< 1 Wafalme 9 >

1 Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya,
所羅門建造耶和華殿和王宮,並一切所願意建造的都完畢了,
2 BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni.
耶和華就二次向所羅門顯現,如先前在基遍向他顯現一樣,
3 Na BWANA akamwambia, “Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote.
對他說:「你向我所禱告祈求的,我都應允了。我已將你所建的這殿分別為聖,使我的名永遠在其中;我的眼、我的心也必常在那裏。
4 Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu,
你若效法你父大衛,存誠實正直的心行在我面前,遵行我一切所吩咐你的,謹守我的律例典章,
5 ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikiseama, 'uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli.
我就必堅固你的國位在以色列中,直到永遠,正如我應許你父大衛說:『你的子孫必不斷人坐以色列的國位。』
6 Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujidia,
倘若你們和你們的子孫轉去不跟從我,不守我指示你們的誡命律例,去事奉敬拜別神,
7 basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote.
我就必將以色列人從我賜給他們的地上剪除,並且我為己名所分別為聖的殿也必捨棄不顧,使以色列人在萬民中作笑談,被譏誚。
8 Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, 'Kwa nini BWANA amefanya hili katika chi hii na kwa nyumba hii?'
這殿雖然甚高,將來經過的人必驚訝、嗤笑,說:『耶和華為何向這地和這殿如此行呢?』
9 Na wengine watajibu, 'Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote.”
人必回答說:『是因此地的人離棄領他們列祖出埃及地之耶和華-他們的上帝,去親近別神,事奉敬拜他,所以耶和華使這一切災禍臨到他們。』」
10 Ilitokea mwishoni mwa miaka ishirini, Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga majengo yote mawili, hekalu la BWANA na ikulu ya mfalme.
所羅門建造耶和華殿和王宮,這兩所二十年才完畢了。
11 Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoa na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya.
泰爾王希蘭曾照所羅門所要的,資助他香柏木、松木,和金子;所羅門王就把加利利地的二十座城給了希蘭。
12 Hiramu akaja kutoka Tiro kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempatia, lakini hakupendezwa nayo.
希蘭從泰爾出來,察看所羅門給他的城邑,就不喜悅,
13 Kwa hiyo Hiramu akasema, “Ndugu yangu, ni miji gani hii uliynipatia? Hiramu akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo.
說:「我兄啊,你給我的是甚麼城邑呢?」他就給這城邑之地起名叫迦步勒,直到今日。
14 Hiramu alikuwa amemtumia mfalme tani nne za dhahabu.
希蘭給所羅門一百二十他連得金子。
15 Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari.
所羅門王挑取服苦的人,是為建造耶和華的殿、自己的宮、米羅、耶路撒冷的城牆、夏瑣、米吉多,並基色。
16 Farao mfalme wa Misri alikuwa ameenda kuitwaa Gezeri, akaichoma moto, na kuwaua Wakanaani katika mji. Kisha Farao akampatia binti yake ule mji, mke wa Sulemani kuwa zawadi ya arusi.
先前埃及王法老上來攻取基色,用火焚燒,殺了城內居住的迦南人,將城賜給他女兒所羅門的妻作妝奩。
17 Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri na Bethi Horoni ya Loweri,
所羅門建造基色、下伯‧和崙、
18 Baalathi na Tamari jangwani katika nchi ya Yuda,
巴拉,並國中曠野裏的達莫,
19 na miji yote ya hazina yote iliyokuwa yake, na miji ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na hata kama alipenda kuijenga kwa ajili ya fahari yake kule Yerusalemu, Lebanoni, na katika nchi yote kwenye utawala wake.
又建造所有的積貨城,並屯車和馬兵的城,與耶路撒冷、黎巴嫩,以及自己治理的全國中所願建造的。
20 Na kwa watu wote waliokuwa wamesalia wa Waamori, Wahiti, Waperezi, Wahivi, na Yebu, ambao hawakuwa Waisraeli,
至於國中所剩下不屬以色列人的亞摩利人、赫人、比利洗人、希未人、耶布斯人,
21 na uzao wao waliokuwa wamesalia baada yao katika nchi, ambao Waisraeli hawakuweza kuwaangamiza kabisa - Sulemani akawafanya kuwa vibarua, ambao wako hata leo.
就是以色列人不能滅盡的,所羅門挑取他們的後裔作服苦的奴僕,直到今日。
22 Hata hivyo, Sulemani hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli. Badala yake, walifanyika kuwa wanajeshi wake na watumishi wake, maakida wake, na wakuu wake, na majemedari wake na wapanda farasi wake.
惟有以色列人,所羅門不使他們作奴僕,乃是作他的戰士、臣僕、統領、軍長、車兵長、馬兵長。
23 Hawa ndio waliokuwa maakida wakuu waliokuwa wakiwasimamia kazi za Sulemani, watu 550, walikuwa wasimamizi wa watu waliokuwa wakifanya kazi.
所羅門有五百五十督工的,監管工人。
24 Binti wa Farao alihama kutoka mji wa Daudi kwenda kwenye ile nyumba ambayo Sulemani alimjengea. Baadaye, Sulemani akaijenga Milo.
法老的女兒從大衛城搬到所羅門為她建造的宮裏。那時,所羅門才建造米羅。
25 Mara tatu kwa kila mwaka Sulemani alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani katika madhabahu ambayo alimjengea BWANA, akifukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu ilyokuwa mbele ya BWANA. Kwa hiyo akalimalizia hekalu na sasa alikuwa akilitumia.
所羅門每年三次在他為耶和華所築的壇上獻燔祭和平安祭,又在耶和華面前的壇上燒香。這樣,他建造殿的工程完畢了。
26 Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.
所羅門王在以東地紅海邊,靠近以祿的以旬‧迦別製造船隻。
27 Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.
希蘭差遣他的僕人,就是熟悉泛海的船家,與所羅門的僕人一同坐船航海。
28 Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14. 5 za dhahabu kwa Sulemani.
他們到了俄斐,從那裏得了四百二十他連得金子,運到所羅門王那裏。

< 1 Wafalme 9 >