< 1 Wafalme 6 >

1 Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.
Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana.
2 Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.
Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini, upana wa dhiraa ishirini na kimo cha dhiraa thelathini kwenda juu.
3 Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.
Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu.
4 Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.
Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu.
5 Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote.
Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu.
6 Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2. 3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2. 8. na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3. 2. upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.
Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano, ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba. Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu.
7 Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likjengwa.
Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika sauti yake katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa.
8 Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.
Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu.
9 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi.
Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha, akiliweka paa za boriti na mbao za mierezi.
10 Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.
Mfalme Solomoni akajenga vyumba vya pembeni kuzunguka Hekalu lote. Kimo cha kila kimoja kilikuwa dhiraa tano. Navyo vilikuwa vimeunganishwa na Hekalu kwa boriti za mierezi.
11 Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema,
Neno la Bwana likamjia Solomoni kusema:
12 “Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo ntakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi.
“Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako.
13 Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa.”
Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.”
14 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza.
Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha.
15 Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.
Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari.
16 Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana.
Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu.
17 Ule ukumbu mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua.
Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini.
18 Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.
Hekalu ndani ilikuwa ya mierezi iliyonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.
19 Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA.
Ndani ya Hekalu akatengeneza sehemu takatifu ya ndani, kwa ajili ya kuweka Sanduku la Agano la Bwana.
20 Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.
Sehemu takatifu ya ndani ilikuwa na upana, urefu na kimo cha dhiraa ishirini ndani kwa ndani. Akaifunika ndani kwa dhahabu safi, pia akaifunika madhabahu ya mierezi vivyo hivyo.
21 Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.
Solomoni akaifunika sehemu ya ndani ya Hekalu kwa dhahabu safi, naye akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande moja hadi ule mwingine mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, ambako palifunikwa kwa dhahabu.
22 Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.
Basi akafunika sehemu yote ya ndani kwa dhahabu. Pia akafunika madhabahu yale yaliyokuwa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kwa dhahabu.
23 Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4. 5 kwa ajili ya chumba cha ndani.
Katika Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni, kila moja likiwa na dhiraa kumi kwenda juu.
24 Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2. 3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4. 5. Yule
Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na bawa jingine dhiraa tano, hivyo urefu kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa jingine ulikuwa dhiraa kumi.
25 kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4. 5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo.
Kerubi wa pili alikuwa na urefu wa dhiraa kumi pia, hivyo makerubi hao wawili walifanana kwa vipimo na kwa umbo.
26 Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4. 5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.
Kimo cha kila kerubi kilikuwa dhiraa kumi.
27 Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana.
Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.
28 Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.
Akafunika wale makerubi kwa dhahabu.
29 Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani.
Juu ya kuta zote zilizozunguka Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi zilizokatwa za makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua.
30 Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.
Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu.
31 Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano.
Kwa ingilio la Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza milango ya mbao za mzeituni, zikiwa na miimo na vizingiti vyenye umbo la pembe tano.
32 Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.
Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa.
33 Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne
Kwa njia iyo hiyo akatengeneza miimo yenye pande nne ya miti ya mizeituni, kwa ajili ya ingilio la ukumbi mkubwa.
34 na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia.
Kulikuwa na milango miwili iliyoweza kukunjuka iliyotengenezwa kwa mbao za msunobari na kila mmoja ulikuwa na bawaba ambazo zingeuwezesha kujikunja kila kipande juu ya kingine.
35 Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.
Akanakshi makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua juu yake na kufunika kwa dhahabu iliyonyooshwa vizuri juu ya michoro.
36 Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.
Tena akajenga ua wa ndani safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa.
37 Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv.
Msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano.
38 Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.
Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba.

< 1 Wafalme 6 >