8 Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.
Finally, be ye all of one mind, having compassion one of another, love as brethren, be pitiful, be courteous:
9 Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.
Not rendering evil for evil, or railing for railing: but contrariwise blessing; knowing that ye are thereunto called, that ye should inherit a blessing.
10 “Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.
For he that will love life, and see good days, let him refrain his tongue from evil, and his lips that they speak no guile:
11 Na ageuke na kuacha mabaya na kufanya yaliyo mazuri. Atafute amani na kuifuata.
Let him eschew evil, and do good; let him seek peace, and ensue it.
12 Macho ya Bwana humwona mwenye haki na masikio yake husikia maombi yake. Lakini uso wa Bwana uko kinyume cha wale watendao uovu.”
For the eyes of the Lord are over the righteous, and his ears are open unto their prayers: but the face of the Lord is against them that do evil.
13 Ni nani atakayewadhuru ninyi, ikiwa mwatamani lililo zuri?
And who is he that will harm you, if ye be followers of that which is good?
14 Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.
But and if ye suffer for righteousness’ sake, happy are ye: and be not afraid of their terror, neither be troubled;
15 Badala yake, mmuweke Kristo Bwana katika mioyo yenu kama mtakatifu. Kila mara muwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza ninyi kwa nini mna tumaini katika Mungu. Fanyeni hivi kwa upole na heshima.
But sanctify the Lord God in your hearts: and be ready always to give an answer to every man that asketh you a reason of the hope that is in you with meekness and fear:
16 Muwe na dhamiri njema ili kwamba watu wanaotukana maisha yenu mema katika Kristo waweze kuaibika kwa sababu wanaongea kinyume dhidi yenu kama kwamba mlikuwa watenda maovu.
Having a good conscience; that, whereas they speak evil of you, as of evildoers, they may be ashamed that falsely accuse your good conversation in Christ.
17 Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.
For it is better, if the will of God be so, that ye suffer for well doing, than for evil doing.
18 Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi. Yeye ambaye ni mwenye haki aliteseka kwa ajili yetu, ambao hatukuwa wenye haki, ili kwamba atulete sisi kwa Mungu. Alikufa katika mwili, lakini alifanywa mzima katika roho.
For Christ also hath once suffered for sins, the just for the unjust, that he might bring us to God, being put to death in the flesh, but quickened by the Spirit:
19 Katika roho, alikwenda na kuzihubiri roho ambazo sasa ziko kifungoni.
By which also he went and preached unto the spirits in prison;
20 Hazikuwa tiifu wakati uvumilivu wa Mungu ulipokuwa unasubiri wakati wa Nuhu, siku za ujenzi wa safina, na Mungu aliokoa watu wachache—nafsi nane—kutoka katika maji.
Which sometime were disobedient, when once the longsuffering of God waited in the days of Noah, while the ark was a preparing, wherein few, that is, eight souls were saved by water.
21 Hii ni alama ya ubatizo unaowaokoa ninyi sasa, siyo kama kuosha uchafu kutoka mwilini, lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo.
The like figure whereunto even baptism doth also now save us (not the putting away of the filth of the flesh, but the answer of a good conscience toward God, ) by the resurrection of Jesus Christ:
22 Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu. Alikwenda mbinguni. Malaika, mamlaka, na nguvu lazima vimtii yeye.
Who is gone into heaven, and is on the right hand of God; angels and authorities and powers being made subject unto him.